Jeshi la Marekani lashambulia Al Shabaab

Jeshi la Marekani lashambulia Al Shabaab

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,561
Reaction score
53,572

140902072622_al_shabaab_512x288_bbc_nocredit.jpg

Wapiganaji wa Al Shabaab



Wizara ya ulinzi ya Marekani inasema kuwa jeshi la nchi hiyo limefanya mashambulizi dhidi ya kundi la wanamgambo wa kiislamu la , Al Shabaab nchini Somalia.

Msemaji wa Pentagon Rear Admiral John Kirby amesema kuwa wanatathmini matokeo ya operesheni hiyo kabla ya kutoa taarifa zaidi .

Al Shabaab kwa sasa wanaendesha kampeni dhidi ya serikali ya Somalia na vikosi vya kimataifa vinavyoiunga mkono.


140902084357_au_soldiers_512x288_bbc_nocredit.jpg

Wanajeshi wa Muungano wa Afrika



Afisa mkuu wa Marekani amesema kuwa maafisa wakuu wa Al Shabaab ndio waliolengwa kwenye mashambulizi hayo.

Kundi hilo lenya uhusiano na al-Qaeda lilitimuliwa kutoka Mogadishu mwaka 2011 mji ambao kwa sasa unadhibitiwa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika.

Hata hivyo kundi hilo bado linadhibiti maeneo ya Kusini ya nchi hiyo.


140902084512_mabaki_ya_gari_512x288_bbc_nocredit.jpg

Mkazi mmoja alinukuliwa akisema alishuhudia moshi mkubwa ukifuka


Tungali tunadadisi hali na matokeo ya shambulizi na baadaye tutaweza kutoa maelezo,'' alisema msemaji wa mkuu wa Pentagon

Wakazi wa kijiji cha Hawai umbali wa kilomita 240 Kusini mwa Mogadishu, wanasema kuwa walisikia milipuko na kisha kuona moshi mkubwa ukifuka.

Mkazi mmoja aliambia BBC kwamba aliona mabaki ya gari moja liliokuwa limelipuliwa ingawa hakuona miili yoyo
te.


Source:
BBC

Jeshi la Marekani lashambulia Al Shabaab - BBC Swahili - Habari


 
Amani ya duniani itatimizwa kwa mabomu vifaru na silaha kali mnoo
SUBIRINI NEW WORLD ORDER IJE NA MASIH DAJJAL tuone kila mtu atakwenda wapi?
 
Back
Top Bottom