Jifunze kuhusu marafiki

IzukeneJr

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2012
Posts
758
Reaction score
753
Hebu chukua dakika 2 ufikirie,

Rafiki zako ulio nao wamekuwa na mchango gani katika maisha yako? Je unafuraha kuwa na marafiki ulio nao? Je, kuna hitaji la kuendelea kuwa na urafiki na hao rafiki zako ulio nao? Ni nini unachokipata kutoka kwa rafiki zako? Je hicho unachokipata kutoka kwa rafiki zako kina mchango gani katika maisha yako? Je, rafiki zako ni faida au ni hasara katika maisha yako?

Nionyeshe marafiki zako, nitakwambia kesho yako. Rafiki ana nafasi kubwa sana katika kukuongoza katika njia ya mafanikio lakini pia anaweza kukuongoza katika njia ya kushindwa.

Ndege wafananao huruka pamoja, na warukapo pamoja safari yao itakuwa na mafanikio kwa malengo waliyonayo, ikitokea njiwa na kunguru wameruka pamoja, unaweza kuwa na uhakika kuwa safari yao itaishia njiani.

Ni vyema kufanya tathmini ya marafiki ulionao, angalia kati ya marafiki zako ni yupi ambae ukiruka nae mtafika mnapohitaji kufika, wewe ni tai unataka kuruka na kunguru, hamuwezi kufika mnapotaka kwenda, atakufanya usifike unapotaka kwenda.

Angalia watu walifanikiwa kimaisha kama Bill Gates, Mohamed Dewij na wengine wengi, angalia marafiki zao, utakuta wana vitu vinavyoendana katika maisha yao na ni kwa maneno, utani na kila kitu wanachofanya pamoja ndo vinawafanya wawe kama walivyo leo.

Kwa upande mwingine, ukiwakuta wanaume wanaonnunua malaya pale Sinza usiku, ukaangalia katika list ya marafiki zao, utakuta kwamba kwa kiasi kikubwa wanavitu wanaendana, na ni kwa maneno yao, utani na maisha yao ya kila siku ndio vinawafanya kufanya hayo wayafanyayo.

Je, ni marafiki wangapi ulikuwa nao siku za nyuma lakini siku hizi wamefuta hata namba yako kwenye simu zao. Unadhani ni nini kimetokea? Umebaki kulaumu, “Aaaah yule jamaa anaringa sana siku hizi, hata nikimpigia simu hapokei”. Unadhani ni kwa nini amekuwa hivyo? Pengine amekuona huna mchango chanya tena katika maisha yake, anaruka na anaofanana nao.

Angalia malengo yako katika maisha, Je umelenga kufanya nini maishani mwako, na je unamalengo ya kufika wapi maishani mwako. Baada ya kujua malengo yako angalia marafiki zako ulio nao, Je watakuwa nguvu ya kukusukuma kwenye malengo yako au marafiki zako ni nguvu ya kukukatisha tamaa usifikie unapotaka kufika.

Mwenyezi Mungu akuongoze kukutana na watu ambao watakuwa chachu ya kufanikiwa maishani mwako, na sio marafiki wa kukukatisha tamaa ya mafanikio maishani mwako.

Share

#SeeYouAtTheTop

Fabian Izukene
 
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106]
 
Ahsante sana, ngoja nifanye tathmini sasa
 
Ni bora kuwa peke yako kuliko kuwa na marafiki ambao watakupoteza. Kama unaamua kuwa na marafiki kuwa nao ambao unaamini watakusaidia kufikia malengo yako.
Poa mkuu, marafiki hasa wanafiki kwangu hawana nafasi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…