Jeshi la polisi kanda maalum lakamata silaha maeneo ya Vikindu

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945

Tuesday, January 17, 2017


Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, limekamata silaha tano na risasi 12, katika pori la vikindu, zikiwa zimetelekezwa kufuatia operesheni maalumu ya siku saba.

Operesheni hiyo ililenga kukamata magari ya wizi, majambazi, wauzaji wa dawa za kulevya, wauza gongo na makosa ya usalama barabarani.

Mbali na hilo, operesheni hiyo imefanikiwa kukusanya sh. 215,090,000,kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani kuanzia januari 13 mpaka 15, mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Simon Sirro.Amesema kuwa wamefanya operesheni hiyo katika pori la vikindu, Mkoani Pwani kufuatia ongezeko la matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Dar es salaam.

Aidha, Sirro amesema kuwa watuhumiwa 362, walikamatwa na makosa mbalimbali na kuongeza kuwa wamekamata silaha aina ya SMG moja, shortgun mbili na bastola mbili.

Hata hivyo, Sirro amesema kuwa katika operesheni hiyo imebainisha maeneo yaliyokithiri kwa matukio ya uhalifu ni Kigogo Freshi na Yombo Vituka.
 
Police Revenue Authority! Matukio ya kukamata majambazi machache sana ila kukusanya pesa daily........!!! Nasikia Police wanaziba gap ya bandari!! Shangaaa wewe! Only in Tanzania!!!
 
Police Revenue Authority! Matukio ya kukamata majambazi machache sana ila kukusanya pesa daily........!!! Nasikia Police wanaziba gap ya bandari!! Shangaaa wewe! Only in Tanzania!!!
Ha ha haa dat means tunaofanya makosa hasa yanayohusiana na traffic sio tena wakosaji bali wachangiaji wazuri wa pato la taifa...
 
Kwani Polisi wanakufuata nyumbani kuchukua faini?
Tunapojichangnya kwao lazima yakukute.
 
Natoa pongezi kwa jeshi la police maana majambaka wanatishia amani sana sasa police inarara nao mbele waache wananchi tukae kwa amani haaaa
 
Hongera sana jeshi letu la polisi, hiyo ndiyo kazi mnayotakiwa kuifanya sio kupambana na ukawa au chadema
 
Hapo najua watu hawawezi kupongeza polisi maana tulishajenga chuki dhidi yao. Ila wenye akili tunajua umuhimu wa polisi, hongera sana polisi kwa kazi nzuri
 
Tunawaombea Muyakamate yooote, Tuishi kwa Amani, wakifika hako jela walime tupate chakula kwa wingi na sio wakaae tu kula kulala, kutia serikali hasara ya chakula, walimishwe hasa mana ardhi ni kubwa sana Tanzania, kiasi kwamba wakitoka huko jela wakija uraiani wanakuwa wakulima au wanapenda kulima.
 
Back
Top Bottom