Kasimba G
JF-Expert Member
- Jan 19, 2011
- 3,428
- 2,611
Katika tawala za JK Nyerere, AH Mwinyi zilikuwa na fashion moja, wanasiasa ndio walikuwa juu ya kilakitu!
Wanasiasa walikuwa wanaakili, wajuaji, ndio waelewa wa kila kitu na wenye akili kupita watu wote nk. wanasiasa ndio walikuwa watoa maamuzi yote na wanakuwa wasomi wa kila taaluma maana hata mambo yanayohusu taaluma wanasiasa hao walikuwa wanatoa solutions za kitaalam.
Wakati wa utawala wa Ben Mkapa waliendelea na mtindo huo huo wa ujuaji japo ilikuwa kwa kipindi kifupi saana. Miezi michache saana ya utawala wa Ben kukatokea janga ambalo likahitaji taaluma katika utatuzi wake, Meli ya Mv Bukoba ikapata tatizo, lakini kama jinsi mazoea ya mifumo ya hapa nchini yalivyokuwa kwamba wanasiasa kuwa ndio walikuwa wako juu ya kilakitu na wajuaji wa kilakitu. Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza akawa mtaalam! akaamuru aliyoyajua yeye na matokeo yake watu mamia wakafariki dunia.
Bwana Ben akajifunza kitu kutokana na mkasa huo wa mv bukoba, na taaluma za watu zikaanza kuheshimika, na kwakweli kama taifa mambo mengi yakaanza kubadirika, as a result mambo serikalini yakaanza kubadirika na serikali ikaanza kuwa na maono na pesa pia. Wataalamu waliotukuka waTanzania wengi wakarudi hapa TZ watu kama akina Daudi Balali, mchumi nguli akaja kuongoza benki kuu, Arthur Mwakapugi mchumi nguli akarudishwa nae kuongoza Macro economy. Na wengine wengi tuu. Kuna taasisi nyingi zikaanzishwa, sera na mipango mingi zilabuniwa, mfano Mkukuta, mkurabita nk.
Serikali ya bwana Kikwete ilikata katikati yaani ikaanza na mambo ya akina mwalimu plus ya Ben. Lakini asilimia kubwa zaidi ilichukua ya Ben huku ikidumu zaidi kuheshimu kwa kiasi kikubwa taaluma za wabobezi, ilifanikiwa pia "kutongoza" watanzania wabobezi waliokuwa nje kurudi kutumika hapa nchini kwetu, kama alivyokuwa akifanya bwana Ben.
Kwa maoni yangu Serikali hii mpya ya bwana JPM inarudi kuleee mwanzoni kwa akina JK Nyerere na AH Mwinyi. yaani wanasiasa wameanza kuwa juu ya kilakitu, wanakuwa wanajua kila kitu na kama Mv Bukoba ingetokea tena Nadhani wanasiasa watakuwa waamuzi wa kila kitu, maana wanajua kilakitu, ni wataalam wa kilakitu nk.
Mifano hai ya upembuzi wangu huu ni suala la sukari. Naona kama kuna makosa mengi ya kiutaalamu kuhusu suala hili. Bodi.ya sukari wanajua kilakitu kinachoendelea na walikuwa na takwimu juu ya kilakitu! lakini nahisi wanasiasa wako juu zaidi ya bodi ya sukari, maamuzi kama kupiga marufuku vibari vya importation ya sukari, sidhani kama kulikuwa na utafiti wowote kabla ya kutoa maagizo hayo, kungekuwa na utafiti kusingetokea matatizo katika suala hili.
Kauli ya jana ya president kuwa anamfahamu mfanyabiashara amenunua tani sijui kasema elfu Nne? oups! kuwa kaficha? kwa ufahamu wangu mdogo juu ya suala la sukari, kuna watumiaji wakubwa na watuimiaji wadogo. Watumiaji wakubwa ni kama akina Zakariah, SS Bakhresa, Mo nk. hawa wana viwanda vikubwa ambavyo sukari ni mojawapo kati ya malighafi zake, ninaufahamu kuwa prodiction ya hapa nchini haiwatosherezi hawa MA tycoon! wanatumia sukari kwenye products zao kama juice, soda, yogut nk. sasa ukienda ghala za matycoon utakuta storage ya kutosha ya sukari. Huwezi kuwatuhumu mojakwamoja matycoon kwa storage yao.
Watumiaji wakubwa hao wa sukari pia walipewa privilege ya kuwa na vibari vya uagizaji wa sukari nje ya nchi nadhani ni kwa nia nzuri tuu.
Ushauri wangu, Raisi apunguze siasa na kuzingatia na kuheahimu taaluma za watu ili kilakitu kiwe kiweledi, si kisiasa, arudi kwenye misingi ya bwana Beni kuheshimu taaluma na aelewe wanasiasa hawajui kilakitu.
Pia aruhusu na kuomba kukosolewa ili hata wasaidizi wake wasibaki kumshangilia hata sehemu wanajua anakosea. Akiomba kukosolewa wasaidizi wake watakuwa wa kwanza kumkosoa matokeo yake utendaji wake utakuwa uliotukuka. Nina ushahidi maana nimemsikia mtumishi wa umma akikiri kumuogopa Magu mnoooo! sasa ukiogopwa mno itakuwa ngimu watu kukushauri.