Jeshi La TZ limejifunza nini MISRI? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi La TZ limejifunza nini MISRI?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MVUMBUZI, Feb 12, 2011.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Ustaarabu na uwezo wa kufikiri, uvumilivu na kukataa kuburuzwa kwa maslahi ya watawala dhalimu ni LEARNING EXPERIENCE ambayo Majeshi ya Misri na Tunisia yameonyesha.

  Tulichoona ni kwamba majeshi ya Misri na Tunisia yameweza kwa kiasi kikubwa kupambanua nafasi yao katika nchi. Wanajitambua wako kwa ajili ya nini na nani na ndio maana wameweza kuwa facilitators badala ya stumbling block kwa mabadiliko yaliyotokea nchini kwao.

  Wameweza kupima kila amri waliyopewa na wakubwa kabla ya kukurupuka na kuitekeleza
  Ni dhahiri wanajua si lazima kutekeleza kila amri wanayopewa na wakubwa bila kuangalia maslahi yake kwa walio wengi.

  Kwa namna hii wamejua wao wako kuilinda nchi na raia wake na siyo kuwaua wale waliopewa thamana kuwalinda maadam wanachofanya siyo dhambi wala uvunjifu wa sheria bali kudai haki.

  Hebu tuje hapa kwetu Tanzania.

  Tofauti iliyopo kati ya majeshi ya Tanzania haswa kuhusu mtazamo wao kwa raia ni sawa na usiku na mchana.

  Majeshi ya Tanzania wana perceive kuwa jeshi maana yake ni ubabe, amri, kutosiliza kupiga na kufanya unacho amriwa na amiri Jeshi mkuu
  Polisi wanafurahia na kushabikia kuwapiga wanafunzi wenye mabango tu kwa mabomu ya machozi bila kufikiri kwamba anaweza kuwepo ndugu yake au mtoto wa rafiki yake. Polisi bila kujua kwamba

  Polisi wanaua tu raia eti kwa sababu wakubwa zao hawataki watu wafanye maandamano ya kuwapongeza wapiga kura wao kwa kuwachagua.

  Polisi wetu na majeshi mengine huwa fahamu zao wanaacha nyumbani na kutumia fahamu za wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, ma OCD na RPCs. Hawatumii utashi wao kwani wamekuwa kama mbwa ambao mara zote wanataka kutikisa mikia kuwa please mabwana zao.

  Je Watanzania leo tukiamua kuleta mabadiliko kwa namna walivyofanya Misri na Tunisia polisi na Jeshi wataua watu wangapi? Je kwa kiasi gani jeshi letu JWTZ inaweza vumilia kuona raia wanapanda juu ya vifaru na kuwakumbatia?

  Nasema Polisi na Jeshi la TZ kwa kiasi kikubwa wamekuwa na wataendelea kuwa kikwazo kwa mabadiliko ya kiraia hapa TZ na wasifikiri wataepuka kuwa waathirika wa viongozi wabovu. Kigezo cha nidhamu ya kijeshi kitaendelea kuwatesa iwe ni umaskini kutokana na uongozi mbovu hadi pale watakapofunguka macho kama wenzao wa Misri na Tunisia

  Hii ni changamoto kubwa kwa majeshi ya Tanzania ambayo utendaji wao unategemea utashi wa wakuu wao na viongozi watawala wa kisiasa ambao hutumia vyombo hivi zaidi kulinda maslahi yao binafsi. Majeshi yetu yamekuwa kama ROBOTI ambazo hazina akili zao wenyewe bali remote ya wakuu wao na akina makamba, mwana wa mkulima na mwanakijiji wa Msoga.

  FUNGUKENI NA JIFUNZENI KWA WENZENU ACHENI KUWA ROBOTI.
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hii imekaa vizuri. Sijui kama hao jamaa watakuwa wamejifunza chochote. Shida ni kwamba wale wakubwa wengi walio kwenye majeshi hayo wanawezakuwa wanafaidika na ufisadi ulio katika serikali. Kuiondoa serikali ya kifisadi inaweza kumaanisha kuwakosesha maslahi binafsi wakubwa wa vyombo hivyo. Kumbe wakubwa wanaweza wasikubaliane na mabadiliko.

  Kingine ni military training yetu. Inasisitiza zaidi utii wa upofu kwa kiongozi hata kama anaamrisha jambo la ajabu. Hawafunzwi kufanya discernment ya jema na ovu na kufuata jema. Bali kwao amri tu!!
   
 3. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  wanatakiwa wa badilike kwa hakika wasisubiri mpaka walowe damu za watanzania siku ambayo raia hawataona tena thamani ya uhai kama haki yao na watoto wao itaendelea kupigwa roba na mafisadi wachache wanaotumia dhamana ya uongozi wa umma kwa maslahi yao na familia zao.
   
 4. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Professionalism waliyoionyesha ni ya hali ya juu na ya kutukuka. Ni mfano wa kuigwa kwa kila mtu ambaye kwa hiari yake ameamua kuvaa sare, kama mlinzi wa nchi na mali zake. Sare ile wanayovaa ni kielelezo wazi cha ukuu wa kazi wanayoifanya. Lakini cha kushangaza, wengine hawajui hata thamani ya kuvaa vazi lile wanakubali kuwa sehemu ya kutekeleza mipango ya kisiasa tena kwa gharama yoyote. I hope Arusha tumejifunza na tutaanza kufanya tofauti kwa kuiga mambo ya Egypt na Tunisia!!
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  LAITI JESHI LA MISRI LINGEKUA LINAENDESHWA KWA MISINGI YA
  KIITIKADI NA KISHABIKI ZAIDI KAMA BAADHI YA
  VYOMBO VYETU VYA ULINZI HAPA NCHINI LEO
  HII MISRI LINGEKUA MGENI WA NANI??


  Nadhani kuna upekee kule Misri kwa njia nyingi mno kuweza kujifunza mtu. Mojawapo ni ukweli kwamba Mubarak alipinduliwa na wananchi bila hata ya kuwepo mtu au kikundi chochote cha kuwaongoza isipokua tu azma yao ya kuwa watu huru na kulinusuru taifa lao na ufisadi.

  Ukweli huu ulidhihirika pale muda wajadiliano na serikali ilipofika na kukosekana kikundi chochote rasmi cha kujadiliana nalo. El Baradei japo kasaidia sana kuweka mambo sawa kwa upande wa waandamanaji, ukweli wa mambo ni kwamba alifanya kudandishwa tu treni iliokua kwenye mwendo tayari huku wengine wakiwa ndio wanapata kumuona kwa mara ya kwanza akitokea ughaibuni hivi karibuni tu. Kwa mantiki hiyo asingeipewa nchi wakati hata kona zake bado kuzifahamu.

  Omar suleiman (Othman wa Misri) licha ya kukubalika sana na mataifa ya Magharibi, naye ilishindikana kumuachia madaraka maaana kwa madai ya vilevile kero za kushabikia serikali ya Mubarak hata kwenye madhambi dhidi ya wananchi naye hadi leo hii nguvu ya umma haitaki kumuona jicho moja akiwaongozi - Misri ni zaidi ya darasa kwa idara zetu mbalimbali katika mataifa ya ulimwengu wa tatu. Lakini hapa kwetu; aaahh wapi, ajaifunze nani wakati sisi kila siku sisi ni mafundi karibia wa kila kitu na kutegemea tu uzoefu wa miaka ya 47 katika karne ya 21.

  Kama kweli tunalo taifa linalojifunza - kama si uchokozi wa makusudi kwa raia kwa KANUNI YA BUNGE ILIVYOPINDISHWA, MWENENDO WA KIMIZENGWE KANA KWAMBA TUNAENDESHA BUNGE KATI YA WATANZANIA DHIDI YA WAMALAWI VILE, CHAMA TAWALA KUJICHAGULIA VIBARAKA KAMA MIMOSA CHEYO KULISIMAMIA KWA NIABA YETU NA KUZUIYA CHADEMA HALALI YAKE NA KUBWA ZAIDI KITENDO CHA KUMWEKA MTUHUMIWA WETU NAMBA MBILI LOWASSA KWENYE KITI HICHO NI KANA KWAMBA CCM TAYARI INAJIANDAA NA VITA DHIDI YA RAIA WAKE KWA KUTETEA UFALME WA KIFISADI - LAKINI MUDA UKIFIKA WALA HAKUNA CHA LOWASSA WALA MJOMBA WAKE - KAZI KUTUTIA TU UMASIKINI HAPA KILA SIKU!!!!!!!!!!!

  Laiti ningalikua Mwamnyange, Mwema, au Othman; kitendo cha kusikia tu kijana wangu anatamba kwamba yeye ni KADA (Adengenya) wa chama hiki au kile, ni wa dhehebu hili au lile, ukanda huu au ule, au tu hata bila kusema ila udadisi wa mtendo yake yanaashiria hayo hapo juu basi moja kwa moja nitachukua hatua ya kumpa muda zaidi kuendeleza hicho anachokipenda zaidi akiwa nje ya jeshi langu.

  Matumizi mabaya yavyombo vya usalama, na hata kufikia mahala hata baadhi ya vyombo hivyo kuwa chini ya MILIKI NA AMRI BINAFSI lakini kuendelea kugharamiwa na wote ni jambo moja linalouma saaana, hutowesha haki upesi, kujenga chuki na watu kugeuka mbogo juu ya hilo.

  Kwa kweli laiti nalo jeshi la Misri lingegeuka kuwa mashabiki wa NDP na Mubarak jinsi ambavyo BAADHI ya vijana wake Othman na Mwema walivyohiari kuwa WATENDAJI WKUU katika mambo kibao yenye maslahi kwa kijikundi tu ndani ya CCM dhidi ya vyama vya upinzani, ambao licha tu ya itikadi zao tofauti, amba ni Wazalendo kweli kweli lakini unachagua tu kumnyima huduma na au kumkandamiza kwa kuwa KAMPINGA SHUJAA WAKO, nadhani nchi ya Misri ingeenda moja kwa moja mikononi mwao kikundi hatari cha Islamic Brotherhood na kulibandua hapo ingalikua mbinde tena!!

  Hakika hili ni dosari kwa baadhi ya watu ndani ya vyombo vyetu ambalo sisi kama raia walipa kodi tunayaona n a yanaweza kuyumbisha imani zetu kwenu kama si kuwanyima kabisa ushirikiano dakika mnapolihitaji zaidi kama hivi sasa vyombo vya dola vinavyowahitaji raia hivi sasa nchini Misri kuliko hata raia wanavyovihitaji vyombo vyenyewe.

  Kusema kwamba Mhe Kikwete sikubaliani na kwa kuwa kaingia madarakani bila ridhaa yetu hilo si sababu tosha kulifanya chombo changu cha ulinzi na usalama kisiendelee kunilinda usalama wangu na mali za kama ambavyo mkataba kati yangu na wewe kikatiba kukutunza kwa kodi yangu inavyoelekeza.

  Mwisho, mafunzo ya vyombo vyetu vyote ni sharti vibuni mitaala ya kuelewa mambo mengi sana yanayoendana na wakati ili kuto huduma bora zaidi, haki zaidi (ikibidi hata kuwakosoa na kuwakatalia wakubwa juu ya baadhi ya mambo yasiotuleta pamoja kama nchi yasitendeke), na kutambua ukweli kwamba Tanzania ni kubwa zaidi kulikohataa rais wa nchi. Leo hii Mubarak hayupo Misri lakini taifa lipo, Mwalimu Nyerere katangulia mbele ya haki lakini Tanzania bado linaendelea licha ya mapenzi makubwa tuliokua nayo kwake.

  lKwa kuhitimisha tu, napenda nirudie kwamba ushiriki wa kishabiki wa baadhi ya vyombo vyetu vya ulini na usalama kwenye mambo ya siasa nchini tangu Pemba, Unguja, Chaguzi zetu mbalimbali, mauaji ya Arusha na Mbarali, yote kwa pamoja ni miongoni mwa mambo ambayo yatachukua kipindi kirefu sana kurekebishwa, kuondoka vichwani mwetu na pia kurejesha imani na heshima kama zamani.

  Chukueni hatua za haraka, za wazi kutufanya tuamini kwamba mnaweza kuwa zaidi ya jeshi la Misri kwa hapa kwetu.
   
 6. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  tanzania hakuna Jeshi.
  Ile ni taasisi ya CCM...
  Tumeshuhudia Miaka kadhaa iliyopita ilikuwa ikikaribia uchaguzi Mahita alikuwa anakurupuka na kutoa maneno ya vitisho...

  Kama hiyo haitoshi mwaka jana akaibuka mwingine kutoka JWTZ nae akamwaga pumba zake....

  Sasa mpk hapo utagundua kuwa vyombo vya usalama ni wazi kuwa viko kwa maslahi ya CCM
   
 7. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  :clap2:Big up, jeshi la Egypt!!
  Majeshi yote ya Africa yaige mfano wao
   
 8. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Salute to people's defense army of Egypt!
   
 9. M

  Msenshe Member

  #9
  Feb 14, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnafikiri hapa kwetu yatawezekana kwa uwepo wa kina Shimbo??
   
 10. W

  We can JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nikuhakikishie, WANAJESHI WA TZ wanaadabu sana, tena sana. Ni wachache tu ndo wanalitia doa jeshi hili. Ktk majeshi yanayoheshimika Afrika, JWTZ imo. Ni kunguru wachache tu ndani ya jeshi ndo hawajui wajibu na nafasi zao. Heko JWTZ....Ni jeshi linalopenda wananchi saana tu. Hivi wewe hukushiriki Uchaguzi mwaka jana nini!
   
 11. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hebu tumwulize fisadi kamanda simbo amejifunza nini kutoka misri na tunisia
   
 12. M

  Masauni JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2011
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jeshi letu linavilaza wengi kama akina shimbo, hawajaenda shule wengi ni darasa la saba na form four, Siku jeshi letu likiwa na wasomi kama wanasheria, wachumi, engineers tunaweza kuona mabadiliko. Lakini kwa sasa msitegemee kitu kutoka kwa vilaza JWTZ
   
 13. k

  kirongaya Member

  #13
  Feb 14, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi hujui jeshini ufisadi ndio kwao, hayajaanikwa tu hayo ya dowans madogo ndugu
  sasa waachie tu muwatoe madarakani ili mfukunyue ya kwao mmmmh ngumu sana
   
 14. M

  MushyNoel Senior Member

  #14
  Feb 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  JWTZ wanatakiwa waelewe kwamba nao ni watanzania na ni wadau muhimu katika mchakato wa kimaendeleo wa nchii.Wasimamie maadili yao ya kazi na dhamana waliyopewa kwa ujumla wake - kulinda mipaka ya Nchi.

  Hawatakiwa wawe pro-utawala flani bali waangalie what is the best for the country.So when it comes a time citizen become so united agains bad behavior of those in high offices JWTZ must measure the impact of change.If is for better tanzania they should be pro such move.

  That we are in the midst of crisis is now well understood,corruption and lack of responsibility of our leaders.Social services are current costly a concequences of irresponsibility of those holding positions.

  There are all indacators that Nguvu ya Umma is innevitable and JWTZ must take it part in ensuring the safety of those protesting and never killing them.
   
Loading...