Jeshi la Polisi laahidi kutoa dau la zaid mil 10 kwa mhusika wa bomu Arusha.

QALLI MIZOH

JF-Expert Member
Mar 19, 2014
2,075
693
Hivi hili jeshi la polisi limeona njia haswa na pekee kumpata mtuhumiwa hadi litoe kitita kwa 'snitch' yeyote atakaetoa info kuhusu majanga ya uhalifu yanapotokea? hizo wanazoziita intelejensia hazifanyi kazi? Kamanda Mangu wapi baba? mi naona hii ya kuahidi kutoa dau kunalilemaza jeshi letu kufanya kazi vizuri.
nawasilisha.:eek:hwell:

------------------------------------------------------------

Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza zawadi ya Tsh.Milion 10 kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa wahusika walioshiriki mlipuko wa bomu lililolipuka Arusha,Bomu hilo lililipuka mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye bar ya Arusha Night Park ambalo lilisababisha majeruhi kadhaa.

Mkurugenzi wa makosa ya jinai Tanzania Dci Isaya Mgula amesema uchunguzi wa awali uliofanywa na wataalam wa mabomu kutoka Jwtz na Jeshi la Polisi Tanzania umebaini bomu hilo limetengenezwa kienyeji mbali na hilo lililolipuka Jeshi la Polisi pia lilibaini bomu lingine lililokuwa kwenye mkoba uliokua umeeegeshwa pembeni ya kiti kwenye bar jirani ya Washington.
 
huu mpango upo kwenye bajeti ya wizara? Wasije wakatoa hizo pesa halafu waanze kuelekeza nguvu kwa kucheza vibati barabarani najua linafahamika hili.
 
Jeshi la polisi lisituletee usanii, mbona limeshindwa kuufanyia kazi ushahidi wa raia wema walioutoa kwenye bomu lililopuka Soweto, Arusha kwenye mkutano wa Chadema na lile lillolipuka kanisani huko huko Arusha?!

Jeshi la polisi litambue kuwa watanzania wa leo hawadanganyiki kirahisi kiasi hicho kama jeshi hilo linavyoweza kuamini!
 
Katika sakata hili la bomu watu hawataki kuamini kama ni tukio la UGAIDI 💣.

Yangetokea Zenji watu wote tungeitwa magaidi lakini limetokea Arusha neno gaidi halijahusishwa.

Mutakuwa waongo wa nafsi zenu mpaka lini ? Jembe lipe jina lake tu usiliite panga kwani mabomu yenyewe ni 'made in mitaani'. 🍼
 
Wameshindwa kazi,.

Afu mtu unaweza kuwaambia afu hiyo m.10
yenyewe ucpewe[mizinguo tu hao]

mfano:unaweza msaidia polic labda mtu kauwawa afu hapohapo na wewe wanakuweka ndani .
 
kalimizzle
===>Sidhani kama mtegaji wa bomu alivaaa gloves wakati analitega,kwa hiyo lazima atakuwa ameyashika kwa mikono hayo mabomu au hizo kemikali.
===>Taarifa ya Waziri wa Mambo ya Ndani aliyo itoa inasema kuwa kulitegwa mabomu mawili,moja halikulipa hivyo hilo la pili lingeweza kutoa ushahidi ambao ungewzea kusaidia kukamata hao wategaji wa mabomu.
****Kwanini nimesema mambo hayo hapo juu?
===>Kama kungekuwepo na vitu vifuatavyo mtegaji angepatikana
1.Mfumo wa kuhifadhia taarifa za Ki jenetikali (Genes)
2.Wataalamu wa Kutafuta na Kuchambua Mabaki (Forensic)
 
kuendekeza uzembe huko, jeshi la polisi linakosa intelijensia katika shughuli zake ni aibu tupu kama ingekuwa kazi ni kuhonga pesa ili kupata wahalifu basi mtu yeyote angefaa kuitwa polisi,,,,,,serikali isituchezee michezo ya kitoto ilopitwa na wakati
 
kalimizzle
===>Sidhani kama mtegaji wa bomu alivaaa gloves wakati analitega,kwa hiyo lazima atakuwa ameyashika kwa mikono hayo mabomu au hizo kemikali.
===>Taarifa ya Waziri wa Mambo ya Ndani aliyo itoa inasema kuwa kulitegwa mabomu mawili,moja halikulipa hivyo hilo la pili lingeweza kutoa ushahidi ambao ungewzea kusaidia kukamata hao wategaji wa mabomu.
****Kwanini nimesema mambo hayo hapo juu?
===>Kama kungekuwepo na vitu vifuatavyo mtegaji angepatikana
1.Mfumo wa kuhifadhia taarifa za Ki jenetikali (Genes)
2.Wataalamu wa Kutafuta na Kuchambua Mabaki (Forensic)

Haha a ndugu yangu hayo yako kwa wenzetu huko majuu. Hapa tunaishi kwa kudula za mwenyez Mungu tu. Alafu tunatambiana oh Tanzania yaongoza kwa upelelezi Afrika, nyoo nani kakwambia?
 
Polisi tunawalipa kwa kodi zetu!

Ni ajabu na inasikitisha, badala ya kufanya kazi ya kuzuia na kukamata wahalifu. Wamebuni njia mpya. Kukaa ofisini na kutangaza dau kama bingo!

Ni tanzania tu!
 
Sasa napata picha kwamba polisi wanaenda chuo cha taaluma Moshi kutalii tu.Kama kweli mafunzo yangekua yanawasaidia sidhani kama wangetangaza hilo dau.
 
Thursday, 17 April 2014

JESHI LA POLISI LIMETANGAZA ZAWADI YA TSH.MILION 10 KWA WEWE MWENYE TAARIFA ZA MHUSIKA WA BOMU ARUSHA

Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza zawadi ya Tsh.Milion 10 kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa wahusika walioshiriki mlipuko wa bomu lililolipuka Arusha,Bomu hilo lililipuka mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye bar ya Arusha Night Park ambalo lilisababisha majeruhi kadhaa.

Mkurugenzi wa makosa ya jinai Tanzania Dci Isaya Mgula amesema uchunguzi wa awali uliofanywa na wataalam wa mabomu kutoka Jwtz na Jeshi la Polisi Tanzania umebaini bomu hilo limetengenezwa kienyeji mbali na hilo lililolipuka Jeshi la Polisi pia lilibaini bomu lingine lililokuwa kwenye mkoba uliokua umeeegeshwa pembeni ya kiti kwenye bar jirani ya Washington.

Tanzania bana, watawala wooote hoi hamna kazi tena wanafanya.
Kwahiyo geshi la polisi limewaachia wananchi wajilinde wenyewe au ndiyo mwanzo wa kuliachia geshi la kujenga na kulinda taifa lichukue nchi.
JM na Lukuvi mmejipanga
 
Danganya toto hiyo mtoto alitoa ushaidi aliyempiga lisasi ni police pili police ndio walikuwa wanalinda siku hiyo then waulize raia
Poor idea interagency wanakazi gani ?
 
Back
Top Bottom