vampire_hunter007
JF-Expert Member
- Jul 25, 2015
- 1,034
- 2,599
Habari wakuu,
Tanzania imekuwa ikipata sifa nyingi sana kuwa ni kisiwa cha amani. Binafsi sifa hizi nazisoma kwenye magazeti tu ya hapa hapa kwetu sijui kama huko duniani pia tunasifa hii maana sijawahi toka nje ya Tanzania. Lakini wengi wanaoinadi sifa hii wamekuwa wakitafsiri neno Amani kwa kufanya comparison na nchi zenye machafuko. Of course hapo tutaiona Tanzania kama pepo.
Lakini tuiangalie amani ya nchi yetu kwa kuangalia usalama wa raia haswa katika maeneo yetu ya makazi. Ni maeneo machache sana katika nchi hii mtu unaweza kutembea barabarani saa tano au sita za usiku, au saa kumi alfajiri. Maeneo mengine ikifika saa mbili tu usiku unatembea kwa khofu. Nimetaja mida hiyo kwani kwa sisi walalahoi ndio mida ya kutoka na kurudi kutafuta tonge la siku.
Imekuwa kawaida sana swala la mtu kukabwa na kuporwa vitu. Bali maeneo mengine ni kawaida kabisa kwa vijana wa kihuni kuvamia maduka na kupora. Kama ilivyotokea hivi juzi maeneo ya Mzinga Kongowe, Dar es salaam. Huu ni mfano mmoja tu. Na huenda watu wengi hawajapata taarifa hiyo kwa sababu ni jambo lililozoeleka hivyo sio Hot news ya kusambaa.
Maeneo ya wakazi wa hali ya chini "Uswahilini" imekuwa kawaida watu kuporwa simu zao na mali zao nyingine mchana kweupe. Na imefikia hatua inajulikana kabisa kwamba njia fulani ukipita utaporwa tu. Maeneo ya waporaji yanajulikana na wezi na majambazi pia wanajulikana.
Ni kawaida sana kukuta maskani ya wahuni wakivuta bangi na kuwadhalilisha dada zetu wanaopita njia hizo. Wauza bangi wanajulikana na wavutaji ndio usiseme.
Hakuna amani. Watu wanajeruhiwa kwa kuporwa na wengine wakipata ulemavu wa maisha. Ni mambo ya kawaida katika jamii. Kiasi kwamba mtu anaweza kusema kumwambia mwenzake " Ile simu yangu niliporwa" na anayeambiwa wala asishtuke wala kuona jambo la hatari. Bali huenda muda mwingine akatumia kauli kuwa Simu washachukuwa wenyewe.
KAMA WEZI WANAJULIKANA KWA NINI JAMII ISIWASHITAKI?
Ni swali zuri. Lakini pia kama unakaa mitaa yetu ya Uswahilini huenda ukawa tayari una jibu.
Binafsi nimeshashuhudia zaidi ya mara moja watu wakivamiwa na kupigwa kwa sababu ya "Unoko". Wanaojitia "kimbelembele" kwenda polisi ndio wamekuwa wakishughulikiwa na kudhuriwa. Hao wezi na wahuni wanaoshitakiwa wamekuwa wakipata taarifa kuwa ni nani kawachongea na huwarudia kuwaadabisha. Maana wanaoshitakiwa baada ya siku kadhaa wanarudi mtaani. Hata wanaofungwa, aliyewashitaki hawi salama dhidi ya genge la mfungwa.
JESHI LA POLISI VIPI?
>Baadhi ya vituo vya polisi vunafungwa saa mbili au tatu usiku (nimeshuhudia)
>Polisi wanawajua wezi, wavuta bangi, waporaji lakini hakuna hatua wanazochukua.
>Polisi wengi si rafiki kwa raia, unakuta mtu aliyeporwa hata kama hana kosa lolote anaogopa kuingia kituo cha polisi
>Mitaa inayojulikana kwa waporaji wa wakabaji huwaoni polisi wakidumisha doria kulinda usalama
>Wamekuwa hawatilii umuhimu usalama wa raia kwa kuchelewa hata kufika maeneo ya tukio la jambazi na wizi
WAKATI HUO HUO
>Wamekuwa wepesi kuwakamata na kuwaweka ndani wanasiasa wa upande wa upinzani
>Utawakuta wakiwapiga raia (hata kama wana makosa) huku wakitushajiisha wananchi tusijichukulie sheria mkononi. Kama vile wao wapo juu ya sheria.
>Kuwakamata bodaboda kwa nguvu kubwa waliyotakiwa kuwakamata majambazi. Kijana anayejitaftia rizki yake anakamatwa katika hali ya kufa au kupona (Dead or Alive).
Mengine mtamalizia wakuu.....
Hawa ndio waliotakiwa kulinda usalama wa raia. Na raia watakapokuwa salama ndio amani itapatikana. Sasa hii hali itaendelea mpaka lini? Wizara husika haioni haya? Mh. Rais umeshateua baraza la mawaziri, huwezi kuwaamrisha mawaziri husika kutekeleza wajibu wao? Hali hii ya JESHI LA POLISI MPAKA LINI?
Nawasilisha