Tanzania Nchi Yetu Sote
JF-Expert Member
- Mar 12, 2017
- 529
- 909
Ukijifunza kusema na kusimamia ukweli, jifunze pia kuishi na kusimama peke yako; maana ni kupitia hili hata ndugu,jamaa na Marafiki watakutenga,watakusaliti na labda wanaweweza thubutu kukuua. Hili si JIPYA,Yesu alisalitiwa,alikanwa na kudhihakiwa na wale wale aliokuwanao siku zote za Maisha yake na sababu kubwa na ya Msingi ilikuwa ni kusimamia na kuishi ukweli alioamini achilia mbali kuwa ilikuwa mpango wa MUNGU.
Japo haitakuwa milele; ila Watu wengi Duniani hupenda uongo wa Muda Mfupi ulio na Mateso ya milele kuliko ukweli unaoumiza wa muda mfupi wenye amani ya milele.
Unachopaswa kujua ni namna ya kuituliza akili yako tu maana nafsi inajua nini cha kufanya ili ijiponye yenyewe;ukishindwa au usipokuwa makini na hili ipo Siku utajikuta uko peke yako wakati daima una amini uko na Watu kwa Maelfu wanaokuzunguka unawaita Ndugu,Jamaa na Marafiki kumbe ni vivuli.
Bora ukajifunza hili ukaelewa, ukiamua kusema na kusimamia Ukweli,amua pia kusimama peke yako.