Jeshi kulinda amani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi kulinda amani

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mundali, Oct 9, 2010.

 1. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Katika hali isiyo ya kawaida, Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania limeamua kuingilia kati mastakabali wa amani ya nchi kwa madai kwamba amani imetishiwa kuvunjika na damu kumwagika.
  Ni jambo la kushangaza sana kuona jeshi lenye dhamana ya kutumikia wananchi kulinda mipaka ya nchi yao, linakuwa mstari wa mbele kujihusisha na siasa za ndani ya nchi ilhali limeegemea upande mmoja.
  Sio siri, ni kwamba jeshi limekuwa upande wa chama tawala na kuhusika kuwalinda bila kificho viongozi wa chama hicho.
  Kwa matamshi ya kulazimisha raia kuyakubali matokeo kwa vyovyote itakavyo kuwa ni urasimishaji wa matokeo ya uchaguzi kabla ya uchaguzi, na kuhalalisha matokeo haramu.
  Kwa upande mwingine kitisho cha majeshi kilichobarikiwa na serikali kina nia ya dhati kabisa ya kuwakatisha tamaa watanzania wapenda mabadiliko, kwani kwa mujibu wa sheria tume ya uchaguzi ikitangaza matokeo hakuna wa kuyabadili.
  Maswali ya kujiuliza ni je, jeshi hili linafanya kazi kwa niaba ya nani?
  Je, wananchi wakipinga matokeo ya uchaguzi jeshi litachukua uamuzi gani?
  Iwapo jeshi litaingia mitaani litakuwa linapambana na nani?
  Je, zana za kivita watakazotumia wanajeshi zitakuwa sawa na wanaopambana nao?
  Kama uchaguzi utakuwa huru na haki, kuna haja ya jeshi kuingilia?
  Hayo yatakuwa mapinduzi ya kijeshi ama kitu gani?
  Jeshi litapokea amri kutoka kwa amiri jeshi yupi, aliyeshinda kwa kura ama atakayetangazwa na tume ya uchaguzi?
  MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
Loading...