Hizi ngonjera hazilisaidii Taifa.Mkuu hiyo taarifa CAG unayoisema ndo ile ile iliyokabidhiwa kwa Naibu Spika then PAC na Wabunge au hii ni nyingine.Wakati kukiwa na taarifa zilizochapishwa kwenye vyombo vya habari kuwa akaunti ya escrow iliyofunguliwa benki kuu ( BOT ), kwa mujibu wa makubaliano yaliyofanyika julai 5, 2006, zilikuwa sh bilioni 306.6, kabla kutolewa kwa fedha hizo mwaka 2013, taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ( CAG ), imethibitisha sio kweli.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya CAG , ambayo Rais Kikwete ameagiza iwekwe hadharani, ili Watanzania waisome na kuielewa, katika ukurasa wa 40 mpaka 42 imebainika kuwa kiasi cha fedha kilichokuwa katika akaunti hiyo, kilikuwa Sh bilioni 182.7. Ambapo TANESCO iliweka kiasi cha sh bilioni 142 na wizara iliweka sh bilioni 40.7, taarifa hiyo ilieleza.
Ripoti hiyo imebainisha kuwa, kama akaunti hiyo ingekuwa na sh bilioni 306.6 basi TANESCO wangepaswa kuweka kiasi cha sh bilioni 123.9 zaidi ya fedha zilizowekwa katika akaunti hiyo.
Kutokana na hali hiyo, mpaka sasa IPTL inaidai TANESCO sh bilioni 123, ambazo ni nyingi kuliko kodi ambayo TRA inaidai IPTL, ya sh bilioni 26.9.
Nikuazime usafiri uwahi mkuu?Hata mimi ngoja nikampigie Mwenyekiti toka CCM.....KUMBE WALIKOSEA ISSUE YA ESCROW?
Kwel ujinga ni mzigo
serekali iwalipe haraka kina Seth Sigasinga kumbe walikosea!
​
Hii ni kutokana na report ya CAG katika ESCROW account
View attachment 212456
View attachment 212457
View attachment 212458
- Ushauri huu ni sahihi kisheria?
- Na je Capaity charge/Demand charge hukokotolewa kutokana na gharama za uwekezaji (Mitambo ya Megawat 100 kwa IPTL) au mtaji wa wanahisa unaoonekana kwa msajili wa makampuni?
- Kama ushauri haukuwa sahihi, ni nini lilikuwa lengo la Mkono kupitia kampuni yake ya uwakili kutoa ushauri wa namna ambao ulipelekea Tanesco kuanzisha madai kwa IPTL
Wajuzi wa sheria mnisaidie
Mkuu huo ndio ushauri wa Mkono sio mimi, soma vipande hivyo vya taarifa ya CAG nilivyowekaKwa UELEWA WAKO HIYO ELFU HAMSINI INATOSHA KUNUNUA HATA WAYA?ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA YA KWAKO!!
Ni muda sasa umepita toka sakata la uchotwaji wa pesa za Escrow ulipobainishwa na mbunge aliye maliza muda wake Bw. Kafulila, tukashuhudia malumbano ndani ya Bunge ambayo yalitishia uhai wa uwaziri wa Mh. Pinda na mengi yakasemwa. Kuelekea uchaguzi mkuu tungependa kupata ukweli wa Escrow na watu waliochukua pesa kupitia Stanbic Bank. Nawasilisha
Ni muda sasa umepita toka sakata la uchotwaji wa pesa za Escrow ulipobainishwa na mbunge aliye maliza muda wake Bw. Kafulila, tukashuhudia malumbano ndani ya Bunge ambayo yalitishia uhai wa uwaziri wa Mh. Pinda na mengi yakasemwa. Kuelekea uchaguzi mkuu tungependa kupata ukweli wa Escrow na watu waliochukua pesa kupitia Stanbic Bank. Nawasilisha