Jeshi la Polisi au Usalama wa raia?

SUPERXAVERY

Member
Sep 5, 2012
80
9
Nimepata mshawasha wa kufuatilia hii habari ya hawa polisi wetu kuwa ni wanajeshi ama la.
Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na gumzo kubwa hasa kutoka kwa wachangiaji mbalimbali kwenye mtandao juu ya usemi wa viongozi wengi kuwa Polisi ni "Jeshi la Polisi".

Nimetaka kufahamu iwapo jina hili la "Jeshi la Polisi" limekuwa likitamkwa kwa bahati mbaya tu au zipo sheria zinazowatambua hivyo hawa polisi.

Katika pitapita yangu nilianzia kwenye katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005.

Ibara ya 147 Ibara ndogo ya (2) na (4) nimekuta maneno yafuatayo kwa kiingereza:

147.(2) The Government of the United Republic may, in accordance with law,
raise and maintain in Tanzania armed forces of various types for the purposes of
the defence and security of the territory and the people of Tanzania.

Tafsiri yangu:- Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaweza kwa mujibu wa sheria kuunda na kuendesha Majeshi yatumiayo silaha ya aina mbalimbali kwa madhumuni ya ulinzi wa ardhi yake na ulinzi wa watu wake.

(4) For the purposes of this Article, the expression "member of the
defence and security forces
" means a member in the service of the Defence
Forces
, the Police Force, the Prisons Service or the National Service, whether on
temporary or permanent terms.

Kwa hiyo basi JWTZ, Polisi na JKT yote ni majeshi ya aina mbalimbali yaliyoundwa kwa mujibu wa ibara hizi za katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sasa je wanajeshi wetu wa jwtz ambao huwadharau na kuwananga polisi kuwa si JESHI, bali kwao jwtz jeshi ni lile la anga, nchi kavu na majini tu. Tafsiri hii wanaipata wapi???? Au wana katiba yao.
Nifahamuvyo mimi majeshi yote yanatakiwa kutunza nidhamu ya hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuheshimu vikosi vingine vya ulinzi na usalama vilivyoundwa kisheria.

Sheria Namba 322 ndiyo iliyounda Jeshi la Polisi, hii ni kwa msaada wa anayetaka kufahamu zaidi kuhusu polisi na kazi zao.

Hili nimeona ni muhimu kulieleza humu kwa kuwa nafahamu wamo WAJEDA wanasoma, kuwasaidia tu kuheshimu wenzao wa vikosi vingine vya kijeshi. Tunaheshimu kazi zao kwani ndio zimeendelea kutunza amani yetu ya Tanzania, ingawa siku za hivi karibuni imekuwa mashakani hasa kutokana na malumbano ya viongozi kadhaa wa kisiasa na Serikali iliyo madarakani kwasasa.
 
Back
Top Bottom