Jibu sehemu ya kwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jibu sehemu ya kwanza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Nov 7, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Nov 7, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Katika siku za karibuni kumetokea watu walioamua kujipanga na kuamua kusambaza taarifa za uwongo na uzushi kuhusu mimi na mmoja wa rafiki zangu ambaye – nimesoma nae , nimekua nae na mpaka sasa hivi bado tunafanya kazi pamoja kwa ushirikiano mkubwa .

  Watu hawa wengi wako katika listi ya mtandao wa wezi wa laptop na simu za mkono , nilipoandika list ile nilikuwa na uhakika nayo na nilifanya uchunguzi wa kina sikuwa na kisasi chochote wala ubaya wowote na mtu wowote yule ila jamii ilipaswa iwajue nami nilipata nafasi hiyo ya kuipa jamii kile ambayo inatakiwa ujue na kuweza kupambana nayo siku za mbeleni .

  Sitangazi vita wala uadui wowote dhidi yao bali nawaambia kwamba vitendo walivyovifanya na wanavyovifanya mpaka sasa hivi vinajulikana na vinarekodiwa wangoje kupandishwa katika vyombo vya sheria na kuhumiwa kutokana na yale matendo waliyoyafanya , majina yao tunayo , namba zao za simu tunazo , wanakoishi tunakujua ndugu na jamaa zao tunawajua kwahiyo wangoje pale masuala mengine yatakapo kamilika .

  Nitaeeleza baadhi ya mambo ambayo yaliandikwa katika ujumbe huo na majibu yake .

  Afande , cid james * - huyu ni askari mpelelezi kituo chake kilikuwa ni mabatini , watu wengi sana wanaoibiwa au kupotelewa na laptop sehemu za kijitonyama , sinza wakienda kushitaki eneo lile huyu askari ndio huhusika sana katika kutafuta na kupeleleza , badala ya kufanya kazi yake hiyo ya kufikisha watuhumiwa katika vyombo vya sheria inapohitajika yeye huwatoa kwa pesa ambayo ni nusu ya mali ile iliyokamatwa au kupatikana mfano kama laptop gharama yake ni dola 800 yeye anapewa dola 400 basi atamruhusu mtuhumiwa aondoke zake na kuacha hiyo mali kwake .

  Kwa mtindo huu amefanikiwa kuwa na laptop nyingi sana za watu haswa mafundi ambayo hupelekewa kutengeneza na huyu huyu bila kujua kwamba ni mitego , ushahidi upo eneo la kati kati ya jiji mafundi karibu wote wa komputa wanamjua na kutambua shuguli zake hizi .

  Mara ya mwisho alikuwa na laptop moja aina ya dell vosto ilikuwa mpya pamoja na fujitsu seamens , hiyo fujitsu ni mali ya mtu mmoja wa dodoma anayeitwa g shirima haijulikani afande james aliipataje mali hii wakati si yake ina ina nyaraka za watu ndani yake , ilikuwa haina adapotor akaenda kununua adapotar katika duka la mitsumi jijini dar es salaam ambayo ni universal .

  Mali hiyo zote huwa haziandikishi katika mapokezi ya polisi badala yake huwa anakaa nazo yeye mwenyewe katika gari lake marino la rangi ya kijani au katika nyumba ya wageni ambayo iko karibu na kituo hicho cha polisi cha mabatini .

  Pamoja na vitendo hivyo vyote amekuwa na ushirikiano na baadhi ya watu wanaojiunga katika forums kadhaa za internet wanaojifanya wamepotelewa na laptop ukiwapa msaada kwamba jaribu hili au lile basi atakuomba kontacts anampa huyu askari anaaza kukutafuta wewe kama mtuhumiwa wananjia mbali mbali majina yao yapo na uchunguzi unaendelea kuweza kuwafikisha katika vyombo vya usalama siku za mbeleni .

  Kuna wakati mmoja wa watuhumiwa wa mtandao udhalilishaji wa theutamu alikamatwa akatakiwa atoe maelezo zaidi na kuja kuhojiwa askari huyu alihusika katika kumdhamini pamoja na watu wake , mtuhumiwa huyo alitoroka bila kuhojiwa na kutoa maelezo ya ziada kuhusu matendo yake baada ya lisaaa limoja tu ilikuwa ni siku ya weekend – atueleze na kesi hiyo ilifutwa mpaka leo hii

  hili ni jibu la kwanza kwa wale ambao walikuwa wanahitaji maelezo ya ziada kama polisi huyo anabisha hafanyi hivi au hajawahi kujihusisha na vitendo kwa namna yoyote ile apeleke suala hili katika vyombo vya sheria mashahidi na watu ambao amewahi kuwadhalilisha kwa njia hizo hapo juu wapo na wako tayari kuja katika vyombo hivyo kutoa ushahidi wa kina wakati wowote watakapohitajika .

  Kawaida yake ni kutishia watu kwamba atawapoteza ndio maana wengi wanaacha mali zao kwake na wengine kulazimika kushirikiana nae kwanjia ambazo sio halali ili kuweza kulinda masilahi yao mengine popote pale

  ni shauri ya wahusika kuhakikisha askari huyu anafikishwa katika vyombo vya sheria mara moja na kuhukumiwa kutokana na sheria zinazomhusu .

  Habari ndio hiyo
   
Loading...