JIFUNZE INFORMATION TECHNOLOGY-(IT-TEHAMA)

JIFUNZE INFORMATION TECHNOLOGY-(IT-TEHAMA)

jikuTech

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2023
Posts
228
Reaction score
290
Jiku Tech Tips inajivunia kuwa mshirika wako katika safari yako ya kujifunza na kukuza ujuzi wa teknolojia. Kama Full Stack Developer mwenye uzoefu na Mkufunzi mtaalamu, Jiku Tech Tips imejitolea kukupa mafunzo bora na yenye tija katika ngazi zote:

  • Ngazi ya Awali: Tunaweka msingi imara kwa wanaoanza, tukihakikisha unaelewa dhana za msingi za programu na teknolojia.
  • Ngazi ya Kati: Tunakusaidia kukuza ujuzi wako zaidi, kukufundisha mbinu za hali ya juu na kukupa uwezo wa kutatua changamoto za kikazi.
  • Ngazi ya Juu: Tunakuandaa kuwa mtaalamu wa teknolojia, kukufundisha kuhusu mifumo changamano na kukupa ujuzi wa kuongoza miradi ya teknolojia.
Kwanini uchague Jiku Tech Tips?

  • Uzoefu wa Kina: Tunajua mahitaji ya soko la teknolojia na tunakupa mafunzo yanayokufaa.
  • Mbinu Shirikishi: Tunatumia mbinu za kufundisha zinazokushirikisha kikamilifu, kuhakikisha unaelewa na unakuwa na uwezo wa kutumia ujuzi ulioupata.
  • Mtaala Uliopangwa: Tuna mtaala uliopangwa vizuri ambao unakusaidia kujifunza kwa utaratibu na kufikia malengo yako.
  • Msaada Endelevu: Tunakupa msaada wa kutosha hata baada ya mafunzo, kuhakikisha unaendelea kukua na kufanikiwa katika taaluma yako.
Jiku Tech Tips inakupa uhakika wa kupata mafunzo bora yatakayokufanya uwe mtaalamu wa teknolojia unayetamani. Jiunge nasi leo ili tuanze safari yako ya mafanikio!


Tembelea kiungo hiki hapa chini kuingia kwenye mafundisho ya IT -TEHAMA yanayo endelea mtandaoni kupitia WhatsApp,Youtube na Live Session

<<<< Jifunze Information Technology (IT-TEHAMA) >>>>



VIDOKEZO

UTANGULIZI

JIKU TECH TIPS ni Software Developer na mkufunzi wa hatua za awali na kati za kujifunza , kufanya na kuishi Tehama ya awali, kati na juu.

TEHAMA kirefu cha maneno Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, huwakilisha teknolojia ya kompyuta na mitandao ya mawasiliano...........................................





Teknolojia ni sayansi​

Sayansi inafanya kazi ya kutafuta, kushughulikia taarifa na kuhifadhi mantiki zote zinazo tokana na taarifa hizo kwa ajili ya matumizi ya baadaye na siku hizo hasa kwenye maamuzi flani.

Taarifa ni Habari maalumu, pia taarifa inaweza kuwa takwimu zenye maana inayoweza kutumika kufanya maamuzi flani............................

..................................................................................................................

Ujuzi Wa Kitaalam/ Ujuzi Wa Hali Ya Juu kwenye tehama​

Huu ni ujuzi/taaluma maalamu ambao ni kwa ajili ya jambo maalam na ujuzi wenyewe unahusisha maarifa ya juu ya software program, Lugha mbalimbali za Kompyuta na mifumo mbalimbali ya Kompyuta yaan complex Kompyuta systems

Hapa ni mifano ya ujuzi wa juu wa Kompyuta





...............................................................................................................................

PROGRAMMING NI NINI?

Programming ni mchakato wa kuunda program za kompyuta kwa kutumia lugha za kompyuta. Programu hizo ni maagizo ambayo kompyuta inafuata ili kutekeleza kazi flani.

............................................................................................................................



Programming ni mkusanyiko wa maelekezo ambayo kompyuta inaweza kuelewa na kutekeleza

Mfano: Programu ya Calculator ( kikokotoo) programu hii inaeleza jinsi ya kujumlisha, kutoa,kuzidisha na kugawanya namba na mengine....... mfano mwingine ni mfumo wa undeshaji , programu hii inaeleza kompyuta jinsi ya kuwasiliana na vifaa kama kibodi, kipanya,monitor na kuendesha programu zingine.



LUGHA ZA PROGRAMU

Programu hizi zimeandikwa kwa kutumia lugha za programu. Hapa kuna baadhi ya lugha za programu.



Lugha za programu ni kama lugha za kibinadamu lakini zimeundwa kwa ajili ya mawasiliano na kompyuta. Ni seti ya sheria na syntax ambazo tunatumia kuandika maelezo ambayo kompyuta inaweza kuelewa na kutekeleza.



............................................................................................



User Interface​

User Interface ni sehemu ya programu ambayo mtumiaji ambaye hawezi na haelewi kuhusu programming na mchakato mzima jinsi program inavyofanya kazi anapata uwezo wa kutumia program bila shida kutokana na maelekezo yanayo kuwepo kwenye screen akiwa amewasha program mfano. Sign in, See More, Like, share, Read More, Play, Downloand, inakuwa ni vitu ambavyo mtumiaji anaelewa kabisa kwamba nikibonyeza hapa naenda kufanya hivi. Hiyo ni sehemu ya User Interface sehemu ya program kwa upande wamtumiaji.

Kuhusiana na User interface kama haujaelewa vizuri unaweza tafuta mtu anaye elewa kipengele hiki akakuelewesha zaidi ya hapa.

..................................................................................................................

Backend Processing​

Ni sehemu ya program ambayo michakato ya kuwezesha kazi kusudiwa ya software inachakatwa , mfano sasa mtumiaji amebonyeza Download Now basi kwenye Backend kuna kuwa na mazingira yanayo wezesha mchakato anao utaka mtumiaji kwa wakati huo , wa kudownload kile alicho kiona na kukipata kama alivyokusudia. Mfano user anataka ku log in kwenye backend ndio sehemu pekee ambapo taarifa zina linganishwa kama ni sahihi na kutoa ruhusa au kukataa ombi la mtumiaji. Mbinu ya kujifunza zaidi kitu ni kutafuta taarifa zake nyingi, kwa hiyo hapa nilikuwa najaribu kutoa mwanga ila unaweza kufuatilia zaidi kwenye masomo ya Backend Programming.

..............................................................................................................................



Data / Taarifa​

Programming inafanya kazi na taarifa, software ina tegemea taarifa ili iziendeshe kwa namna mbalimbali kama alivyo panga mtengenezaji kwa software yake itaenda kutatua changamoto gani . Katika Programming kuna Utaratibu wa kuhifadhi taarifa.

Taarifa huhifadhiwa kwenye Database, Kuchakatwa kwenye Server na kisha Mtumiajia.

Mtumiaji anapo jisajili kwenye mfumo flani anakuwa anawasiliana na server ifanye kazi anayo ikusudia mfano kujisajili anakuwa anaiambia server imsajili, ambapo server itachukua taarifa za mtumiaji huyo na kisha kuzihifadhi kwenye database kwa ajili ya baadaye zikihitajika ziwepo.



Mtumiaji anapo Log in anawasiliana na server, server inafanya uchunguzi kama hizi taarifa zipo kwenye database au amna kama amna ina kata ombi kama zipo inatoa ujumbe wa OK na taarifa zinazohitaji kwa mtumiaji huyo.

Taarifa zinaweza kuwa za aina nyingi mfano, Video, Maneno, Picha na Audio. Server inafanya kazi kwa kushirikiana na database ili kutoa huduma kwa mtumiaji, yaani inapokea maombi na kujibu kama ilivyo elekezwa na aliye itengeneza. Ambaye kwa wakati huo utakuwa wewe.



....................................................................................................

Mfano ikiwa haujui kusoma lazima umfuate anaejua kusoma akufundishe kwa ajili ya wewe kujua kusoma. Mara nyingi ni Kwenda shule, mara chache kutafuta Mwalimu mtaani.

Mtu utakuwa na amani kujifunza jambo ambalo linatoa kiu yako, na hapo ndio NIA ya kujifunza au angalau kuanza kufuatilia itakuja...................................

.................................................................................................................




Mtandao wa intaneti ni muunganiko wa kimataifa unaounganisha kompyuta kote ulimwenguni. Kwenye huu muunganiko wa kimataifa wa kompyuta ndio kuna seva,taarifa, na client kama tulivyo eleza hapo awali.

Seva: ni sehemu au ni kompyuta kubwa maalum kwenye mtandao wa intaneti kwa ajili ya kuhifadhi taarifa.

Taarifa: ni Habari au kumbukumbu zinazo hifadhiwa kwenye seva au maelezo .



Client(mteja): ni kompyuta inayo tumiwa na mtu anaye tafuta taarifa kwenye mtandao wa intaneti......................................

..............................................................................................
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom