Jeshi la Polisi mmelitia simanzi Taifa zima

Jeshi la Polisi mmelitia simanzi Taifa zima

Shebbydo

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
1,174
Reaction score
1,937
Habari wana jf

Taifa zima lipo katika huzuni kubwa kutokana na kifo cha mapema cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT). Kifo ambacho kimesababishwa na utendaji mbovu na usiyozingatia sheria wa Jeshi la polisi.

Nadiriki kusema ni utendaji mbovu kwa sababu moja tu, kutumia risasi za moto kudhibiti maandano na vurugu za raia wasiokuwa na silaha za moto. Mimi binafsi nilisikitishwa sana na kauli ya wakuu wa jeshi la polisi walipokuja na kauli ya kwamba, kifo cha Aquilina ni cha bahati mbaya sana. Eti kwa sababu kimetokea kutokana na askari kupiga risasi juu ili kuzuia vurugu za waandamanaji. Swali moja la kujiuliza, hiyo risasi ipigwe juu, iweje tena irudi chini iende tena kwa ulalo (horizontally) imuue mtu? Au je kuna maaskari hawana mafunzo ya kutosha kutumia silaha? Majibu haya anayo aliyepiga risasi.

Laiti kama jeshi la polisi lingetumia weledi wake kuzuia vurugu hizo, haya yaliyotokea yasingetokea. Jeshi la polisi lina nyenzo nyingi za kupambana na vurugu za raia. Mabomu ya machozi, maji yanayowasha na virungu huwatosha kabisa kuwatawanya raia waliopagawa.

Lakini ni kwa nini kumekuwepo kwa utumiaji wa nguvu nyingi sana wa jeshi la polisi? Kwa mtazamo wangu nadhani ni kutokana na mambo haya;
Jeshi la polisi hivi sasa limebeba taswira ya kulinda mambo ya kisiasa na kutumiwa na wanasiasa. Kwa mfano, kitendo cha askari wake kuonekana katika studio za Clouds FM wakiwa na silaha katika tukio lililoonekana la kipuuzi kabisa ni ishara ya wanasiasa kujipenyeza ndani ya jeshi, kulitumia katik kutimiza malengo yao.

Kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa ngazi juu za kuwahimiza askari kutokuwa na mazoea na raia, wakati mwingine zikihimiza kutumia silaha, madhara yake ni haya. Askari anakwenda kutuliza vurugu rayari akiwa amejenga fikra kwamba hata nikipiga risasi ni sawa tu. Hili la Aquilina limebeba taswira hii kwa sababu Aquilina alikuwa mwanafunzi, je yeye ndiye wa kwanza kuuwawa na jeshi la polisi kwa risasi? Jibu ni hapana, nyuma kuna matukio mengi ya askari kuua lakini hayapewi uzito kama huu.
Hebu waandishi wa habari fuatilieni kilichojiri huko kanda ya ziwa katika operation ya Luhaga Mpina ya uvuvi haramu. Nendeni visiwa hivi vipo; Kweru mto na Bushengere vipo huko wilayani Ukerewe. Watu wamepigwa kama wanyama. Inasemekana wengine wamefia hospitalini kutokana na kipigo cha polisi. Wengine ni vilema sasa.

Jeshi la polisi nyinyi mnabeba dhamana kubwa ya usalama wa raia. Rai yangu kwenu rudini katika utendaji wenu uliotukuka ili yasijirudie haya ya Aquilina. Uhai wa mtu ukitoka haurudi tena. Hata ukifanya nini katika mazishi yake, hata ukitoa fidia ya mabilioni mangapi uliyemuua hapati chochote. Watakaofaidika ni wale waliobaki duniani wakiendelea kula ugali. Yeye atakuwa ameondoka kabisa katika uso wa dunia wala hatorudi tena kwa ajili ahadi zako. Kifo ndiyo adhabu ya mwisho kabisa kwa mwanadamu. Jeshi la polisi acheni kuleta simanzi kwa Watanzania. Nyinyi ni ndugu zetu, binadamu wenzetu na raia watarajiwa pindi mnapostaafu mnarudi kuishi na jamii kama raia wengine.
 
Tanzania hatuna icho kitu kinaitwa Jeshi la polisi...tuna kundi la wauwaji...waliobinafsisha vichwa vyao kwa wanasiasa wanachoambiwa ndicho wanachofanya bila hata ku reason. Kiikwel ningekuwa mchawi ningeloga polisi yoyote ninaekutana nae rod. Heri tuajiri lile kundi la panya road atleast wanatumia vichwa vyao kuliko haya majitu yanayovaa magwanda. Siwapendi na huo ndo ukweli. Na chuki hii inayozid juu ya hawa wauwaji na raia iko siku moja itawatafuna.
 
Naona chuki kubwaaa ikiongezeka kati ya raia na polisi.sijui nini kitatokea ikiwa mauaji yataendelea
 
Naona chuki kubwaaa ikiongezeka kati ya raia na polisi.sijui nini kitatokea ikiwa mauaji yataendelea
Kuna haja ya kujitathimini kama taifa tunakoelekea. Vinaweza kuchukuliwa kama vitu vidogo lakini athari yake ikawa kubwa.
 
Back
Top Bottom