Jeshi la Polisi nchini, limejiweka njia panda, kufuatia taarifa yake kwa vyombo vya habari kukanusha habari iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania toleo namba 7235 la Alhamisi 21.02.2013, yenye kichwa cha habri WATUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRE WAKAMATWA KENYA. Kwa mujibu wa taarifa hiyo ni kuwa habari hiyo ni ya Uongo.
Maswali ya Msingi. [Habari zote zinahusu habari isiyo ya kweli dhidi ya polisi]
Maswali ya Msingi. [Habari zote zinahusu habari isiyo ya kweli dhidi ya polisi]
- Je Mwandishi wa habari hiyo wa Mtanzania atatafutwa na kupekuliwa chumba kama yule wa Tanzania Daima aliyeandika habari na baadaye kuomba radhi?
- Je Mhariri wa Mtanzania na Mwandishi wake watahojiwa kwa masaa zaidi ya sita, na kutolewa kwa dhamana Kama walivyohojiwa Mhariri na Mwandishi wa Tanzania Daima?
- Je Mhariri Mtendaji wa Mtanzania, na Mmiliki wa Gazeti hilo, na Mchapishaji watatafutwa kama wanavyotafutwa Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Mmiliki wa Gazeti na Mchapishaji ili wasaidie Polisi?
- Je Mtanzania litatishiwa kufungwa na Rais kama si huyu basi ni ajaye?
- Je Taaluma ya Mmiliki wa Gazeti la Mtanzania (Mfanyabiashara) itahojiwa kwanini anamiliki gazeti, kama walivyohoji Mmiliki wa Tanzania Daima kuwa Daktari lakini anamiliki gazeti?.