Jifunze ewe mwanamke

Jifunze ewe mwanamke

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
1. Usikimbilie kuhama na kuondoka nyumbani kwa wazazi wako kabla hujajipanga vizuri.

2. Usimsubiri mwanaume ndio uanze maisha, unaweza ukaishi maisha yako mwenyewe na ukaweka msingi mzuri utakaokusaidia huko baadae.

3. Kaa mbali na marafiki waovu, jifunze kuheshimu kila mtu kuwa na busara na vaa mavazi ya heshima.

4. Usimchekee chekee kila mwanaume, kwa maana wengine sio waoaji ni chui waliojivika ngozi ya kondoo! Ni bora ukaendelea kuabki single kuliko uje kuolewa na mtu ambaye atakufanya ujute maisha yako yote hapa duniani. Omba Mungu akupe busara na ustahimilivu.

5. Jijengee tabia ya kula kwa afya, siku zote jitahidi ule milo yote mitatu acha kula biscuit na soda, usipendelee chips na mishkaki na vyakula vya aina hiyo. Fanya mazoezi mepesi kuuweka mwili wako uendelee kuwa mzuri wa kuvutia. Wewe ni tunu kwa mume wako mtarajiwa au uliyenae.

6. Vaa kwa heshima, watu watakujaji kulingana na jinsi tu ulovyovaa hata maongezi yao yataegemea kutokana na uvaaji wako.

7. Usitumie SEX kama njia ya kujihakikishia Mapenzi. Kufanya mapenzi sio tiketi ya kupendwa. Ata SEX na wewe na atakuacha kwenye mataa ya ubungo junction.

8. Usiolewe nae kwa vile ana pesa za kutosha na ni tajiri kwa sababu karibuni tu na wewe utakua moja ya mali anazomiliki.

8. Jiongezee thamani, get a career! Usiwe mpumbavu kufikiri mwanaume ndio atasuluhisha matatizo yako yote. Jibidiishe kwa kazi zako binafsi hakuna raha juu ya kuwa na maamuzi ya kutumia kile kipato ulichokipata kwa jasho lako.

10. Wewe ni wa muhimu mno, una thamani kubwa sana! Jipende jiheshimu, jijali. Usijali umetendwa na wangapi katika mahusiano! Usikate tamaa jiweke vizuri. Ishi maisha yako. Hayo unayopitia ni funzo tu ktk maisha.

Above all, Remember this, Charm is deceitful, and beauty is vain: but a woman that fears the LORD, she shall be respected.


MUNGU AWABARIKI WANAWAKE WOTE ULIMWENGUNI.

Mwalimu Tweve Hezron
 
Mwenye masikio na asikie mimi nimesikia nakunifunza asantee mwaya
 
Umeongea yote mleta mada,ila kwa upande wangu mimi mwanaume wa kiafrica najiuliza tu ikiwa binti anaishi mji mmoja na wazazi wake na amebarikiwa kupata kazi au kufungua biashara,ni kitu gani kitakufanya uhame kwenu ukaanze maisha yako kabla hujampata mwenzako wa kukutoa hapo kwenu kwa heshima zote?
 
Umeongea yote mleta mada,ila kwa upande wangu mimi mwanaume wa kiafrica najiuliza tu ikiwa binti anaishi mji mmoja na wazazi wake na amebarikiwa kupata kazi au kufungua biashara,ni kitu gani kitakufanya uhame kwenu ukaanze maisha yako kabla hujampata mwenzako wa kukutoa hapo kwenu kwa heshima zote?
Naungana na wewe kwenye huo UANAUME WA KIAFRIKA kwenye kuhoji......labda waseme wazazi wanaishi kwenye nyumba ya kupanga, lakini pia akae nyumbani mpaka atakapopata sababu inayoeleweka ya yeye kwenda kuishi peke yake. Kama atakuwa amejenga, ruksaaaa! Lakini sio akapange ilhali nyumbani kupo!
 
Kuna wadada humu ni wabishi na wagumu kuelewa.

Hapo wanasoma wanasonya kimya kimya.
 
Ukitaka wanaume wasikutongoze hovyo kuwa muongeaji ukiwa nao jiachie ongea watakuona mshikaji wao na rafiki tu watakutamani lkn kukutamkia ni ngumu. Lakini ukiwa mpole unawavutia kukutongoza na kila huyo atajaribu bahati yake kwako.
 
Dah.... kiuhalisia hizo sharia zitaanza kupunguzwa moja moja kadiri muda unavyosogea....kutoka "mbwa mkali" hadi "tunauza ice cream"[emoji41] [emoji87] [emoji13]
 
Ktk kumi waliosoma ni mmoja tu ndo aweza zingatia hayo!
 
Umenena vyema madame bt No. 1.nawatupia lawama wazazi wa hao mabinti why mzazi anamruhusu binti yake aondoke nyumbani bila kuwa na uhakika anachokwenda kufanya huko aendako?kuna mabinti jirani hapa wanaishi na wanaume kindoa(kama mke na mume)ilihali wanaume hao hawajulikani na familia za mabinti hao, swali la kujiuliza mabinti hawa waliondoka vipi kwao?kwanini wazazi wa mabinti hawa hawafuatilii kujua mabinti zao wako wapi na wanaishi vipi? Mungu atusaidie baadhi ya wanawake bado tuna safari ndefu sana ya kujitambua!!
 
Mkuu nimependa ushauri wako.

Ila hiyo namba 5 hiyo kwakweli naomba uwasamehe, hilo litawashinda wengi kama sio wote. Wanawake kwa kula kula hawajambo, tena kula vitu visivyoeleweka, mara bisi, ubuyu n.k

Mkuu naona hiyo list isiwe na vipengele kumi toa hiyo namba tano

Tisa vitapendeza zaidi
 
Ukitaka wanaume wasikutongoze hovyo kuwa muongeaji ukiwa nao jiachie ongea watakuona mshikaji wao na rafiki tu watakutamani lkn kukutamkia ni ngumu. Lakini ukiwa mpole unawavutia kukutongoza na kila huyo atajaribu bahati yake kwako.
Kwahyo ndyo kusema kuwa unawafundisha wanawake wakatae kutongozwa wakat wote.....hahahahaa...
 
Kwahyo ndyo kusema kuwa unawafundisha wanawake wakatae kutongozwa wakat wote.....hahahahaa...
Hayo ni madini nawapa mabinti wadogo waweze kumudu mikiki mikiki ya wanaume wasio lazima kuwa waume zao vinginevyo mimba zisizotarajiwa na kujiliza liza huku wajiitwa kwa kejeli Single Mothers
 
Back
Top Bottom