Gurudumu
JF-Expert Member
- Feb 5, 2008
- 2,349
- 261
Wandugu,
sifahamu hasa wamiliki wa JF na kwamba waliazisha wakikusudia nini.
Kwangu mimi ni dhairi kwamba JF imechangia sana katika kukuza demokrasia katika siasa na sera za Tz. Pia katika mapambano dhidi ya ufisadi.
Siku chache kabla ya Uchaguzi mkuu wa Octoba 2010, MM aliazisha thread ambayo alidai angejiuzulu kuandikia humu JF kwa kuwa alihisi impact ya nguvu zake haikuwanufaisha wananchi wa vijijini. Patten ya idadi ya kura na ushindi katika Uchaguzi uliopita pengine ilithibitisha hilo
Kwa kuwa naamini kwamba bado tunahitaji JF kuelekea 2015, ingekuwa vema JF ikafanya impact assessment kuona achievment na changamoto ili kuboresha zaidi
Wandugu,
nashukuru sana kwa michango yenu kwenye Part one ya thread hiyo hapo juu na link yake hii. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/92335-jfs-impact-on-tanzanian-politicts-4.html
1. Kwa ufupi mchango wa kwanza uliibuka kulalamikia Mods lakini kadri mjadala ulivyoendelea ilikuwa wazi kwamba Mods wanafanya kazi nzuri sana na kwamba hata kama kuna kasoro chache zinatokana na ubinadamu pamoja na ufinyu wa rasilimali walizonazo.
2. Wazo la pili lilikuwa kwamba JF ni muhimu sana kwa kuchochea mjadala na kushirikishana taarifa muhimu. Hapa changamoto imetajwa kuwa ni wale mavuvuzela wasio na ufahamu wa kujadili hoja kwa kutumia sayansi ya mantiki. Kwamba wanapotezea wenzao muda na kukera
3. Wachangiaji pia walikiri kwamba JF ilikuwa burudani zaidi kabla ya kampeni za uchaguzi wa 2010 kwani kipindi cha uchaguzi waliingia watu waliokuwa na kazi ya kutetea na kusifu vyama vyao na itikadi zake.
4. Kwa ujumla wachangiaji wengi wamekiri kwamba access ya JF ni kwa wateule wachache. Hasa wenye fursa ya internet ofisini kwao, wanaoishi mijini, na hasa wanaume.
5. Mtazamo ulikuwa ni kuelekea 2015, hivyo mapendekezo machache yalitolewa.
6. Kwamba ili kufikia watu wa vijijini, wachangiaji wengi wa JF waandike makala za uchambuzi wachape kwenye magazeti yasambazwe. Pia radio ilionekana ni mojawapo ya njia kuu ya kuweza kuwafikia watu wa vijijini na hasa wale wasio na access na internet. Tv nayo ilitajwa.
7. Lengo ni kusambaza hizi fikra zinazopatika hapa kwenye kisima JF kuamsha uelewa na ari ya wananchi wengi katika kuleta mabadiliko ya kisiasa na kisera.
8. Kuna magazeti ambayo kuchukua mijadala iliyojiri humu JF na kuandika. Nimefurahi kwamba Star TV nao wameanza kutumia JF kama njia ya kuzalisha fikra ambazo wanazitumia kuendesha mijadala ya kitaifa ambayo watazamaji na wasikilizaji ni wengi zaidi kuliko wanaotembelea hapa JF.
9. Je, kuna jitihada za kuanzisha JF radio ambazo zitakuwa zinatumia mijadala hii hapa kuendesha live discussion na wananchi hasa katika yale maeneo ya nchi hii ambayo mwamko wa elimu ya uraia umedhihirika kwamba ni mdogo? Awamu hii tuna kazi kubwa na ngumu ya kudai katiba mpya, tume ya uchaguzi huru, na sheria ya uhuru wa habari. haya ni majukumu makubwa ambayo yanahitaji mjadala mijadala mipana katika ngazi zote za jamii yetu. Ni vizuri kufanyia kazi hili