kilimbamula
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 1,792
- 853
Wana Yanga pamoja na wanasoka nchini walikuona au kukusikia ukitangaza kwa mbwembwe kuwa pamoja na urafiki binafsi uliokuwa nao na Niyonzima, kwa kosa hili alilolifanya huna msamaha naye na hakuna kuoneana haya.
Kama ungelisema hili kwa nafasi yako ya usemaji wa timu mimi nisingekuwa na shaka na kauli hiyo kwa sababu ni sehemu ya kazi yako kuelezea masuala mbalimbali yanayohusu Yanga.
Lakini ulienda mbali zaidi kama vile wewe ni mwajiri binafsi wa Niyonzima kwa kutoa tuhuma juu yake ambazo binafsi umedai kuwa una ushahidi na huo ni mchezo wake wa mara kwa mara.
Lakini hivi majuzi mmekuja na habari ya kitoto na kuamua kumsingizia katibu kuwa kaficha barua.
Kwa kuwa uliuelezea umma pasi na shaka kuwa hata wewe umejiridhisha, sioni eneo lolote ambalo unaweza kuwa mbali na tuhuma hizo za mchezo mchafu ambao umemgharimu Katibu wa timu Bw. Tiboroha.
Kwa heshima yako uliyojijengea siku nyingi, ni vema ukajiuzulu ili uendelee kusimamia maamuzi yako. Ukikaa kimya unamaanisha kuwa siyo mtu makini bali ni msaka tonge kwa kujikomba.
Tunasubiri kauli yako ya kushujaa.