Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linawashikilia jumla ya watuhumiwa 20 kuhusiana na tuhuma za mauaji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Taarifa kwa vyombo vya habari


Jeshi la polisi mkoa wa morogoro lina washikilia jumla ya watuhumiwa 20 kuhusiana na tuhuma za mauaji.

Mnamo tarehe 29/09/2021 majira ya saa 11 jioni huko maeneo ya kitongoji cha mgamba , kijiji cha dakawa , kata ya bwakila chini, wilaya na mkoa wa morogoro.

Juma s/o katinda ,58yrs, mkulima, mnyamwezi, mkazi wa dakawa, aliuawa na kundi la watu waliojichukulia sheria mkononi kisha mwili wake kuuteketeza kwa moto.

Chanzo cha tukio hilo ni kwamba, marehemu alichoma moto nyumba iliyojengwa eneo la karibu na jilani yake anayejulikana kwa jina la ruchamla.

Marehemu alikuwa safarini na aliporudi nyumbani aliona ujenzi huo ndipo alipo kuchukua uamuzi huo kwa madai yakwamba lile lilikuwa ni eneo lake.

Aidha baada ya marehemu kuchoma moto nyumba hiyo wananch walijitokeza ili kutoa msaada ila yeye alizuia watu wasitoe msaada ndipo wananch wakaitana kwa wingi kisha kumzingila na kumshambulia kwa silaha za jadi hadi ku muua kisha mwili wake kwenda kuuteketeza kwa moto.

Baada ya uchunguzi wakina na msako mkali tumefanikiwa kukamata watuhumiwa 20 na tunaendelea na kuwahoji ambapo 8 kati yao walikamatwa ndani ya bus wakiwa ktk harakati za kutoroko.

Mwisho

- Kamanda amefanya mkutano na wananch wa kata ya bwakila chini ulio udhuliwa na mwkt wa kijiji , diwani wa kata pamoja na mtendaji kata, kisha kuwataka wananch kuachana na vitendo vya kujichukulia sheria mikononi.

- Pia kamanda ametembelea na kuwapa pole familia ya marehemu iliyo okolewa ktk tukio hilo ambapo marehemu alikuwa na wake 03 , watoto, ndugu na jamaa jumla yao watu 11 na wamepata hifadhili kituo cha polisi duthumi.

Ahsanteni.

Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi

Fortunatus musilim

R.P.C Morogoro

IMG-20211002-WA0008.jpg
IMG-20211002-WA0007.jpg
IMG-20211002-WA0009.jpg
 
Ikithibitishwa na mahakama, sheria ifuate mkondo wake...

Inasikitisha sana...
 
Back
Top Bottom