JF members tupime ukimwi

Yo Yo

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,217
1,702
Ni vizuri members tupime ukimwi....Ni jambo la busara ili kujua mipango yako ya baadae......fuata moyo wako sio ulazimishwe......

Hivi ukipima na ukakutwa 'unao' unajisikiaje? Nini raha yake haswa?

Nilipima... Majibu yalipokaribia kuletwa nikahisi ganzi kila sehemu. Nilikuwa naangalia Tv nakumbuka... Lakini sikumbuki hata kama niliona kipindi gani nilikuwa naangalia! Mbaya zaidi nilipoitwa niingie kwa Dr... Nilikuwa nahisi nisiende kabisa... Nini kilikuwa kinanisababishia woga? Nazini sana? NO! Si kama hivyo... Wasiwasi wa endapo nitaambiwa nimeathirika, nani atakuwa kaniambukiza? Nilikosa mwelekeo.

Dr akaniuliza kama nina partner nimeenda nae ili tuweze kupewa ushauri pamoja. Nilijibu kwa kifupi SINA. She was shocked and said "Mbona unaonekana mnyonge sana?". Swali hilo lilikuwa linanifanya nihisi kama kuna kingine anacho cha kuniongezea simanzi. Ili kuua 'soo' nikamwambia "Hapana dadangu ni kuwa sina muda mrefu sasa ndo maana nataka niijue afya yangu kabla sijaenda hatua nyingine".

Guess what? Akasema "Nasikitika..." simu yake ikaita akapokea bila kumalizia. Almost I was dead! Nilikuwa nahisi kama jasho linatiririka. Alipomaliza akasema kakangu uko OK kabisa na nakushauri ujiepushe na ngono kabisa na ukishindwa tafuta mwenza na uje nae mpime kisha mfunge ndoa.

Kidogo nimkumbatie as if yeye ndo alikuwa anaulinda mwili wangu.

UZURI WA KUPIMA: Ukijua hujaathirika basi inakuwa ni silaha tosha kukwepa anasa zinazoweza kukupelekea kuupoteza uhai kirahisi kwa starehe za dakika 30-50!

Nawashauri mkapime "Kama moyo mnao!". Na ni vema kupima mara 3 ili kuthibitisha usahihi wa vipimo.

UKIMWI upo na unaua vibaya sana! Usiombee umwone aloambukizwa... Hutotamani kufanya upuuzi kufanya ngono zembe
 
loh......
Nakumbuka mara ya kwanza kupima ilikuwa mwaka 2006......
Walllahhhhhhhhhh sirudii tena kupima.....
Jasho lilinitoka....
Nilipokuwa nafata majibu sikuwa najielewa elewa..........


Unadhani nitarudi kupima?
Labda mnibebe na winchi....
 
Owesome ideas...but kipi kimekusukuma kuja na mawazo haya!!...You sounds like umeumwa na nyoka so ukifunguka zaidi it will be icing on the cake.
 
Ni vizuri members tupime ukimwi....Ni jambo la busara ili kujua mipango yako ya baadae......fuata moyo wako sio ulazimishwe......
It begins with YOU.


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kapime ili uwape wezako dili. Mi SIPIMI. Sema hawa wahuni wana mbinu nyingi za kukufanya upime, wanalazimisha kila mama mjamzito lazima kupima, sasa mkeo mjamzito akipima si mmeshapima wote?, aah! ngoja nichukuwe glasi ya maji ninywe. www.maajabuyamaji.net
 
daima siamini kama kunakuishi kwa matumaini hasa kwa masikini na hapo ndipo ninapopata mashaka kuhusu suala zima la kupima vinginevo its a good idea
 
Nimecheka sana! Umenikumbusha jamaa angu mmoja naye alisema kama wewe: kwamba wasubiri mpaka atakapokuwa hajiwezi wambebe kwa machela ndo wakampime. Loh!

Hata mi namkumbuka maana alisema yeye ni striker Kama Drogba!!
 
Back
Top Bottom