PISTO LERO
JF-Expert Member
- Mar 8, 2011
- 2,819
- 1,455
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime Rorya, limemtendea unyama askari wake G. 2751, PC. Japhet Samwel, aliyeumia mkono akiwa kazini mgodini Nyamongo kwa kumnyima fedha za matibabu na hivyo kumsababishia ulemavu.
Samwel ambaye mkono wake hauwezi kufanya kazi kwa sasa na hivyo kushindwa kuisaidia familia yake, alikuwa ni miongoni mwa askari 31 waliopelekwa mgodini Nyamongo wakitokea mjini Tarime kuanzia Septemba 30 hadi Desemba 25 mwaka jana.
Tanzania Daima inayo nakala ya barua UPEL.TRR ® Polisi (W) zote ® vikosi vyote TRR/A.24/5/Nyamongo/232, iliyosainiwa na SSP Sebastian Zacharia, ikiwaweka tayari askari hao kwa safari hiyo.
Kwa mujibu wa nyaraka, viongozi wa kikosi hicho cha askari 31 walikuwa ni SGT Tabu, WP Vailet, PC Mauki, G9455 PC Hosea na D.2766 PC Andrew waliokuwa wakitumia gari ya polisi PT.1685.
Akizungumza na gazeti hili, Samwel alisema kuwa wakiwa kazini walishambuliwa kwa mawe na watu wasiojulikana na kuwasababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwilli.
Alisema kutokana na tukio hilo walifungua kesi M/NY/3032/10/2012 Oktoba 23, 2012, kuhusu shambulio hilo ambalo lilimjeruhi mkono wa kulia.
PC Samwel alisema kuwa alipewa barua na uongozi wa mgodi ili aweze kwenda hospitali ya Bugando.
Kwa mujibu wa Dk. Gerald Lenjima wa mgodi wa dhahabu wa Barrick uliopo Nyamongo, askari huyo alikuwa ameumia sana kiganja cha mkono wa kulia na hivyo angehitaji uangalizi wa karibu wa madaktari bingwa.
Lakini mnadhimu wa jeshi hilo mkoani Mara alikataa ushauri wa daktari na kuamrisha apelekwe hospitali ya Shirati iliyopo mkoani humo.
Alisema kuwa baada ya kubaini kuwa mkono wake unaharibika, alienda kumwona Kamanda wa Polisi, Justus Kamugisha kuomba fedha za matibabu na nauli ili aweze kwenda Bugando kama alivyoandikiwa na daktari.
Daktari bingwa wa Bugando alielekeza kuwa PC Samwel ahudhurie matibabu ya mkono huo kwa wiki nane mfululizo kwa kuwa mifupa ilikuwa imevunjika.
Lakini Januari 21, 2012 aliomba ruhusa ili aweze kwenda Bugando kwa wiki nane na kujibiwa kuwa; ‘Umeamriwa kuondoka hapa kesho kwenda Bugando kwa ajili ya matibabu na umepewa siku tatu urudi hapa mara umalizapo matibabu'.
"Nilitekeleza amri halali za jeshi, lakini mkono wangu uliendelea kuharibika kwa kushindwa kupata matibabu husika kwa kipindi kinachofaa na muda mrefu nimejitibu kwa fedha yangu," anasema.
Katika hatua ya kushangaza, chanzo chetu cha habari kinasema kuwa askari waliokuwa katika operesheni hiyo walikuwa wanalipwa na mgodi huo sh 25,000 kila mtu kwa siku, lakini Samwel baada ya kuumia aliacha kulipwa.
Samwel alisema kuwa akiwa katika hali hiyo ngumu, mkono wake ulibadilika rangi na hivyo akalazimika kufika tena ofisini kwa kamanda wa polisi kuomba ruhusa, fedha za nauli na matibabu aweze kurudi hospitali, lakini aliambulia matusi ya nguoni.
Kwamba alitishiwa kuwekwa mahabusu ya polisi kama mtuhumiwa kwa kumsumbua kamanda wa polisi, huku kamanda huyo akisema; "Nimekwambia jeshi halina fedha za kukutibu, unataka niuze gari ya kamanda ili nikupe nauli na fedha za kutibiwa?"
Baadaye alipewa ‘movement order' ya kuruhusiwa kwenda hospitali, na kwamba akiwa huko baada ya siku tatu, mtoto wa kamanda wa polisi aliuguliwa na mwanaye na kumpeleka na gari hiyo ya ofisi hadi hospitalini Bugando.
"Nilipopeleka maombi ya kulipwa fedha nilizotumia kujitibu nilikataliwa na mnadhimu wakidai hawana fedha," alisema.
Samwel aliongeza kuwa alipokwenda kwa kamanda alikamatwa na kuwekwa mahabusu na kupigwa marufuku ya kumwona bosi wake huyo na kuelezwa kuwa akirudia mkataba wake utazuiwa ili afukuzwe kazi