JF-Expert Member
- Oct 29, 2012
- 1,889
- 1,127
Leo July 09 2019 Jeshi la polisi nchini limetoa ufafanuzi kuhusu tamko la kupiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya kisiasa kuwa tamko hilo lililenga kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na tamko hilo halikupiga marufuku mikutano ya kiutendaji na kiutawala ya vyama vya siasa inayofanywa kwa mujibu wa katiba na kanuni za vyama husika.
Hivyo jeshi la polisi linawataka watu wasipotoshe watu kuhusu tamko hilo na pale hali ya kiusalama itakapotengemaa, mikutano na maandamano ya vyama vya siasa itaruhusiwa kufanyika
Hivyo jeshi la polisi linawataka watu wasipotoshe watu kuhusu tamko hilo na pale hali ya kiusalama itakapotengemaa, mikutano na maandamano ya vyama vya siasa itaruhusiwa kufanyika