Jifunze kuthamini vya kwako

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Habari wanajamvi wenzangu

AWALI YA YOTE WANAJAMVI WENZANGU NIMEINGIA TENA KIDIGITAL NA SIO KIANALOGIA KWA KUWAPA SOMO HILI HAPA, NAJUA KWA WALE WALIO MAKINI WATAFUNDISHIKA ILA KWA WALE WENZANGU NA MIMI WATALETA KASORO ZAO. NAYO SIO MBAYA KWANI NIKUHABARISHANA NA KUSAIDIANA KATIKA JUKWAA LETU. LEO NIMEINGIA HIVI:

WAKATI MWINGINE TWAJIFUNZA VITU KWA KUONA NA KUIGA. NA MAMBO MENGINE HUWEZI KUFANYA BILA KUANGALIA UMUHIMU WA KITU UNACHOTAKA KUKIFANYA KWA WAKATI HUO, JAMII YA SASA INAJIFUNZA VITU KWA KUONA NA KUIGA MAMBO YA MAGHARIBI WANAVYOFANYA, MPAKA IMEPELEKEA KUTOTHAMINI TAMADUNI NA MILA ZETU. VIJANA WENGI WAMEJITUMBUKIZA KATIKA MAMBO YA KISASA NA KUONA HAYO YANAFAA NA KUMBE WANAJIDANGANYA WENYEWE NA KUJIANGAMIZA.

KUTANA NA KITABU CHANGU AMBACHO KIKO MBIONI KUSAMBAA KATIKA MIKOA MBALIMBALI, KIHUSUCHO JICHO LA WOGA. UTAKAPOKISOMA KITABU HIKI KITAKUFUNGUA MACHO YAKO NA KUONA ZAIDI YA VILE UONAVYO SASA, YAANI KUWA NA MTAZAMO HALISIA WA WEWE UFANYE NINI NA KITU GANI UWEZE KUIGA TOKA KWA WENGINE.
HEBU KUWA MTU WA KUTHAMINI VILE VYA NYUMBANI KWAKO YAANI UTAMADUNI WAKO NA SIO KUIGA VITU VISIVYOPENDEZA. WENGINE WANAVAA NGUO NUSU UTUPU, WENGINE WANANY'OA AU KUSUKA STYLE AMBAZO HAZILINGANI NA TAMADUNI ZAO, WENGINE WANAIGA MAMBO AMBAYO HAYAMTUKUZI MUNGU. JE RAFIKI BADO UTAENDELEA KUIGA MPAKA LINI MAMBO YA WENGINE KWANINI USIILETE MAPINDUZI KATIKA TAMADUNI NCHINIK KWAKO, UTAKUWA MTU WA KUIGA MPAKA LINI. UTAKUWA NA KITU GANI CHA KURINGIA KUWA ULIFANYA WEWE NA UKALETA HISTORIA NCHINI KWAKO. KAMA UTAPENDA KUWA MTU WA KUIGA BASI UTAIGA MPAKA WANAVYOKOGA UGHAIBUNI.

NADHANI SASA RAFIKI UTAELEWA UMUHIMU WA KUONA MAMBO YALIYO MAZURI NA KUYAFANYA. JE RAFIKI WEWE UNAJIFUNZA NINI KATIKA KUONA NA KUIGA NIANDIKIE YALE YALIYOKUGUSA NA UKAYATENDA KWA KUONA KWAKO SASA. SAMAHANI KAMA UTAKUWA UMEBOREKA LAKINI UJUMBE UMEKUFIKIA HAPO ULIPO. NAOMBA UNIPENDE KAMA NINAVYOKUPENDA MM RAFIKI

HEBU ANGALIA PICHA HIZI ZIFUATAZO NAMBIE UNA NINI UMEJIFUNZA HAPA,
 

Attachments

  • MAN PUTTING SHEDO.jpeg
    2.8 KB · Views: 282
  • MAN2.jpeg
    2.6 KB · Views: 287
  • wear.jpeg
    3.8 KB · Views: 284
  • HAIR.jpeg
    5.1 KB · Views: 285
ladyfurahia
Hongera kwa kuweka mawazo yako katika kitabu..
::
Wanaoacha asili wanasahau usemi kuwa Titi la mama tamu hata kama la mbwa.
=
 
Last edited by a moderator:
nimeona mengi sana mpaka sasa sijui nichangie lipi na kuacha lipi?
 
napenda mitazamo hii binafsi kuna vitu vinanikera mno huku kuigaiga kunasababisha hata vijana wanataka kuwa kama hawana akili (hebu fikiria kijana kachomeka visikiliza sauti maskioni kwake zaidi ya masaa matatu mfululizo je kuna jipya analoweza kutupa kijana huyu)
big up...sna
 
Hivi jamani kuvaa nguo fupi si ndio utamaduni wa mwafrika, tulikuwa tunavaa nguo za kuficha utupu wetu tu hapo zamani za kale, wazungu wakaja na utamaduni wao wa kuvaa nguo ndefu tumechukua vya wazungu na sasa tunasema wale wanaovaa vimini wanaiga utamaduni wa mzungu. mi nakataa wavaa mini na nguo fupi hao ndio wanatunza mila zetu lol
 
Mimi sielewi kabisa napoona wanawake wamejikandamiza suruali tena Dar kwenye joto kali,mie nilijua wenzetu ughaibuni wanavaa suruali vile kule ni baridi sana hata mie nilazimika kuvaa jeans japo sipendi.

Utu wa mwanamke nijuavyo ni maziwa yake,ukitaka kuhakiki jambo hili uingie sehemu ambako kuna wanawake zaidi ya mmoja wakiwa uchi wengi wataficha maziwa yao,lakini ukiingia kwa wanaume waliouchi wataficha fimbo ya Musa.point yangu ni kuwa inakuwaje mwanamke anaacha maziwa yake sehemu kubwa inaonekana? ni kujionyesha malaya aliye kubuhu hata kama ni mke wa mtu akipata chance tu anafanya vituko.

wanaume nao eti kuvaa heleni? jamani!
 
mbali ya hao ndugu yangu wako wanaoimba kwa nguvu huku wameweka eyephone yaani ni kelele tupu njia nzima na kero kwa wenzake ukimuuliza atakwambia mambo ya mjini haya si ushamba tu
 
umenena vyema mkuu hapo hebu ona hapa si udhalilishaji tunaojionesha jamani eti kuiga kwenda na wakati haaa! jaamani

 

Attachments

  • woman.jpg
    7 KB · Views: 157
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…