Jeshi la Marekani limefanikiwa kufanya jaribio la kudungua kombora la masafa marefu

justin mwanshinga

Senior Member
May 22, 2014
179
621
Jeshi la Marekani limefanikiwa kulidungua na kuliharibu kabisa kombora la masafa marefu (ICBM) kwa kutumia mfumo wake mpya wa ulinzi dhidi ya makombora ya masafa marefu, kombora hilo lililorushwa kutoka Kwajalein Atoll huko Pasifiki liliharibiwa na roketi (interceptor) iliyorushwa kutoka kambi ya jeshi la anga ya Vandenberg jimbo la California jioni ya jana kwa saa za California (GMT-8).

Haya ni mafanikio makubwa dhidi ya tishio la makombora kutoka Korea Kaskazini, hii ni dhahiri kuwa sasa Marekani haiwezi guswa na kombora la aina yoyote endapo litarushwa kuelekea nchi hiyo . Mfumo huu wa kiulinzi dhidi ya makombora ya masafa marefu ulianza kitengenezwa mwaka 2002 na umegharimu kiasi cha Dollar bil 40 sawa ni Trillion 90 za Kitanzania .

Hongereni Pentagon.

Source :
Josephat Nyambeya

mwanshinga Jr
 
Sina uhakika kama wanaweza kulitungua kombora jipya alilojaribu KIM lenye atitude ya 2000. Yaani lisiloonekana kirahisi na rada kwa kuwa linapita juu sana kuliko ICBM zilizopata kutengenezwa.
 
Hii habari ingeandikwa kuwa jeshi la marekani imefanikiwa kufanya jaribio la kudungua kombora la masafa marefu!


Haiihitaji tuition kujua kuwa kurusha kombora mwenyewe na kulidungua mwenyewe hayo ni majaribio ya udunguaji wa hilo kombora
 
Nadhani wamarekani wanafanya "masterbertion" ya kivita..........
Akili za US hazitofautiani na akiliccm saa zingine!! Kutaka kuonesha wananchi wake kuwa mambo yako sawa kodi zinaishia kwenye upuuzi!!
Wapo waliopiga kelele humu kwenye jukwaa "sasa mapanki anaenda kupigwa!" baada ya kusikia manowari kubwa zinaenda rasi ya Korea... Mwisho wa siku ziliondoka kimyakimya huku dogo akiharibu scud za mwaka 1965 kwa kuzitupa baharini!!!
Nadhani katika kulipiza ndio US wanajitoa kwenye mkataba wa mazingira na wao watupe Atomic zao za 1945 baharini!!!
 
Na huku ndo kuogopa kivuli chako mwenyewe, watu waliwaita north wapuuzi mbona marekani hafanyi majaribio, kwanza teknolojia ya kisovieti haya sasa hiyo hiyo ya kisovieti mtu t*ko linamuwasha huko ndo mjue north korea kwa kiduku sio kama mnavyoelezwa..
 
Back
Top Bottom