The Senetor
Member
- Aug 23, 2014
- 41
- 23
Wakuu ni ajabu sana mpaka sasa jeshi la polisi halijachukua hatua kwa watu waliofanya fujo wakiongonzwa na Paul Makonda.Nina uhakika tukio lile lingefanywa na vijana wa CHADEMA/CUF/NCCR basi ingekuwa tofauti.Siku zote kwenye mikutano ya wapinzani jeshi la polisi huizuia wakidai kuna taarifa za kiinteligensia hivi ni kweli jana hawakujua kuhusu mipango ya akina Makonda?Basi hakuna usalama wa Taifa katika nchi hii, kama watu wanaweza kupanga tukio lile na wasijue sasa nini kazi ya polisi na usalama wa Taifa?.Ndugu zangu nguvu ya CCM ni jeshi la polisi ambao tunaishi nao na tunawadai kodi baadhi yao hivyo njia rahisi ya kuimaliza CCM ni kutowapa polisi ushirikiano wowote kwenye jamii yetu.Lakini huko hatupendi kwenda polisi timizeni wajibu wenu wa kuwalinda wananchi mbona JWTZ na wanajeshi wengine wanaheshimika kwanini na nyie msibadilike.?