Jifunze Kiingereza kwa muda mfupi

Jifunze Kiingereza kwa muda mfupi

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,614
MBINU 10 ZA UHAKIKA ZA KUFAHAMU KIINGEREZA/ENGLISH KWA MUDA MFUPI
Kujifunza lugha mpya kunaweza kuwa ni kugumu, lakini inawezekana. Je unatamani kufahamu na kumudu lugha ya Kiingereza kwa muda mfupi? Kumudu Kiingereza inawezekana lakini kuna mambo kadhaa unatakiwa kuyafahamu na kuyafanya kwa uhakika.​

Ikiwa unapenda kuwa wa kimataifa, basi fuatilia mbinu 10 za uhakika zitakazo kuwezesha kufahamu Kiingereza/English kwa muda mfupi.

1. Penda na furahia Kiingereza
Ili uweze kufanya au kujifunza kitu chochote ni lazima kwanza ukipende. Ikiwa unataka kufahamu Kiingereza kwa muda mfupi ni lazima ukipende kwani ndipo utaweza kujifunza kila mara bila kuchoka wala kukata tamaa. Kila mara jihamasishe kwa kutafakari manufaa utakayoyapata baada ya kufahamu Kiingereza vizuri.

2. Jifunze Kiingereza kila siku
Huwezi kufahamu Kiingereza kama hutojifunza kila siku. Hakikisha unaongeza misamiati, unajifunza matamshi pamoja na kanuni mbalimbali za lugha.

Mambo ya kukumbuka hapa:

Nunua kamusi ya Kiswahili na Kiingereza.

Soma vitabu na machapisho mbalimbali yaliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza.

Tumia tovuti za kujifunza lugha kama vile Duolingo, Babbel, BBC Learning English n.k. kujifunza Kiingereza.

Kama inawezekana, tafuta mwalimu au chuo cha kujifunza Kiingereza.

3. Zungumza Kiingereza
Huwezi kumudu kuzungumza Kiingereza kama hutozungumza. Jitahidi katika kutumia Kiingereza katika mazungumzo yako hata kama utakosea.

Jifunze maneno uliyoyazoea kuyatumia mara kwa mara na uyafahamu kwa Kiingereza ili uyatumie katika mazungumzo.

Jambo la kuzingatia ni kuangalia tu mtu unaye ongea naye; ikiwa mtu hajui Kiingereza basi usitumie Kiingereza kwani anaweza kuona unamdharau.

Hata kama huna mtu wa kuzungumza nae, unaweza kuzungumza mwenyewe tu kwa sauti ndogo bila shida; kwani ni mambo mangapi unayokuwa unanayawaza na kuyajadili akilini mwako peke yako? Anza kuzungumza sasa.

4. Andika Kiingereza
Kuandika kwa Kiingereza kutakusaidia sana kuboresha uwezo wako wa Kiingereza cha kuandika. Ikiwa unaandika ujumbe, machapisho (posts) kwenye mitandao ya kijamii, kadi, au hata shajara (diary); basi tumia lugha ya Kiingereza.

5. Usiogope kukosea
Ni rahisi mtu kushindwa kujifunza Kiingereza kwa kigezo tu cha kuogopa kufanya makosa. Makosa ni hatua muhimu katika kujifunza kitu chochote.

Unapofanya makosa na kuyabaini, ni wazi kuwa mbeleni hutoyarudia tena. Hivyo, tumia Kiingereza katika kila eneo bila kuogopa kufanya makosa.

6. Sikiliza na tazama vitu au vipindi vya Kiingereza
Najua wengi ni wafuasi wa miziki na filamu; miziki na filamu za Kiingereza zinaweza kukusaidia kwa kiasi kikubwa kujifunza lugha. Usipende kutazama filamu zilizotafsiriwa; jitahidi kujifunza maana za maneno unayosikia kwenye filamu na miziki kwa kutumia kamusi niliyoitaja kwenye hoja namba moja.

Jitahidi pia kutazama vipindi au hotuba mbalimbali zilizoandaliwa kwa lugha ya Kiingereza kupitia televisheni au mtandao wa YouTube. Jifunze jinsi watu wanavyotamka maneno pamoja na kuchunguza maana zake.

7. Waza kwa Kiingereza
Kuwaza kwa Kiingereza? Ndiyo, kuwaza kwa Kiingereza kutaongeza uwezo wako wa lugha kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano badala ya kuwaza “Nitakwenda mjini kesho…” unaweza kuwaza “I will go to town tomorrow…” n.k. Kwa kufanya hivi kutakujengea uwezo wa kutumia na kufahamu Kiingereza zaidi.

8. Elewa na usikariri kanuni
Kila lugha ina kanuni zake. Usipoteze nguvu kubwa kukariri kanuni, bali elewa matumizi ya kanuni zinazotawala mpangilio wa maneno na matumizi yake.

Kwa mfano sentensi nyingi za Kiingereza huwa na (Mtenda-Tendo-Mtendwa au Kitendwa) yaani (Subject-Verb-Object)

Mf. Jackson killed the dog. (Mtenda = Jackson, Tendo = Kill, Dog = Mtendwa)

John is cooking the food.

Kufahamu kanuni kama hii na nyinginezo, kutakuwezesha kuelewa kwanini mtenda huanza kisha kufuatiwa na tendo pamoja na mtendwa au kitendwa katika sentensi za Kiingereza.

9. Tafuta rafiki au mshirika
Ikiwa kuna mtu ambaye mnaweza kujifunza kwa pamoja, basi mshirikishe ili mjifunze kwa pamoja. Au ikiwa kuna mtu anamudu vyema Kiingereza, unaweza kumwomba akusaidie katika mchakato wako wa kujifunza.

Kwa kufanya hivi utaweza kuuliza maswali au hata kuzungumza moja kwa moja na mshirika wako. Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa mtandao, unaweza kupata mshirika kwenye mtandao pia.

10. Kuwa na subira na usikate tamaa
Ni wazi kuwa zipo chngamoto katika kujifunza lugha mpya hasa Kiingereza. Lakini ni muhimu ukafahamu kuwa ni swala la muda, uvumilivu, mazoezi na nia tu ndivyo vitakavyokuwezesha kufahamu Kiingereza vyema. Hakuna kitu kizuri kinachotokea kwa usiku mmoja, fanya bididi usikatishwe tamaa na changamoto; nawe kwa hakika utafikia lengo.

Hitimisho

Ni ukweli usiopingika kuwa kufahamu Kiingereza siyo lazima uwe umezaliwa kwenye nchi ya watu wanaozungumza Kiingereza, bali ni kuzingatia mbinu tajwa hapo juu pekee. Naamini ukizingatia mbinu zilizojadiliwa hapo juu kwa bidii utaona matokeo mazuri katika uwezo wako wa lugha ndani ya muda mfupi.

Ahsante sana!


Je bado umekwama kwenye kujifunza Kiingereza? Je una swali au maoni? Tafadhali fika Mwasenda Youth Centre; tuko Nyasaka Centre jijini Mwanza. Tunao walimu wenye nia ya kuhakikisha unaelewa kiingereza ndani ya muda mfupi.

Mawasiliano: 0655-533543. E-mail: mwasenda2018@gmail.com / info@mwasenda.org
 
Noted with thanks Tutor, ngoja nizingatie hizo kanuni ,ntaleta mrejesho🙂
Na hizi kanuni sio kwa lugha ya English peke yake; bali ni kwa lugha yoyote ile. Ila kwa kuwa English ndo kikwazo kwa mfumo wa elimu ya bongo; ndo maana tumeelezea kuhusu hiyo.
 
Nitakuja soon hivi nyasaka centre ni hapa jirani na blessing school?
 
Na iwapo utahitaji kuhudumiwa ukiwa mbali; tuna machapisho ambayo yako simple kuyasoma na kuelewa ndani ya muda mfupi. Utapatiwa namba ya Mwalimu ambaye mtakuwa mnawasiliana kwa simu pale utakapohitaji msaada. Moja ya chapisho la kukusaidia kuelewa ndani ya wiki mbili ni hilo hapo ....
Every Day Conversation Book Cover.jpg
 
Nimejifunza kuwa kuna mambo ambayo yanarahisisha sana namna ya kujifunza lugha. Hivi karibuni nilitumia mbinu hizo kujifunza lugha fulani kwa miezi mitatu tu.

Pia kama mwalimu binafsi wa lugha, nimeona wanafunzi wangu wengi wakikwama kupiga hatua katika kujifunza English kwa namna isiyo sahihi ya jinsi ya kujifunza wanayojaribu kufanya. Ndio maana nimeamua kuandika ili kutoa muongozo kwa wanafunzi wangu wa English lakini pia kukushirikisha wewe na jamii kwa ujumla.

Ni ukweli usiopingika kuwa kabla ya kujifunza kitu chochote ikiwemo kujifunza lugha ni muhimu kujua namna ya kujifunza kitu husika, ili uweze kujifunza kwa ufanisi na kwa urahisi.

Hata hivyo elewa kuwa ninaposema kujifunza kwa urahisi, simaanishi kuwa basi kujifunza kwako hakutakuwa kugumu.

Baadhi ya mambo katika lugha yatakuwa magumu hata hivyo kwa mbinu sahihi na kwa bidii ya dhati, mchakato wako wa kujifunza utakuwa rahisi zaidi kuliko bila kuwa na mbinu na ufahamu wa namna sahihi ya kujifunza.




Vifuatavyo ni vipengele vya hizo mbinu za kujifunza lugha hususani lugha ya English.



1. Kudhamiria kuweza:

Usianze au kuendelea kujifunza kiingereza bila kujiaminisha na kudhamiria kuweza haswa kwa ufasaha. Haitoshi tuu kutamani kuweza kiingereza, unahitaji nguvu ya dhamira ya toka moyoni , na kujiaminisha kuwa wewe unaweza.




2. Kujiwekea muda maalum wa kufikia kiwango fulani :

Haitoshi tuu kudhamiria kuweza kuongea lugha ya kiingereza. Unahitaji kujiwekea malengo na mikakati ya kufikia hilo lengo na iwe kufikia lengo fulani ndani ya muda maalum.

Njia bora ya kujiwekea muda ni kuligawa lengo lako la kufahamu lugha katika vipengele vidogo vidogo halafu unaweka malengo ya kufanikisha hivyo vipingele vidogo vidogo ndani ya muda fulani.

Kwanza fahamu picha kubwa ya yote unayotakiwa kujifunza, kisha jiulize yapi kati ya hayo tayari unayajua au pengine una ‘idea’ nayo.

Hivyo weka malengo kwa kila kipengele kuendana na uwezo wako wa kuelewa.

Mfano ukishajua vipengele vyote mfano vya TENSES, jiulize ndani ya muda gani utaweza kukamilisha tenses. Hivyo hivyo kwa vipengele vingine .

Kutambua viungo mbalimbali vinavyounda sentensi:

Kila unachoandika, kuongea, kusikia au kusoma ni SENTENSI. Katika sentensi unaandika, kusoma, kusikiliza au kuongea maneno. Hata hivyo ili kurahisisha watu kujifunza lugha, maneno hayo yamegawanywa katika makundi , na hayo makundi yanafafanua matumizi na kanuni kuhusu kila neno katika kundi husika.


Mfano sentensi hii : Will you come to school ? - Je utakuja shule ?

Hapa tuna maneno matano, na yanatoka katika makundi yafuatayo:

Verbs: Will na Come

Pronoun: You

Proposition: TO

Noun: School

Kufahamu kanuni zinazoongeza makundi haya zitakafunya ujue kwanini hayo maneno yamepangiliwa hivyo yalivyo , mfano kwanini haikuwa COME WILL TO SCHOOL YOU ?

Katika kujifunza kanuni hizi ndipo utakapojitofautisha wewe na wale ambao wanadhani kujifunza lugha ni kujua maneno mengi.

Kuna watu wengi wanajua maneno mengi ya kiingereza na ni wepesi wa kuchanganya kiswahili na kiingereza wakati wa mazungumzo ila inapofika kuongeza kiingereza tuu kwa mfululizo inakuwa ni tabu kwakuwa hawana ujuzi wa kuunda vema sentensi.

3.Kusoma kwa mpangilio:
Baada ya kufahamu kuwa lugha ina vipengele kadhaa vinavyounda sentensi na kanuni zinazoongoza kila aina ya maneno , bila kusahau nyakati –tenses, jiwekee utaratibu wa kusoma hatua kwa hatua kwani vipengele vingi vinaendana.

Mfano kama haujaelewa vizuri tenses, itakupa shida kuelewa active and passive voice, na reported speeches.

4. Kusoma kwa mfululizo bila kukatisha:

Mbinu nyingine ni kuhakikisha kuwa unajifunza lugha kwa muda maalum na kwa mfululizo. Sio unajifunza kwa "manati" mara moja au mbili tuu ndani ya mwezi.
Ili kufanikiwa kujifunza kwa urahisi na kwa haraka hakikisha unatenga muda walau mara tatu kwa wiki, na kwa muda wa walau masaa mawili kila siku na hakikisha unasoma hivi kwa muda mrefu mfano walau kwa miezi mitatu mfululizo kwa kasi hiyo hiyo ya kujifunza.

Kwanini unahitaji kujifunza kwa mfulululizo ? Ni kwa sababu kujifunza lugha kunahitaji sana kukumbuka na kuhusanisha uelewa wa vipengele tofauti vya lugha.

Hivyo kujifunza mfululizo kunatuma ujumbe kwa ubongo wako kuwa hayo unayojaribu kuhifadhi katika kumbukumbu yako ni ya muhimu, hivyo nao unatenga nafasi ya kukusaidia kuyapata haraka unapohitaji –yaani kumbukumbu ya haraka.

Kumbuka pia hata kama unasoma na yanakuwa magumu, ukiendelea kurudia mara kwa mara jambo lile lile baada ya muda unajikuta umeshajenga aina fulani ya kumbukumbu na uwezo wa kuhusanisha yale uliyojifunza zamani na taarifa mpya ya jambo hilo hilo husika.

5. Kufahamu matumizi ya nyakati na kanuni zake :
Mbinu hii inahusu vitu viwili muhimu sana, kwanza kujua uwepo wa nyakati na matumizi yake yaani je katika hali ipi unatumia present tense, au past tense, au future tense, halafu kitu kingine cha pili cha muhimu sana ni kujua kanuni zinazoongoka namna ya utungaji wa sentensi katika kila aina ya nyakati.

Hitimisho:

Kwa ujumla wake nilitaka kukuonesha kuwa kujifunza English ni zaidi ya kusikiliza, na kusoma, unahitajika wewe mwenyewe kuingia hasa katika mchakato wa kuelimika kwa kufanya bidii kujikumbusha na kurahisha namnaya kuelewa unachosoma.

Kwa msaada wa maelekezo binafsi ya kufahamu vema lugha ya kiingereza; karibu kituoni kwetu – Mwasenda Development Intervention – Nyasaka Centre (Nyamuge) jijini Mwanza. Wasiliana nasi kwa 0655-533543 au kwa mwasenda2018@gmail.com / info@mwasenda.org
 
Karibu tukuhudumie ... au unaweza kujisomea nyumbani kwako pale utakapokuwa umechukua vitabu vya mwongozo.
 
Back
Top Bottom