Jeshi la Polisi lifumuliwe, halina ubunifu na weledi!

Jeshi la Polisi lifumuliwe, halina ubunifu na weledi!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
18,616
Reaction score
30,925
Jeshi letu la Polisi limerithi mbinu na harakati za kazi ambazo sasa ni wazi limekuwa kama mzee kibogoyo.

Matukio ya hivi karibuni ya kuvamiwa vituo na silaha kutekwa sehemu mbali mbali nchini ni kiashirio tosha cha kuonyesha jinsi taratibu za jeshi hili zilivyochoka.

Haingii akilini kituo kikubwa kama Sitakishari kuvamiwa n armoury silaha kuvunjwa na watu kuondoka na silaha, na huku hakuna back up ya aina yoyote wala emergency road blocks kudhibiti hali hiyo.

Taratibu imani ya kwangu na pengine wananchi wengine imenza kuyoyoma.

Nanajiuiza kama viji Bureu De Change vidogo vinawez kuwa na kamera, vituo vikubwa vya polisi kwa nini viswe na kamera hizo, tena zinazokuwa connected na makao makuu kabisa?

Miji mikubwa yote ina kamera kwenye intersections zote, ikiwa njia rahisi kuliko zote kukusanya intelijensia.
Polisi ina maofisa wa kizamani sana wasiobadilika ili kwenda na maendeleo ya kisasa katika uhalifu.

Majambazi na wahalifu kwa upande mwingne wameendelea sana kwa kutumia mitandao na teknohama
Polisi asa hivi wanauliwa na kuynyaswa na wahalifu kwa vile wanatumia mbin za mwaka '47 mbinu za kufukuza mwizi kwa kirungu mtaani.

Badilikeni polisi.
 
ila mimi nadhani endapo polisi watapewa lungu, wahalifu wote watakwisha sema wanaogopa sana. maana nasikia hata polisi akiua jambazi inaweza kula kwake.
 
ila mimi nadhani endapo polisi watapewa lungu, wahalifu wote watakwisha sema wanaogopa sana. maana nasikia hata polisi akiua jambazi inaweza kula kwake.

Kuua si tatizo. tatizo liko katika mbinu za kizamani sana za kukusanya babari haraka na kuzitumia vizuri.
Kupiga wahalifu kwaweli ni ushamba, badala yakelazima kuwa na maabara ya forensic investigation pamoja na ukusanyaji mzuri na wa haraka wa data.
 
Jeshi la Polisi linachojua ni kupambana na upinzani, baada ya hapo linajitoa akili na kulala. Jeshi linaloongozwa na akili za kitoto
 
Polisi wooote wanakuwa kaunta ili kusubiri kodi ya hiari. Kwa maana hiyo kwa nje hakuna mlinzi wa kituo husika! na hii inatokea kwa sababu akiwa nje analinda wenzake ile michango(kodi) ya hiari hataipata! Kama huku uraiani unamweka mbwa kwa nje ili akulinde usiku ukiwa umelala inakuwaje polisi woote wako ndani ya kituo na kuuwawa kama mende kwa kutumia dawa ya Rungu????!!!!
 
Jeshi letu la Polisi limerithi mbinu na harakati za kazi ambazo sasa ni wazi limekuwa kama mzee kibogoyo.

Matukio ya hivi karibuni ya kuvamiwa vituo na silaha kutekwa sehemu mbali mbali nchini ni kiashirio tosha cha kuonyesha jinsi taratibu za jeshi hili zilivyochoka.

Haingii akilini kituo kikubwa kama Sitakishari kuvamiwa n armoury silaha kuvunjwa na watu kuondoka na silaha, na huku hakuna back up ya aina yoyote wala emergency road blocks kudhibiti hali hiyo.

Taratibu imani ya kwangu na pengine wananchi wengine imenza kuyoyoma.

Nanajiuiza kama viji Bureu De Change vidogo vinawez kuwa na kamera, vituo vikubwa vya polisi kwa nini viswe na kamera hizo, tena zinazokuwa connected na makao makuu kabisa?

Miji mikubwa yote ina kamera kwenye intersections zote, ikiwa njia rahisi kuliko zote kukusanya intelijensia.
Polisi ina maofisa wa kizamani sana wasiobadilika ili kwenda na maendeleo ya kisasa katika uhalifu.

Majambazi na wahalifu kwa upande mwingne wameendelea sana kwa kutumia mitandao na teknohama
Polisi asa hivi wanauliwa na kuynyaswa na wahalifu kwa vile wanatumia mbin za mwaka '47 mbinu za kufukuza mwizi kwa kirungu mtaani.

Badilikeni polisi.

Pole Jidula! Police as a law enforcement agency hapa Tanzania ilikufaga tangu 1995 nchi ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi, watawala wakaingia kwenye panic na defensive mode; wakaaanza polepole kuligeuza jeshi la nchi yetu kuwa Jumuia ya CCM kama vijana UVCCM, wanawake UWT na WAZAZI; ikazaliwa POLICCM; General police code; GPO kwa maana ya kanuni zinazoongoza kazi za jeshi la police ikawa inatokana na ILANI ya Uchaguzi ya CCM! upo bro?!, hiyo ndio summary ya safari ya anguko la jeshi letu la Polisi as a Law enforcement agency in Tanzania.
 
Kuna siku nilikuwa naangalia R.T nikakuta documentary ya retired detective. . . . . .Ukisikia masimulizi ya training ile unaweza pata picha kwanini tuko nyuma
 
Tatizo haliko polisi tatizo liko kwenye serekali yenyewe kwa kushindwa kuwekeza kwenye ulinzi kama nchi zingine ambazo huwa wanatumia gharama kubwa kwenye ulinzi.

Hata hizo camera unazozisema wanaotakiwa kununua na kuzifunga ni serekali na siyo polisi,utashangaa hata ulinzi huu kidogo unaofanywa na polisi asilimia kubwa utakuta wanagharamia wao wenyewe kwa kutumia fedha zao mifukoni.

Ndio maana utakuta askari wengi wanahangaika kuwatafuta wadau wa kuwawezesha ili kazi ziweze kufanyika bila kufanya hivyo kuna hatari ya kutokufanyika kazi za ulinzi kabisa.

Serekali kuwa mbali na polisi ndiyo chanzo cha wananchi kudaiwa hela za mafuta ya kuendeshea magari ya polisi wanapokwenda kutoa malalamiko vituoni,wanalazimika kutoa fedha za kununulia stationary,fedha za kusafirishia watuhumiwa n.k kwa hali kama hii kutakuwa na ulinzi wa maana hapo?.
 
Jeshi la Polisi limepitwa na wakati na linatumia mbinu za kizamani sana.
Mfano kwenye ujambazi uliofanyika pale kituo cha SITAKI SHARI-UKONGA, polisi walikuwa hawana haja ya kumwua mmoja wa majambazi ambae baada ya kupigwa risasi ya mguuni alisha-surrender lakini ukiiskiliza mojawapo ya ile klip ya hili tukio unaskia askari wa kike anasema "...bado hajafa mlenge ya kichwani..."na kweli akalengwa ya kichwani na kufa papo hapo. Sasa wanapata wapi ushahidi wa kuanzia katika kuyakamata na kutokomeza uhalifu wa namna hii?? Pengine yule jambazi waliyemwua mwisho ambae tayari walishamdhibiti kwa risasi ya mguu ndie angekuwa main source of all the information kwao. Lakini kwa vile wenzao wameuwawa, nao wameamua kuwauwa majambazi pale ovyo ovyo.
Thinking capacity ya Polisi wengi ni vilaza na ndio maana umeona baadhi ya maiti za polisi pale kituoni zimevaa yebo yebo, polisi upo kwenye lindo utavaaje yebo yebo??
Jeshi lote lifumuliwe na wasipofanya ivyo ipo siku watavamiwa pale central na Kova akiwa mle ndani.
 
Huu ni mtazamo wangu ambao umeegamia kiimani zaidi.
Mimi ni shabiki mkubwa wa makala za Mwl Mkuu wa Watu Mzee Pascally Mayega za kwenye Tanzaania Daima kila jtano.
Siku zote amekuwa akisema katika makala zake, vifua na mioyo ya wananchi wengi wa TZ imevimba kwa hasira na chuki kwa jeshi la polisi, na hii imetokana na madhila na maonevu mengi jeshi hili linavyo wafanyia wananchi. Mara ngapi utasikia jeshi lina bambikia watu kesi, jeshi linatesa watu mpaka vifo nk nk mfano akina Mwakiongosi wamepotezewa uhai wao mikononi mwa polisi nk nk., Dr Ulimboka alivyoteswa na watu wa TISS etc etc.
Sasa hauwezi fahamu and this is my perception, labda Mungu kufuatia kilio cha waja wake ambao wamekuwa wakiteswa sana na hawa ma polisi ndio anawajibia kwa kuwapa polisi mapigo mbali mbali kama haya matukio ya ujambazi, matukio ya kuchomwa moto kwa vituo vya polisi, matukio ya polisi kuvamiwa vituoni nk nk.
Polisi tendeni wema na haki kwa raia wenu ili chuki wanayoionyesha kwenu iishe sasa.
 
Ni matusi makubwa sana kitendo cha majambazi kuvamia kituo cha polisi. Kuna haja ya kuwawezesha zaidi polisi wetu kimafunzo (mbinu) na zana ili kukabiliana na mabadiliko ya nyakati.
 
Aanzie waziri wa mambo ya ndani anatakiwa aache kazi mara moja yeye mwenyewe bila kuambiwa. Jamaa hawawezi kuwa na nguvu kuliko police. Pia kila siku askari wanauwawa na hakuna hata kushtuka. Wajinga mno uongozi wote. Pu..........wamalizie wenyewe.

..mba.....

..fu. Huwezi ukaacha walinzi wavamiwe na ni kila siku.sasa raia je. Kikwete haraka jamaa leo waondoke.
 
Tatizo haliko polisi tatizo liko kwenye serekali yenyewe kwa kushindwa kuwekeza kwenye ulinzi kama nchi zingine ambazo huwa wanatumia gharama kubwa kwenye ulinzi.

Hata hizo camera unazozisema wanaotakiwa kununua na kuzifunga ni serekali na siyo polisi,utashangaa hata ulinzi huu kidogo unaofanywa na polisi asilimia kubwa utakuta wanagharamia wao wenyewe kwa kutumia fedha zao mifukoni.

Ndio maana utakuta askari wengi wanahangaika kuwatafuta wadau wa kuwawezesha ili kazi ziweze kufanyika bila kufanya hivyo kuna hatari ya kutokufanyika kazi za ulinzi kabisa.

Serekali kuwa mbali na polisi ndiyo chanzo cha wananchi kudaiwa hela za mafuta ya kuendeshea magari ya polisi wanapokwenda kutoa malalamiko vituoni,wanalazimika kutoa fedha za kununulia stationary,fedha za kusafirishia watuhumiwa n.k kwa hali kama hii kutakuwa na ulinzi wa maana hapo?.
Mkuu masuala ya usalama wa nchi na wa raia si ya kuchezea hata kidogo.
Wananchi tunaumia tukiona vijana wetu wakicharazwa na kuuwawa hovyo utafikiri jeshi la polisi ni boy scouts.

Tukubaliane kuwa katika muda huu tulionao jeshi letu la polisi haliko katika ufanisi wala weledi wa kutekeleza majukumu yao.

Na ndio maana nasema lifumuliwe na kuundwa upya kama Nyerere alivyounda upya JWTZ miaka ya '60.
 
Mwalimu aliwahi kustaafisha kwa manufaa ya umma, safu nzima ya maofisa wa polisi kwa kuhisiwa tu kuwa ni wala rushwa.
Haya tunayoyona ni ule uzembe wetu wa kuyachekea tu malalamko ya wananchi.

Makosa mengi ni polisi kuwa wala rushwa na wanashirikiana na wahaliu, hilo liko wazi.

Pale Wazo ofisa mmoja ninaye mfahamu alidiriki kummbambika silaha mwananchi mmoja, lakini siri ilipobainika badala ya kuchukuliwa hatau akahamishiwa Kiteto.
 
Hii ni agenda ya UKAWA, walishasema watakapoingia madarakani watatengeneza jeshi safi sana la polisi litakalokuwa kwenye standards za mataifa yaliyoendelea. Ccm wakifanya hili, ni kudandia hoja na mwisho wake utakuwa kuboronga kama walivyoboronga walipotaka kudandia sera ya elimu, na zoezi la katiba mpya ambazo zote zilikuwa agenda za CHADEMA.

Ccm zero kabisa!.
 
Pole Jidula! Police as a law enforcement agency hapa Tanzania ilikufaga tangu 1995 nchi ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi, watawala wakaingia kwenye panic na defensive mode; wakaaanza polepole kuligeuza jeshi la nchi yetu kuwa Jumuia ya CCM kama vijana UVCCM, wanawake UWT na WAZAZI; ikazaliwa POLICCM; General police code,kea maana ya kanuni zinazoongoza kazi za jeshi la police ikawa inatokana na ILANI ya Uchaguzi ya CCM! upo halo bro?!, hiyo ndio summary ya safari ya anguko la jeshi letu la Polisi as a Law enforcement agency in Tanzania.

Mkuu umenena vema, jeshi hili na mengine yote hayafanya kazi kwa weledi kamwe serikali mbovu hizi za CCM zikiendelea kubaki madarakani!! IGP, RPCs n.k ni eti ni "marafiki na mashoga" wa damu na wataala!!! Hamna majeshi hapoo...kuna utoto tu!
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Back
Top Bottom