JF HILI TATIZO LA UMEME Tuna Vongozi wa Kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JF HILI TATIZO LA UMEME Tuna Vongozi wa Kweli?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mo-TOWN, Dec 6, 2010.

 1. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Inawezeka kuna thread tayari tumegusia swala hili. Nimeanzisha hii thread kwa kuwa nakerwa sana na hii hali kupita maelezo.

  Ni aibu watu wamekuwa wabinafsi wenye kufikiria matumbo na familia zao tu wakati wamepewa madaraka ya kitaifa.

  Hainingii akilini kabisa serikali inayoongozwa na madokta (labda ni kweli madoka feki) kibao wanaweza kuwa wapuuzi kiasi hiki. Kwanza nisema ukweli kuwa hili tatizo la umeme linatuathiri zaidi wananchi wa kawaida kuliko viongozi ambao kwa bahati mbaya ndio wanapashwa kushughulikia tatizo hilo.

  Nasema wanafanya mambo ya kipuuzi sana sababu ya kushindwa hata kuwa na uhakika wa umeme kwa watumiaji ambao ni chini ya asilimia 14 ya watz takribani milioni 40.

  Katizo la umeme kwa zaidi ya saa 12 kwa siku (mfano Arusha) halafu viongozi wanazunguka huku na kule wakati wanashindwa kupata ufumbuzi.

  Ni tatizo gani lilowakuta TANESCO ambalo limekuwa emergency kiivyo? Je ni maji? au vipuri au ni upuuzi wa mikataba ya Ki-Karl Peters.

  Mnisaidie jamani hivi huyu Minister wa energy na mining ana-minister nini? Mimi ndio maana napata shida kweli nikifikiria haya mambo watawala wanayotufanyia watanzania kwa kisingizio cha kuwa Tanzania ni nchi ya amani. Watu wanatoa majibu ya jumla na kirahisi tu kwa sababu vyovyote watakavyosema no body anaweza kuuliza kwa sababu viongozi ktk nchi hii hawawajibiki kwa wananchi!! Shame. Utasikia maneno kutoka kwa viongozi kama haya hii ni hali ya kawaida hata nchi fulani inatokea!! Nonsense tupu. Watz tubadilike viongozi mtoe leadership kama haiwezekani msikimbilie na kulazimisha kupewa vyeo wakati hamna uwezo.

  Naomba wana JF tujadiliane kwa maana ya kujenga. Hali ni mbaya kuliko maelezo.
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  hebi fikiria mtu mzima anaulizwa tena mkuu wa kaya...mna matatizo gani nchini ...nae akajibu..tunasumbuliwa malaria!!!..
  akaulizwa tena kwa hiyo tukusaidie nini.....akajibu...naomba mnipe vyandarua!!!... huu ni upuuzi wa hali ya juu sana.

  huyu mwingine eti wazir mkuu..kakataa gari kisa lakifahari sana haliendani na hali na kusema apewe mtu mwingine...kana kwamba huyo mwingine atakuwa analilisha uji....halafu hapo hapo hakushilikishwa wakati wa maamuzi ya kukunua magari......sasa hapo unaweza kusema kuwa tuna Waziri mkuu?? au tuna waziri mkuu kivuli....kwa hiyo linapokuja swala nyeti kama holi la umeme kwa mtindo huu hakuna suluhu yenye maana.....tayari keshaanza kuzurula wakati huko alikokwenda hata angenituma mimi ningrmwakilisha vema.....

  kila siku anasema tatizo la umeme litakuwa historia....ananidhi sana huyu jk
   
 3. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu nimekuelewa, halafu hapa kwenye kukutumia wewe ni mhimu sana. Nafikiri kuna umhimu wa kuanza kuwatumia wanachi wa kawaida kwenye kazi kama vile anavyokwenda kuomba vyandarua na dawa mseto.

  Nafikiri hii itasaidia kupunguza matumizi ya kodi za wananchi, kwani gharama za ulinzi zitapungua na msafara pia na hii itapelekea kupunguza matumizi kwa kiasi kikubwa.

  Suala la mgawo wa Tanesco ni kichefuchefu
   
 4. FuturePresident

  FuturePresident JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 322
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Management ile ile y a shirika, mkuu wa kaya yuleule, Waziri wa wizara yule yule na matatizo yale yale kilichobadilika hapa ni this time kwa kasi zaidiiiiiiiiii...........wakubwa no need to complain..........eti bongo its a Island of peace :embarrassed:
   
Loading...