Jifunze kuto-kukata tamaa


Jayspeed

Jayspeed

Senior Member
Joined
Feb 23, 2014
Messages
151
Likes
151
Points
60
Age
24
Jayspeed

Jayspeed

Senior Member
Joined Feb 23, 2014
151 151 60
Je kuna jambo fulani huliwezi tena yaani umeshalifanya mara zaidi ya moja linakushinda na ukasema hulifanyi tena hii inaitwa KUKATA TAMAA
Umeomba kazi kila unapoomba unakosa na ukasema sasa basi siombi kazi tena
Umefanya biashara zaidi ya mara moja ikaanguka ukajiapiza na kusema hufanyi tena?
Yote hayo yanaitwa kukata tamaa
Una ndoto kubwa, Una malengo makubwa, Una mipango mikubwa, lakini kila unachofanya kina feli unaamua kukata tamaa jua kwamba unapishana na utajiri au unapishana na mafanikio
Hupaswi kufanya hivyo, kwanza tambua kukata tamaa ni dhambi na ni dhambi ambayo itakuadhibu na umaskini

Fikiria kipindi Musa anawatoa waisraeli Misri mpaka nchi ya ahadi Kanani, japo yeye hakufika lakini aliwaonyesha njia, vikwazo vingapi alikutana navyo lakini hakukata tamaa alivumilia mpaka mwisho na wana waisraeli wakafika nchi ya ahadi kupitia Musa
Musa angekata tamaa wana waisraeli wangebaki Misri kwa Farao na kuendelea kuteseka..
Nawe jenga mawazo yako kuwa sasa upo sehemu ya mateso kama Misri ile ya Farao unahitaji kutoka ufike Kanani nchi ya ahadi. Je, ungekata tamaa na uendelee kubaki Misri?
Muda mwingine kukata tamaa kuna kuja kuathiri familia yako mbeleni, maana maisha uliokua unataka kuishi si hayo ila kukata kwako tamaa pamekufanya uishi maisha hayo mabaya

Watu hawauzoei umaskini, watu hawautaki umaskini wala kuusikia lakini wanakata tamaa katika kutafuta utajiri wa mafanikio.
Kukata tamaa ni kukosa maarifa, kukosa njia ya pili ya kujikomboa wazungu wanaita PLAN B

Kufeli masomo, kufeli kazi, au kufeli biashara sio uzembe bali uzembe ni kukata tamaa

Hebu mfikirie Moja ya matajiri wakubwa huko china na duniani kwa ujumla JACK MA mmiliki na mwanzilishi wa kampuni ya Alibaba Group kama angekata tamaa ya maisha asingekuwa hapa alipo sasa hivi.
JACK MA baada tu ya kuhitimu masomo yake aliomba kazi tofauti 30 lakini zote alikataliwa , aliomba kazi ya upolisi alikataliwa na kuambiwa hafai kuwa polisi lakini hakukata tamaa fikiria kama angekubaliwa ungekuta leo hii Jack Ma angekuwa anakimbizana na vibaka kule miji ya Shanghai na Hong Kong na asingejulikana leo hii kama mwenyekiti wa Alibaba angekuwa koplo tu lakini kukataliwa kwake palikuwa na sababu..
Katika hizo kazi 30 alizokosa Jack Ma alishawahi kwenda kwenye usahili walikuwa watu 24 baada ya ushahili watu 23 walipata kazi lakini yeye pekee ndio alikosa...jiulize aliumia kiasi gani lakini bado hakukata tamaa aliamini ipo siku alipambana zaidi mpaka mwisho akawa miongoni mwa matajiri wakubwa duniani..

Jifunze kwa Jack Ma na watu wengine wengi waliofanikiwa bila kukata tamaa japo walipitia vikwazo vikubwa, kukata kwako tamaa leo panakuzuia kuwa Jack Ma wa kesho...

Haijalishi itachukua Muda gani kufanikiwa lakini usikate tamaa
Haijalishi itakugharimu kiasi gani usikate tamaa
Haijalishi umechoka kiasi gani usikate tamaa, unapoanza kuchoka ndio unapokaribia mafanikio

Ishi ndoto zako
Pambana mpaka pumzi yako ya mwisho
Mafanikio yapo ka wote ila wote wanaopambana bila kukata tamaa


By Jay Speed
 
Marlex Jr El

Marlex Jr El

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2015
Messages
1,326
Likes
1,465
Points
280
Marlex Jr El

Marlex Jr El

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2015
1,326 1,465 280
Mazingira yetu kwa kiasi kikubwa ndio chanzo cha vijana wengi kukata tamaa mapema...

Viongozi wetu pamoja na wazazi wetu ushindwa kuandaa mazingira yaliyo bora ili kusaidia vijana wasomi na wasio wasomi kuziona fursa sahihi kwa wakati.

Ebu fikiri leo kijana una mwambia afanye kazi lakini akitazama hata kiwanda kimoja japo cha ngozi hakioni... Kilimo chetu pia ni kama sisi ni waharibifu tu wa ardhi ukiachilia mbali ukosefu wa mvua.

Nina uhakika asilimia kubwa ya vijana wa kitanzania ni wabunifu lakini kinacho tuponza ni mazingira yetu hayajaandaliwa kuwa supportive.
 
Jayspeed

Jayspeed

Senior Member
Joined
Feb 23, 2014
Messages
151
Likes
151
Points
60
Age
24
Jayspeed

Jayspeed

Senior Member
Joined Feb 23, 2014
151 151 60
Mazingira yetu kwa kiasi kikubwa ndio chanzo cha vijana wengi kukata tamaa mapema...

Viongozi wetu pamoja na wazazi wetu ushindwa kuandaa mazingira yaliyo bora ili kusaidia vijana wasomi na wasio wasomi kuziona fursa sahihi kwa wakati.

Ebu fikiri leo kijana una mwambia afanye kazi lakini akitazama hata kiwanda kimoja japo cha ngozi hakioni... Kilimo chetu pia ni kama sisi ni waharibifu tu wa ardhi ukiachilia mbali ukosefu wa mvua.

Nina uhakika asilimia kubwa ya vijana wa kitanzania ni wabunifu lakini kinacho tuponza ni mazingira yetu hayajaandaliwa kuwa supportive.
sidhan kama mtu ukiwa mbunifu unakosa soko maana ukiwa mbunifu kila mtu atahitaj kuona ubunifu wako kila mtu anahtaj kutumia ulichobuni.....mazingira sio supportive mazingira yapi unayasemea kwa upande wako?? .....tatizo la vijana wetu ndio ni wabunifu lakini hawataki kuonyesha ubunifu wao hadharani huwez kuwa mbunifu halaf ulalie ubunifu wako ndani ujisifu ww ni mbunifu na kitu cha pili kinachifanya vijana tusionyeshe ubunifu wetu ni kutokujiamini unaona kama utakosea wakati ujafanya wanasema mpango wa kichwani bila kufanya au kuonyesha sio mpango onyesha halaf shindwa useme mpango ulifeli......
 
Nyaka-One

Nyaka-One

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2013
Messages
2,184
Likes
1,971
Points
280
Nyaka-One

Nyaka-One

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2013
2,184 1,971 280
Kuna wakati uwa najiuliza pale Yesu Kristo alipopata mateso na kutundikwa msalabani na yeye kupaza sauti akisema "Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?" naye ilifikia pointi akapoteza imani juu ya Mungu baba hadi kufikia kukata tamaa na kutamka maneno hayo?
 

Forum statistics

Threads 1,235,150
Members 474,353
Posts 29,213,333