Jeshi la Marekani lathibitisha uwepo wa viumbe vya ajabu angani

Kabla ya kuja kwa wakoloni, babu zetu waliwasiliana na mizimu na waliweza kuwafundisha tekinelojia. Hata uwezo wa kutengeneza upinde na mshale pamoja na mikuki.

Si ajabu na sisi tungekua tunakwenda mwezini sasa.
Kwani mpaka sasa huingii mwezini? Basi kuna shida Mahari,kamuone Physician.
 
Awali lilikuwa ni jambo la kubezwa na kudharauliwa. Wale walioripoti kuona vitu vya ajabu angani hawakuaminika, lakini sana jeshi la Marekani limethibitisha uwepo wa viumbe hivyo. Je, vina madhara kwa ulimwengu na binadamu? Fahamu zaidi kwa kutazama video hii: Jeshi la Marekani lathibitisha uwepo wa viumbe vya ajabu angani - BBC News Swahili

Chanzo: BBC Swahili (24 Juni 2021, 05:41 EAT)
Hiki kitu mbona kinajulikana siku nyingi? Uthibitisho mwingine huu hapa wa Japan Cargo Flight 1628 ilikuwa inalelekea Anchorage













 
Lazima wafanye hivi kwani mchina anaogopeka Sana Kwa sasa kwani ni majuzi tu Taifa la watu Jamhuri ya China wamefanikiwa kupeleka wanasayansi wao watatu katika moja ya station yao angani
Maendeleo ya wachina na uboreshaji wa sayansi ya anga kwa hawa macho madogo ni pigo na hatari Sana Kwa world order
Binafsi naamini hu ugomvi wa China na mataifa ya magahribi ni kiini macho tu, wote hao ni member wa hiyo ulioisema, yaani NEW world order. Kwa nje wanaonekana kama wagomvi but usiku wanakaa na kupanga mikakati vizuri tu, case study, CORONA. Imeanzia wapi na nani anafanya management yake????
 
Hivi kwanini hivi viumbe wanaviona au vinaonekana kwao tuu?
Sababu kubwa wao wana vifaa vyenye uwezo wa kunasa hivyo vitu na kutoa taarifa mitandaoni na watu wao kuwa na curiosity ya kujua kinachoendelea.

huku unaweza ukaona kitu cha ajabu na usiwe na hata simu ya kurekodi sababu inaweza kutokea kijijini.
Au unaweza kuona kitu cha ajabu na usijue kama cha ajabu au usitoe taarifa na ukitoa taarifa mara nyingi utaonekana umechanganyikiwa au ni ushirikina.
Hivyo ni ngumu kusikia haya mambo huku africa.

Mimi niliwahi shuhudia usiku wa saa nane kitu kikubwa chenye mwanga mkali kikimulika dirishani kwangu nilidhani ni mwezi sababu kilikuwa juu sana lakini niligundua sio mwezi baada ya kukiona kikisogea huku na huko kisha kinapotea na kurudi tena then kikaondoka kabisa.

Nilishindwa kurekodi sababu nilikuwa natetemeka kwa uoga na kila niliyemwambia alidhani nimerogwa au nimepanda kichaa hivyo nikakaa kimya tu.

Huo ni moja ya mfano hai unaoonyesha haya mambo yapo kila sehemu duniani ila bila media kuspread hizo taarifa hayatofika popote na hakuna atakayejua yanayotokea.
Bila shaka bila media kubwa au taarifa kusambaa hakuna mtu angejua kuhusu hayo yanayotokea huko kwao na considering media za kiafrika zimewekeza kwenye siasa na mambo ya entertainment za kijinga na ujinga mwingine hivyo bila shaka hakuna atakayekusikiliza ukipeleka taarifa kama hiyo.

na kingine ni asilimia kubwa ya africans hawana interest wala curiosity na mambo kama hayo mara nyingi interest zao zipo kwenye wasanii, ngono na burudani au kiufupi mambo mengine yote yasiyo tumia nguvu za kufikiria na akili, hivyo hata hizo taarifa hazitofika popote sababu hakuna mwenye interest.

Jibu fupi ni Media
 
Back
Top Bottom