Nimeamka kisha nikawaza, nikaona ingekua poa sana kama kungekua na app ya JF ya windows 8/8.1, ingependeza sana, iwe na features kama instant notifications, instantnotifications za subscribed threads... Na ikiwa na Live tiles itapendeza sana kwenye start screen...
Najua ipo ya simu...
Wenye windows 8/8.1 plz support this...
Kuna siku nilitoa hilo wazo kwa Invisible na kumuomba nitengeneze desktop application yenye features kama ulizozitaja @wickerman na nyingine nyingi including chats n.k but sikupata majibu niliyoyatarajia kwani kuna vikwazo vya kitekniko ambavyo vilikuwa nje ya uwezo lakini cha msingi hii kitu ni muhimu kwani kufungua browser kunatia uvivu.
Lakini kwa upande mwingine nadhani JF wanaogepa kujikita kwenye mobile & desktop apps kwa ajili ya kuogopa matangazo yao kama ya AdSense na mengine kusosa viewers... so bado kunachangamoto nyingi, ila tuwe wavumilivu nadhani vitakuja muda sio mrefu.
Daaah tena ingepatikana Metro App ingekuwa raha sana lakini labda kwa badae sana kwani nnavyojua mimi JF haina programmers wa kutengeneza hizi app kwa sababu wanategemea app ambazo zinakuwa customized special kwa vBulletin... Forums
Ushauri wangu. JF tafuteni madevelopa muwape hela wataifikisha JamiiForums mbali kwa sababu wataleta vitu vipya....
JF kuwa hivihivi siku zote inaboa watu wanahitaji mabadiliko kadri yanavyotokea.