Jifunze kumuacha aende

Zero Competition

JF-Expert Member
Sep 12, 2018
310
451
Katika mahusiano kugombana na kupatana ni kitu cha kawaida sana na ukiona watu wanagombana na wanapatana tambua kwamba neno "nisamehe" limetumika sana.Hakuna mahusiano ambayo hayana changamoto kabisa na ukiona uhusiano wako na mpenzi wako haujawahi kupata changamoto yoyote basi tambua kwamba hapo kuna tatizo mana hata vikombe kabatini vinagongana sembuse nyinyi.Nyinyi sio malaika kusema kwamba kila siku mtakua sahihi na hamtokwazana, kutofautiana kupo na ndio maana kukawepo na neno "samahani"

Kuna wakati inafikia mmoja wenu anakua mgumu sana kutoa msamaha ili mambo yaendelee kuwa kama awali hata kama ameombwa kufanya hivyo na mwenzake.Hakuna kitu muhimu katika mahusiano kama uvumilivu sababu bila uvumilivu hamuwezi fika mbali kwenye mahusiano yenu.

Unapogundua kwamba kwamba umemkosea mpenzi wako huna budi kumuomba msamaha baada ya kutambua kosa au makosa yako.Kuomba msamaha ni kitu kizuri mana umetambua kosa lako ila suala la yeye kukataa kukusamehe ilo ni tatizo lake mpenzi wako sababu wewe kwa upande wako unakua umetimiza wajibu wako.

Inapotokea umemkosea mpenzi wako muombe msamaha kisha mpe muda wa yeye kutafakari juu ya ombi lako la kusamehewa.Kama ikionekana kwamba hataki muendelee na mahusiano yenu kama awali huna budi kumuacha aende.

Kuna wakati unafika inakubidi uwe na maamuzi magumu na ukubaliane na matokeo.Jaribu kumuonyesha kwamba unaweza kuishi pasipo kutegemea uwepo wake sababu mmoja kati yenu anapogundua kwamba anapendwa sana basi hutumia fursa hiyo kumtesa mwenzake kihisia kiasi kwamba kuna wakati atakuomba hata vitu ambavyo viko nje ya uwezo wako sababu tu anaamini unampenda na lazima utatekeleza hata kwa kuiba ili tu umridhishe yeye.

Inawezekana amekuchoka na anaamini kwamba anaweza kupata mtu bora kushinda wewe, ikifikia hatua hii mruhusu tu aende tena ikiwezekana mpe na nauli.Najua ugumu wa kumuacha mtu unayempenda but try to be strong my friend,let him/her go.Ipo siku atakuja tambua umuhimu wako kwako baada ya kuwa na watu tofauti tofauti na kugundua kwamba wewe bado ni bora kuliko hao wengine aliokutana nao kitu ambacho itakua ni too late sababu atakapotaka kurudi kwako atakukuta na wewe umeshapata mtu sahihi ambae ulipaswa kuwa nae tangu awali.

Sihamasishi watu kuachana ila unapoona mambo yanazidi kuwa magumu kwenye mahusiano yenu jifunze kumuacha aende.
 
Ila serious kuacha na kuachwa hii ngoma ni moto.

Mi nawashaur. Ukiona Demu wako kaanza kubadilika,Kiasi kwamba anakuonyesha dalili za kua na mwingine , PIGA CHINI MAPEMA SANA .

TIMING ndio inaamuaga maumivu .... Ukimwacha demu ambaye alikua keshaanza kukuzengua sababu anamshikaji,..Huja Kuumia mwenyewe .

Ila ukisubiri mpaka akuambie "Kuanzia leo sikutaki"Bro kamba ileee....alafu dems wana akili kinyama, Anaweza kua anakukubali lkn akakuanza yeye kukuambia "muachane", maana anajua ukimuanza ww basi yeye ataumia sanaa.

Saizi ni kusoma ALAMA ZA NYAKATI tuu mazee.
 
Nyakati za mashaka
 
Hahahahaha vi wooooonder
 
Back
Top Bottom