Jeshi (JWTZ) na Ujambazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi (JWTZ) na Ujambazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Aug 2, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limemkana askari wake, koplo Julius Abraham Kwayu, ambaye alidaiwa kuhusika katika tukio la ujambazi lililotokea Julai 24 mwaka huu, Manzese jijini Dar es Salaam na kueleza kwamba aliomba likizo na hakurejea kwa muda mrefu.
  Taarifa ya JWTZ iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano makao makuu ya Jeshi hilo kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana ilisema Koplo Kwayu, alikuwa mtoro wa jeshi kwa kipindi kirefu na kwamba jeshi lilikuwa likimtafuta.
  ... habari nimeikata....
  Hata hivyo, taarifa hiyo ilifafanua kuwa ili kukabiliana na tabia mbaya kwa baadhi ya watumishi, jeshi limebadili utaratibu wa kuajiri askari wapya na kwamba kuanzia sasa vijana wote wanaoomba kujiunga na JWTZ watalazimika kupata mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) au Jeshi la kujenga Uchumi (JKU) ili wachunguzwe mienendo yao. mwisho wa nukuu.
  --------------------------------------

  Nionavyo

  Sasa kutokana na hilo suala hapo inamaanisha kuna uajiri mmbovu katika kuwasajili vijana katika kulitumikia jeshi na vilevile kunaonyesha hakuna kumbukumbu za askari hao hapo katika Jeshi kwa maana jeshi halina ufuatiliaji ,kwa maana jeshi halina full address ya mtumishi wake ukizingatia kuwa hii ni sehemu nyeti ya Taifa ,hivyo badala ya kuona chombo hiki watu wake wanamaliza wakiwa na utiifu na heshima na pia kuheshimika kwenye jamii ,kimekuwa ni chombo kinachotoa wahalifu ,imekuwa ni chuo cha kusomeshea wahalifu ambao wakimaliza hapo huwa na uzoefu wa hali ya juu na kama ni shahada basi shahada yao ni hatari kwa Taifa hili na watu wake.

  Msemaji wa Jeshi anadai kuwa Mjeshi atalazimika kupitia JKT au JKU sijui JKU kuna uhusiano gani na JWTZ,hayo ni yake tumwachie mwenyeewe,sasa ni kitu gani ambacho kitamfanya alie na nia ya kusomea ujambazi katika JWTZ asitimize yote hayo ,je ni kweli kuwa vijana wanakuwa na lengo maalum au vijana hao huharibika wakishaingia kwenye JWTZ ,hapo napo naona ndipo pa kupachunguza ,huenda huko ndani ya JWTZ hakuna mafunzo ya dhamana juu ya mtu kuwa ni mwanajeshi.

  Aidha kuna mambo kibao ambayo yamejitokeza katika mitaa inayokaribiana na kambi za Jeshi ,kama wanajeshi kutoka na kuvamia ,kupiga kila alie mbele yao aliehusika na asie husika ,sijui wanatumia sheria gani katika kujihukumia huko au ndio nidhamu za kijeshi haswa inapokuja kesi za raia na wanajeshi .landa tuamini kuwa katika JWTZ hakuna nidhamu ? Jambo ambalo naamini kabisa sio kweli.

  Nitawapa kisa kimoja ,wakati nikiwa mwanajeshi mpya katika kambi fulani pale Nachingwea ,kwanza kuingia pale tu tulikuwa vijana kama 67 hivi,na kati yao mimi peke yangu ndie niliekuwa mweusi kama kiza maana wengine huwa weusi lakini wanang'ara kidogo mimi hamna ni kiza tu ,nikicheka labda ndio utaweza kuona meno yalivyo meupe ni hayo tu sina kingine labda siku hizi nimeongeza mamnvi kumkaribia Lowasa ,sasa hapo ule mkuu akaniita ,wewe Jaluo kuja hapa ,mimi nikasita japo nilikwisha elewa lakini nikaona kama leo ndio nimepata kazi na leo ndio itakuwa mwisho basi naiwe hivyo ,sikuinua hatua hata moja ,akaita mpaka akaona sasa ipo kazi na yeye amepata kazi,ili kuonyesha kama yeye ndio yeye na ujeshi umemkolea na kutaka kutonyesha sisi wageni 'New comers' akanisogelea na kunikamata ukosi kwenye shingo kwa mbele akilikunja shati langu na kutaka kama kuninyanyua juu kwa kweli nilikuwa nimeshiba vyakula vya nyumbani ,basi sikujua ni wakati gani nilimuweka ngwara akaanguka chini na hapo ndio ikawa mwanzo wa kupata mateso alituwachia kufika usiku wakaingia Mp na yeye yupo akawanyoonshea kidole kuwaaashiria kuwa jamaa mwenyewe ndio yule pale basi wakanichukua na kuanza kunitesa wakanipa adhabu zoteila adhabu moja ambayo nikuweka kidole chini na kuzunguuka ndio iliyonimaliza ,kule kwenye bweni jamaa walimwendea mkubwa kabisa wa kambi ambae walimueleza kisa chote ,aloo mkubwa huyo aliona anataka kumwagiwa unga wake akatoka huko kama mbogo na kuja kule nilikokuwa nikiadhibiwa kufika tu alisimamisha kila kitu na mambo yote kumgeukia yule komandoo ambae alipewa adhabu kwa muda wa siku kumi uchimba mahandaki ya watu wawili wawili kwa kila siku alitakiwa kuchimba kumi kwa maana baada ya siku kumi yawe yamefikia mia.Nilichosikia pale ni kuwa adhabu aliyonipa hairuhusiwi jeshini na haimo katika taratibu za mafunzo ya kijeshi na hapo sisi tumekuja au ni wageni na tulihitajiwa kukaribishwa kwa ukarimu na sio vitisho vya kutufanya tuone jeshi ni sehemu ya mateso.

  Kwa habari hiyo ndio nikasema kuwa JWTZ inawezekana kabisa ndipo tabia za mtu zinapoanza kuharibiwa na kufundishika kinyume na matarajio,na purukushani zote zinazosababishwa na wajeshi wa JWTZ ni kuonyesha kuwa jeshi hilo limepoteza nidhamu kila mmoja ni komando na kila mmoja anaweza kufanya lolote lile na hakuna wakumdhibiti ,jambo ambalo ni kosa na ni hatari sana ,nidhamu ndani ya Jeshi ni kitu cha lazima kabisa na hakina mbadala.


  Kusema waanzie JKT au JKU ni kukwepa lawama ambazo hivi sasa linaziandama jeshi hilo la JWTZ ,hivi kwa nini isiwepo sheria ya kumzuia na kumbana mjeshi kumpiga raia ? Kwa nini sheria hii isiwepo na kama ipo mbona hatusikii kutumika ,nahisi WaJeshi wawe ndio watu wa mwanzo kufuata sheria ,na iwe ni kosa kubwa kwa mwanajeshi kumpiga raia akiwa na vazi la kwanza Jeshi hilo pili akiwa bado analitumikia jeshi hilo bila ya sababu za msingi ,maana kuvamia stand na kupiga raia wote hilo haliingii akilini kuwa kuna jambo amefanyiwa mwenzao au wenzao ,hapo kuna watu hawakuhusika na ni raia wema kabisa. utasikia wamevamia baa kwa kuwa tu mmoja wao alikuwepo hapo na kukatokea ugonvi wa kugombea mwanamke ,jamaa akarudi kambini na kukusanya wenzake na kurudi tena baa na kuanza kutoa kisago cha kumpiga mbwa koko.


  Sheria na dhamna ya chombo hiki haifuatwi ,watu wanaachiwa bila ya kufuatiliwa nyendo zao au kupewa adhabu ya kuvunja sheria wakiwa ndani ya jeshi, natumai hata bila ya kupitia JKU au JKT ,ndani ya JWTZ kunaweza kuanzishwa mikakati ya kuweka sheria nzito pale tu mtu anapoandikishwa basi iwepo na fomu maalum ya kujaza ambayo itamfunga yeye na uvunjaji wowote wa sheria akiwepo ndani ya kukitumikia chombo hicho ,vile vile udhibiti wa safari za kibinafsi akiwa karibu au mbaloi ya kituo japo kwa likizo,ni lazima ajulikane ametokea wapi na kijiji gani alipokulia alipolelewa aliposomea alipochezea hata kufika kujiunga na jeshi hilo.
   
Loading...