Jeshi na ukombozi wa Mtanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi na ukombozi wa Mtanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Godwine, Mar 22, 2010.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  taifa linaendelea kuibiwa na mafisadi wageni na wazawa, umaskini unaendelea kushamiri, amani inaelekea kutoweka mfano mara, viongozi macho yote kwenye uchaguzi ujao, je umaskini wa watanzania waliochoka unanafasi gani ?
  nani mkombozi wa maskini?
  jeshi linanafasi gani katika kumkomboa mnyonge na kulinda rasilimali zetu na kuzuia ufisadi?
   
 2. Moderator

  Moderator Content Quality Controller Staff Member

  #2
  Mar 22, 2010
  Joined: Nov 29, 2006
  Messages: 479
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Badala ya kutumia shortcuts za Kijeshi, tuwaelemishe wananchi kutumia vizuri kura zao na kulinda demokrasia.
   
 3. G

  Godwine JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  lakini tume ya uchaguzi ni mali yao, unadhani ni mpaka lini wananchi wataendelea kuteseka?
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Unafikiri wananchi wataelewa kwa shule zetu za kata?
   
 5. G

  Godwine JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  jamani ukienda vijijini wananchi wanateseka naomba watz watambue ya kuwa watu wa vujijini na ata wa mijini wanaoteseka ni ndugu zetu
   
 6. G

  Godwine JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kuna wakati ambao taifa linashindwa kuwa na uelekeo kama tulipofikia sasa . nadhani ni wakati muhafaka kwa jeshi kulazimisha vyombo vya utendaji na siasa kuwajibika kwa namna yeyote kwani katika nchi yetu jamii inaendelea kupoteza tumaini ambacho ni kitendo kibaya zaidi katika historia ya mataifa yote;

  je hakuna namna yeyote ya jeshi kulinda rasilimali zetu?
   
 7. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #7
  Apr 11, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Godwin 60% ya bajeti yetu inategemea kupata msaada kutoka nje, kila kona ya duniani dhana ya utawala bora na demokrasia vimeshika kasi, wanajeshi wakiingia hali itakua ngumu zaidi., kwani tutatengwa, wa TZ hawajachoka na sidhani kama watachoka hivi karibuni wakichoka wataingia barabarani na watapiga kambi kwenye mjengo karibu na soko la samaki wakiwataka watawala wao wang'oke!
   
 8. G

  Godwine JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  unadhani mataifa yanayotoa msaada hayanufaiki na taifa letu? tz ni nchi tajiri kuliko wanaotupa msaada; kwani tuna madini na zaidi tambua kwamba gesi tuliyonayo inamnufaisha mgeni na tunaambiwa kwamba songgas inajiendesha kwa hasara; watanzania wanatakiwa kutoogopa tawala za kijeshi kwani kuna nchi ambazo tutaendelea kufanya nazo biashara kama china cuba venezuela; nadhani imefika wakati wa kuweka namna ya kampuni za kigeni lazima kugawa hisa kwa serikali na hii inaweza kufikiwa kwa shinikizo la kijeshi kwani BUNGE NA VYAMA VYA KISIASA vimeshindwa;
  jeshi lina nafasi gani katika hilo?
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe Mtumishi. Naamini wananchi ni jeshi linalofaa kufanya mapinduzi haya
   
 10. G

  Godwine JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  mpitanjia lakini ni lini wananchi wa tanzania wakapata upeo japo wa kutambua haki zao kwa nionavyo mimi ni kuendelea kuteseka na kupokea zawadi za kanga katika chaguzi, mbona naona wananchi wamepoteza uelekeo pia, unadhani ni tatizo gani wanalo wananchi wa tanzania na viongozi wake kutothamini utaifa wao na kuuza rasilimali za taifa lao, kwanini nchi imefika hapa ilipo?
   
 11. c

  care4all Senior Member

  #11
  Apr 11, 2010
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona hukupitia JKT wewe ndio maana unawahitaji sana hao jamaa kwenye utawala...Raia hatapewa nafasi au hata uhuru wa alionao sasa, afande hakosei bwana na nilazima uti amri yeke kwanza ndipo uhoji/ulalamike pia utapigwa mapororo (pololo) weee!....Mwenyakiti wa CCM and Katibu Mkuu si WAJESI au kwa vile hawavai magwanda?...makuruta (hasa volvo) mara ngapi wamewatembezea wananchi mkong'o bila sababu za msingi....uongozi wa kijeshi Nigeria ulifanikiwa vipi kuondoa mafisadi? Toa mfano wa nchi hasa Africa ambayo imefanikiwa kwasababu inaongozwa kijeshi.....wale wanafundishwa jinsi ya kuvizi na kuua tu ( kuua mtu adhaniwaye ni adui) hawajaandaliwa kwa mambo ya siasa au utawala...unataka kuwa mtu wa ndiyo afande?
   
 12. G

  Godwine JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Care4all tambua kwamba wanajeshi wetu wa bongo ni wastaharabu hawatatesa wananchi zaidi ya kusimamia
  rasilimali nadhani watatawala kwa kipindi cha mpito tu then wawaachie raia kwani Comoro mbona wamepindua
  nchi then wakawaachia raia wenye malengo pasipo na ukandamizaji , je unafahamu Comoro wemesaidia
  kuleta haki na kulinda rasilimali za nchi, tazama tz wafanyakazi wananyanyaswa , wakulima ndo usiseme,vijana
  wanageuzwa wapagazi wa siasa yani kushangilia baba wa wenzao kwenye kampeni, rasilimali za taifa zinachukuliwa
  na wageni, kwenye biashara wazawa wamebaki wachuuzi wa ndizi na maembe,
  je jeshi aliwezi kuweka shinikizo la kuleta haki na kuacha raia waendelee kujitawala kwani Bunge na mahakama
  zimebaki watazamaji tuu?
   
 13. m

  matawi JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wakuu wa nchi wanajua hatari ya jeshi kusaidia wadanganyika ndo maana vigogo wengi wa jeshi hupewa rushwa ndefu kama mzee mboma alivyokula mgodi wa makaa ya mawe
   
 14. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #14
  Apr 11, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Ni jeshi la wananchi si jeshi la uvamizi au la ugandamizaji" Benjamin.w.Mkapa
   
Loading...