Jifunze kusema Hapana

Jifunze kusema Hapana

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,579
Reaction score
161,430
Katika maisha watu watakufitini, watakurubuni na watakukatisha tamaa. Sema hapana kwa ndiyo nyingi.

Katika maisha watu wengi hawataki kukuona ukiendelea kwa sababu ukiendelea unakuwa kioo kwao. Ghafla wataanza kukutazama. Wanajua wana akili kama wewe, wamesoma kama wewe, au wana akili kuliko wewe, au wamesoma kuliko wewe, na labda wanazijua sifa zako za udhaifu na sifa zako za ushupavu toka utotoni kwako. Lakini ghafla unakuwa kioo, na wanapojitazama katika hicho kioo, wanajiona taswira zao isipokuwa sasa hawapo mahali ambapo wewe upo.

Katika maisha watu watakushauri, watakufitini, watakurubuni na watakukatisha tamaa. Sema hapana kwa ndiyo nyingi kwa sababu hawaoni unachokiona, hawajui unachokifanya na hawajui unapoelekea.

Unachokiona ni takdiri ya maisha yako, unachokifanya ni kupanda mbegu na kuzimwagilia kwa imani, na unapoelekea ni kileleni. Hivyo, songa mbele, kuwa wewe daima, wape muda, wape nafasi.

“Say no to a lot of yeses.” – Enock Maregesi

Mtu akikushauri kufanya kitu ambacho ni kinyume na takdiri (‘destiny’) ya maisha yako, hata kama huyo mtu hana nia mbaya na wewe, sema ‘hapana’ kwa hiyo ‘ndiyo’ yake.
 
Tuko pamoja mkuu
 
Nashukuru kama imeeleweka
Hapana sawa lakini sio kila kitu mfano mzuri rudi kwa Mzee Mugabe yeye hakuamini mawazo ya wengine na alisimamia kile alichokiamini tu bila kujali mawazo ya wengine sasa ameacha legacy ipi kwa kizazi chetu.tukubaliane sio kila mahala useme hapana...
 
Back
Top Bottom