Jeuri ya Serikali ya Tanzania

jiamini360

Member
Jan 26, 2016
35
19
china-is-very-busy-milking-africas-resources.jpg

Mpaka sasa China imedhamini miradi takribani 62 Tanzania kupitia soft loans na aid hii pamaoja na £1.3b ya pipeline ya gesi Dar-Mtwara. Na mpaka sasa Tanzania ni Nchi ya pili kwa kupata mikopo na misaada kutoka china ambayo si chini ya $5b.

Pesa za MCC si kitu kwa seriakali ya Tanzania. Kwa sababu ya hili taifa la China, hili ni moja ya taifa kuu kiuchumi duniani na wanatengeneza mausiano kabambe na viongozi wa Afrika kwa sababu ya lasilimali zilizopo Afrika mfano Congo kuna malighafi zinazotumika kutengeneza simu,tablets n.k, Tanzania gesi, madini n.k, Kenya mafuta.

Serikali ya China nadhari(theory) yake ni Tupatie tunachohitaji na sisi tunakulipa kwa kukupatia misaada(aid) soft loan na trade pact bila kujali kuhusu demokrasia wala mambo ya haki za binadamu nk.

Sasa kwa theory ya China inatosha kabisa kukuonyesha jeuli ya serikali inatoka wapi.
11-2-africas-natural-resources.jpg
 
50 mins ·
Uzalendo ni kutaka haki ya kidemokrasia Zanzibar. Haki ya Wananchi waliochagua viongozi wao oktoba 25, 2015. Sitakubali kuvishwa koti la uzalendo kwenye suala la MCC. Hilo ni suala la CCM, kukosa misaada ya Marekani ni matokeo ya ubabe wa CCM kuhusu Zanzibar. Haina mahusiano yeyote na Uhuru wa Nchi yangu. Nawasihi Wazanzibari wawe na subra Mola kamwe hatawatupa. Haki itapatikana tu. ‪#‎DemokrasiaTu‬. Nawasihi Watanzania kuelewa kwamba CCM ndio imetufikisha hapa na iubebe mzigo huu bila kufanya ni mzigo wa Nchi
zanzibar.jpg
 
Hii ndo akili ya mbele kwa mbele hasa
Shetani mpya usiyemjua ni bora kuliko shetani wa zamani unayemjua.China ni wazuri zaidi.Misaada yao haina masharti kama ya wamarekani.
Hii ndo akili ya mbele kwa mbele hasa
 
Urusi juzi juzi vikwazo akaanza lia lia
Nyinyi ni kina nani?
Nq msipoangalia bomba la mafuta litapita Kenya
 
Washauri wake wakubwa ni wana-CCM, ambao kimsingi wapo tayari iendelee kukaa madarakani hata kama tukitengwa na dunia nzima

Tatizo linaweza kuwa yeye(raisi) ndio anawashauri washauri wake (aambiliki)
 
kitu kimoja ni kutambua kuwa nchi nyingi haziwezi kupeleka fedha nyingi hivyo katika nchi na zikapotelea huko.

wanaangalia kuingiza fedha zikawapumbaza alafu wanachukua zaidi ya kile walichokiweka.

mambo ambayo yanatajwa kama vigezo sioni mabadiliko makubwa katika siasa za tanzania bali mabadiliko ninayaona katika sera za uchumi.

kusema wageni, sijui mikataba ya kifisadi, haya yote wamepima wakaona fedha zitakuja na zitabaki nyingi na wao hawata pata. china na wao kanuni zao ni hizo hizo maana wewe unaangalia fedha iliyokuja hutizami fedha inayokwenda kwao kupitia bidhaa na makampuni ya ukandarasi.

tatizo la JPM ni kupiga kelele kwenye majukwaa maana ukiwatisha hawa jamaa wanachukua hatua za kujihami.

ni lazima JPM afanye jitihada kuhakikisha mbinu zake za kiuchumi zinakuwa na tija maana kama ni kelele tu akidhani uzalishaji utabaki palepale huku yeye akibana wageni na kuzuia fedha zisitoke tu ajue uongozi wake utasababisha hali mbaya ya kiuchumi maana fedha nyingi zilizokuwa zinakuja hazitakuja.

lakini afanye mambo bila kuwapigia kelele wageni bali wakija kuguta wanaona mambo yamebadilika, kwa njia hiyo tunakuwa na transition period. mabadiliko ya ghafla ya kupiga kelele watu wakazuia fedha zao zisije ghafla yatawaumiza watanzania maana wanahitaji mda wa kutoka kwenye hali ya sasa ya kutegemea nje mpaka warudi kutegemea ndani.

View attachment 333242

Mpaka sasa China imedhamini miradi takribani 62 Tanzania kupitia soft loans na aid hii pamaoja na £1.3b ya pipeline ya gesi Dar-Mtwara. Na mpaka sasa Tanzania ni Nchi ya pili kwa kupata mikopo na misaada kutoka china ambayo si chini ya $5b.

Pesa za MCC si kitu kwa seriakali ya Tanzania. Kwa sababu ya hili taifa la China, hili ni moja ya taifa kuu kiuchumi duniani na wanatengeneza mausiano kabambe na viongozi wa Afrika kwa sababu ya lasilimali zilizopo Afrika mfano Congo kuna malighafi zinazotumika kutengeneza simu,tablets n.k, Tanzania gesi, madini n.k, Kenya mafuta.

Serikali ya China nadhari(theory) yake ni Tupatie tunachohitaji na sisi tunakulipa kwa kukupatia misaada(aid) soft loan na trade pact bila kujali kuhusu demokrasia wala mambo ya haki za binadamu nk.

Sasa kwa theory ya China inatosha kabisa kukuonyesha jeuli ya serikali inatoka wapi. View attachment 333243
 
Ngumu kumesa...

Ila JPM kaanza vibaya sana aiseee
We kweli taka taka kabisa kaanza vibaya kwakuwa tumenyimwa misaada? Kama mmechoka kuishi nchini nendeni marekani!

Ni bora watunyime ili tujifunze kujitegemea..na nyie nendeni mkafanye sherehe ya kunyimwa misaada!
 
--->>Naamini rais magufuri hakuona ubaya wowote wa seif kuongoza Zanzibar // nadhani kuna ushauri mbaya ulipita .......!?
uliokuwa na dhamira ya snitch / dont-go-fast.
 
Back
Top Bottom