Jf doctors- nisaidieni mkono wangu upone. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jf doctors- nisaidieni mkono wangu upone.

Discussion in 'JF Doctor' started by kvelia, Jun 12, 2012.

 1. kvelia

  kvelia JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndugu zanguni wataalam, nina tatizo la muda mrefu. Nikiwa kijijini kama mwaka na nusu uliopita nilikuwa namwelekeza ng'ombe kwenye zizi lake ghafla akanivuta na mkono ukauma sana. Nilienda hospitali nikapigwa X-RAY doctor akasema hakuna mfupa ulioteguka wala kuvujika, nilipewa dawa za kutumia kama mwezi hivi. Nilipata nafuu lakini baadae kama miezi sita hivi kipindi cha baridi mkono ukauma tena na haufai kabisa kufanya kazi yeyote. Nauliza kuna uwezekano nikapona na niende wapi, NISAIDIENI JAMANI, TATIZO NI NINI. Natanguliza shukrani
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Pole sana kwa kuumwa namkono fanya hivi. Tafuta Karafuu gramu 50,Pilipli mtama gramu 50,Tangawizi kavu gramu 50 vitu hivyo vyote twanga uchekeche upate unga wake Uchanganye na na siki ya Zabibu ( Vinegar) Au siki ya Apple (Apple cider) chupa moja uwe unajipaka kila siku asubuhi na usiku kwa muda w siku 7 inshallah akipenda Mwenyeezi Mungu utapona . tumia kisha unipe feedback...@kvelia

  ukisha maliza kujipakaa hiyo dawa tafadhali uoshe viganja vyako vya mkono uliotumia kujipaka kwani hiyo dawa inakuwa ni sumu haifai kwa kunywa ni ya kujipaka tu
   
 3. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Ushauri mzuri sana
   
 4. kvelia

  kvelia JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nashukuru sana MziziMkavu, nitaanza kutafuta hayo material, kisha nitakupa feedback, Mwenyezi Mungu akuzidishie.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...