Jeshi la Polisi Zanzibar latoa Ufafanuzi Kuhusu Madai ya CCM kutaka Seif akamatwe

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Jeshi la Polisi Zanzibar limetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa jeshi hilo linapanga kumkamata Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi, CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Taarifa zinazosambaa kwa kasi mitandaoni zinasema Maalim Seif anatakiwa kukamatwa kwa tuhuma zinazohusiana na kujitangazia ushindi katika uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015 kama inavyoshinikizwa na Chama cha Mapinduzi Zanzibar.

Akiongea na mwandishi wa Dw, Issac Gamba, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Kamishina Mkadam Khamis Mkadam, amesema yeye hajapata taarifa yoyote toka kwa wakubwa wake inayomtaka amkamate Maalim Seif.

Amesema jeshi la polisi ni taasisi kubwa inayohusisha viongozi mbalimbali, hivyo yaweza kuwa amri kama hiyo imetolewa kwa viongozi wengine
 
Wakubwa zake ndio hao viongozi wa CCM? Kwahio it is fine to conclude kwamba CCM na Polisi ni chombo ni mtu na Mkewe??
 
Akiongea na mwandishi wa Dw, Issac Gamba, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Kamishina Mkadam Khamis Mkadam, amesema yeye hajapata taarifa yoyote toka kwa wakubwa wake inayomtaka amkamate Maalim Seif.
Wakubwa zake ni akina nani? Viongozi wa CCM au wengine? Kwahio wakimpa taarifa (hao viongozi wa CCM) wataenda kumkamata
 
Wakubwa zake ni akina nani? Viongozi wa CCM au wengine? Kwahio wakimpa taarifa (hao viongozi wa CCM) wataenda kumkamata
Hawa ccm hawa! Hivi Elli mkuu wangu, jirani yako hata kama ana maguvu vipi akikuchokoza nawe ukamwambia hutaki ugomvi kisha ajakuona fala na kukufata mbele ya mkeo na wanao na kukuchapa makofi utaendelea kuwa muungwana?
Naanza kuona CUF WAMEKUWA pushed too much na wanaweza kulianzisha.
 
Halafu huwa mara nyingi unaishia kupigwa, nilishaona mara nyingi sana jamaa anavua shati kabisa au mtu anasema "jamani mshikeni nisije nikamuumiza huyu" Hahahahaa kinachotokea hapo ni kupewa kichapo cha maana. yaani anayetishia kupiga pamoja na mikwara mingi anaishia kupigwa. CCM waangalie sana
 
Huku Mdee huku Maalim Seif,majambazi wanapeta mitaani.
Ccm mnaitumia polisi vibaya
 
Back
Top Bottom