Echolima1
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 6,929
- 6,030
Jeshi la Marekani limepeleka ndege zake za kivita za kisasa zaidi aina ya F-35A Mashariki ya Kati, huku likiendelea kushambulia waasi wa Houthi nchini Yemen — kundi linaloungwa mkono na Iran ambalo limekuwa likishambulia meli za kibiashara katika Bahari Nyekundu.
F-35A ni ndege ya kisasa ya kivita yenye uwezo wa kujificha kwenye rada na kutumia silaha mbalimbali za kisasa. Ndege hizi zilishatumika awali wakati wa mzozo wa Gaza, zikiwa sehemu ya juhudi za Marekani kuzuia vita vya kikanda.
Sasa, chini ya kampeni mpya ya Rais Trump ya mashambulizi makali dhidi ya Houthi, Marekani imeongeza vifaa vya kijeshi katika eneo hilo.
Jeshi pia limeongeza muda wa kikosi cha meli ya kivita ya USS Harry S. Truman kubaki katika Bahari Nyekundu, na kutangaza kuwa meli ya kivita ya USS Carl Vinson itajiunga hivi karibuni.
Aidha, ndege za kivita aina ya A-10 Warthog na B-2 Stealth Bomber zimepelekwa katika kituo cha kijeshi cha Diego Garcia, ambapo sasa karibu nusu ya ndege zote za B-2 zinazoweza kufanya oparesheni ziko huko.