Jeshi la Sudan lashambulia Waandamanaji

Jeshi la Sudan lashambulia Waandamanaji

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,958
3 Juni 201
Vikosi vya ulinzi nchini Sudan vimetumia nguvu kujaribu kuwatawanya waandamanaji waliokita kambi nje ya makao makuu ya jeshi jijini Khartoum.
Kwa mujibu wa waandamanaji hao, milio ya risasi imekuwa ikisikika na tayari watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa kwenye rabsha hizo.
Sudan imekuwa chini ya utawala wa Baraza la Kijeshi la Mpito toka Rais Omar al-Bashir alipinduliwa mwezi Aprili.
Waandamanaji wamekuwa wakilazimisha utawala urejeshwe mikononi mwa serikali ya kiraia.
Jeshi la Sudan laafiki kipindi cha mpito cha miaka mitatu
"Kwa sasa kuna jaribio la kutawanya waandamanaji waliokita kambi," imeeleza taarifa fupi kutoka kwa Jumuiya ya Wataalamu wa Sudani amabo ndio waratibu wa maandamano hayo ya kitaifa.
Mashuhuda wanasema kuwa kwa sasa waandamanaji wanachoma matairi na kuweka vizingiti ili kuwazuia maafisa usalama kuwafikia.
Inaripotiwa kuwa mtu mmoja amepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa.
Waandamanaji wamekita kambi mbele ya makao makuu ya jeshi toka Aprili 6 mwaka huu, siku tano kabla ya Bashir kupinduliwa na jeshi.
Mwezi uliopita, viongozi wa waandamanaji na majenerali wa jeshi walitangaza kuwa wamefikia muafaka wa muundo wa serikali ya mpito ya miaka mitatu ambayo itaandaa uchaguzi wa kiraia.
Lakini wamesema bado wanatakiwa kufanya maamuzi ya nani aingie kwenye baraza huru ambalo ndilo litakuwa na maamuzi ya mwisho kwenye kipindi cha mpito cha miaka mitatu.
Hapajaweza kufikiwa makubaliano juu ya upande upi baina ya raia na wanajeshi uwe na wawikilishi wengi kwenye baraza hilo.
BBC
 
Raia wanataka utawala urudi kwao
Huku wajeda wamenogewa!

Ova
 
Uongozi wa nchi raha sana.
Sasa wajeda wana nafasi zao kijeshi tena kubwa tu za kufaidi nchi ila bado wanataka na kula tu.

Wakiwakabidhi raia nchi yao wao wanapungukiwa nini?

Na bahati mbaya nchi zetu za kiafrika viongozi wake ni zaidi ya mabeberu kwenye kuachia madaraka ndiyo maana lazima waue ili kujenga hofu kwa wengine ili wao watawale siyo kuongoza.
 
Haya mambo watu hua hawayaelewi, ni mara chache sana nchi ikichukuliwa na jeshi hua inatulia, wasiwafananishe na wazimbabwe ambao walimtoa raisi Mugabe kwa amani na baada ya siku kadhaa wakaurejesha utawala kwa wananchi, hiyo hua inakua ni bahati tu.
 
Wanajeshi wapumbavu wanaanzaje kutamani nafasi za kiraia!!!? Wakati mwingine umoja wa afrika na UN wapo kama picha tu,wanashindwaje kuingilia Mara moja hao wapumbavu wa kijeshi warudi kambini kwao??
 
Mara nyingi nchi ikishaingia kwenye mivurugano hua inachukua muda mrefu kutulia, yaani wale wasudani siku zote hua najiuliza kupiga kambi nje ya kambi ya jeshi ni ujasiri kweli kweli, halafu ni muda mrefu sasa tangu April.
 
Tabu imeanza baada ya kiongozi wa kijeshi kutembelea misri na saud arabia wakampa kichwa atumie mabavu dhidi ya raia,ujue sudani kuna struggle ya mataifa mbalimbali kucontrol sudan kwasababu ipo eneo muhimu pale Red sea,uturuki na Qatar nao wanastruggle kuhakikisha saud arabia hapati influence pale,kwahiyo ni suala la mda kabla haijawa full blown civil war
 
Tabu imeanza baada ya kiongozi wa kijeshi kutembelea misri na saud arabia wakampa kichwa atumie mabavu dhidi ya raia,ujue sudani kuna struggle ya mataifa mbalimbali kucontrol sudan kwasababu ipo eneo muhimu pale Red sea,uturuki na Qatar nao wanastruggle kuhakikisha saud arabia hapati influence pale,kwahiyo ni suala la mda kabla haijawa full blown civil war
Mapinduzi ya kijeshi sio suluhisho la matatizo ya kisiasa hapa Africa
 
Back
Top Bottom