Jerry Muro: Urais wa Kizalendo ni mgumu Tanzania

Jerry murro nakupongeza sn kw wzalendo wako na moyo saafi.nakumbuka ulivyokuwa ukipambana na rushwa mpk ukabambikizwa kesi ya AJABU.pigana.pambana.tupo pamoja
 
Muro ulishawahi kununua sukari kwa 5000? huo ndio uzarendo, kutudanganya sio.

kuficha Ndege zetu kukamatwa ndio uzarendo huo, kufukuzwa Yanga kumemchanganya hana kazi sasa hivi, harafu si wameshamjua mkuu anapenda wambea?
Huwa namdharau sana mtu aneshindwa tu kutofautisha kati ya herufi"R"na "L"...

Rudi shule jinga ww.
 
Nakumbuka Wakati Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akishirikiana na Waziri Mkuu ambae nae ni Marehemu Mzee wetu Edward Moringe Sokoine, baadhi ya wananchi walilalamika sana kutokana na Viongozi hawa kupambana na Rushwa na Ubadhirifu wa Mali ya Umma,

Naambiwa ilifikia mahali wahujumu UCHUMI walikana Mali walizonazo na wengine KUZITUPA majalalani zile zilizoweza kutupika, walijitahidi Kujenga taifa la Kizalendo, taifa lenye Umoja wa dhati Misingi ambayo tumeendelea kuitumia mpaka Leo wakati ambao Misingi hiyo imeanza kuweka NYUFA, inataka KUBOMOLEWA na Mataifa Makubwa kwa KIVULI cha kukwapua RASILIMALI zetu.

Mungu sikuzote ni mwaminifu na wa HAKI, baada ya Kilio cha Muda Mrefu Kutoka kwa Viongozi wa Dini, wanasiasa na wananchi kuhusu kukithiri kwa Vitendo vya KIFISADI, Mungu AMEJIBU maombi tena amejibu kwa MOTO, ametuletea Rais Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli anepita Katika NYAYO za Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, ametuletea Mhe Kasim Majaliwa Kasim waziri Mkuu Mzalendo anaefuata NYAYO za Marehemu Edward Moringe Sokoine, hii ni HESHIMA kubwa sana kwetu kuwa na Viongozi wa Haina hii.

Nilijaribu kufanya Udukuzi kidogo wa Taarifa zao za Benki Nilishanga kuona Kiasi KIDUCHUU cha fedha zinazotokana na Mishahara yao, nikadadisi tena kwa watu wao wa KARIBU nikaambiwa Mishahara yao ikiingia tu Benki Hutolewa kiasi kidogo kidogo kwa Ajili ya Kuchangia HARAMBEE za Ujenzi wa SHULE, ZAHANATI na wakati Mwingine kusaidia kununulia Magari ya Wagonjwa na Kiasi kinachobaki hutumia Na familia Zao.

Niliamua Kudadisi Tena Maisha ya Ndugu zao wa Karibu Ndugu Wa Kuzaliwa Tumbo moja, watoto wao, Mashemeji zao na majamaa na Marafiki zao nikakuta idadi kubwa Wanaishi Maisha ya kawaida kama sisi uku Ubungo Maziwa, watoto wao wanasoma Shule za Msingi na sekondari kama wa kwetu na Juzi juzi Niliona Mtoto Mmoja wa Mhe Rais amepata Udahili wa Masomo ya Shahada ya Uzamili katika chuo cha Tanzania, tena kiko Mkoani na Sio Mjini

NIKAENDELEA kumtukuza Mungu mana VIONGOZI hawa MATENDO yao yanaakisi Maisha yetu, hapa nimeona utofauti ambao umewafanya hata baadhi ya Wasaidizi Wao kuwarejesha watoto waliokuwa wanasoma UGHAIBUNI, tumeona uwiano wa Maisha ukianza Kurejea, waliochini taratibu wanaelekea katika Uchumi wa Kati kwa Kufanya kazi kwa BIDII kupitia Mapinduzi ya Viwanda iwe Ujenzi wa Viwanda Vikubwa mfano Kiwanda cha Kutengeneza SUKARI kule Mbigili vitakavyozalisha Ajira, na kuchangia mapato ya serikali kupitia KODI, viwanda vitakavyozalisha BIDHAA kwa ajili ya soko la Ndani hali itakayofanyika bei za bidhaa hizo kushuka mana zitakuwa Nyingi Sokoni, bidhaa zingine zitauzwa Nje ya Nchi (export) tutapata fedha za kigeni na Kuimarisha Shilingi dhidi ya Dollar.

Nimejifunza mambo mengi sana ambayo ya nazidi kuniimarisha katika SIASA, nimejifunza jambo moja kubwa, HAIJAWAI KUTOKEA TANGU ENZI YA UTAWALA WA MWALIMU NYERERE MPAKA LEO MHE MAGUFULI NIKAONA AU KUSIKIA RAIS ANAPONGEZWA.

1. Enzi ya Nyerere walimsema sana kuwa ni dikteta, kasababisha maisha Magumu lakini Alipofariki ametangazwa "Mtakatifu "na hotuba zake zinanukuliwa kila siku.
2. Mzee Mwinyi walimsema sana mara Anauza na kugawa mpaka tausi wa Ikulu wakampachika mzee wa Ruksa, japo walikudhihaki Leo WANAKUKUMBUKA wanatamani hata Ruksa Kidogo tu ya KUKWEPA KODI.
3. Mzee Mkapa wakalalamika maisha magumu sana wakamtundika jina la "UKAPA" wakasema amechukua migodi, kapewa pande la DHAHABU maneno Lukuki, Leo wanamuota na Kusema Heri ya UKAPA kuliko HAYA
4. Mzee Kikwete, huyu sihitaji hata kusema, walimdhihaki sana nadhani kuliko Rais Mwingine yoyote Tanzania, Mara ufisadi umeongezeka, mara mwanae Anauza UNGA, mara nchi haina Rais iko AUTO pilot, Mara Rais LEGELEGE, wakasema sana, ila nikashangaa Siku Mzee Kikwete amemsindikiza "MAMSAPU" kuapishwa Bungeni wale wale bila AIBU walilipuka SHANGWE na NDEREMO na kumwambia TUNAKUKUMBUKA MZEE, nilishangaa sana nikasema hivi hizi ndio SIASA za Tanzania KWELI?

Mzee Kikwete akabaki kuwacheka sana, najua alikuwa ANAWAZOMEA MOYONI mana alijua pamoja na mitusi yote ile "WALIKUMBUKA SAMBUSA NA JUICE TU " Ni sawa na wana wa Israel kukumbuka MANA za kule Misri.

Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, mama Samia Suluhu Hassan na Kaka Yangu Mhe Majaliwa Kasim Majaliwa siku mkiondoka MADARAKANI nawahakikishieni lazima hawa wanaowatukana WATAWATANGAZA nyinyi WATAKATIFU na mashujaa wa Tanzania, subirini mtaona kwa MACHO yenu, miaka nane sio MINGI, Subirini mtaona.

Urais Tanzania ni MATESO, Ngoja ninukuu alichosema Mwandishi mwenzangu Chakubanga hapa kidogo

"..... Kauli ya JPM kwamba "Urais ni mateso" inanikumbusha kauli ya Masiha wa Bwana aliposema"Ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke" Na hata pale Msalabani Calvary aliposema "Ee Baba Mbona umeniacha".

Kibinadamu Ni Kauli zinazoonesha kufikia mwisho wa uwezo wa kibinadamu,lakini kiimani ndipo Safari inapoanzia kuelekea kupita uwezo wa kawaida wa mwanadamu na kuweza kuandika historia,Kwa kiingereza "beyond human knowledge and ability,that's an exceptional case".

Masiha ni Mteule Kwa jina lingine ni Mkombozi,Neno hili linatokana na ushindi ama kuwashindia wenzako vita,ama hatari iliyokuwa inawanyemelea ama kuwakumba, Mara chache dunia inapata kuwashuhudia wakombozi katika jamii zao na katika vitabu vya dini tunapata kuona neno masiha, na kuliendana na kusulubiwa na kwa Masiha kusulubiwa msalabani kulimaanisha kuukomboa Ulimwengu, hivyo tunaipata picha ya kwamba changamoto zinapozidi na bado kila sensi inakutaka kuendelea na changamoto hizo basi wewe ni masiha Kwa maana nyingine ni Mkombozi.

Kuna story moja ya Paulo akisema "Baba mwiba katika mwili wangu" na Baba alimjibu "Neema yangu yakutosha" Ooh kumbe unapopewa mwiba katika mwili wako au Changamoto zinapokuzidia kuna neema ambayo inaweza kukutosha kukupitisha kwenye changamoto hizo na ukatoka ukiwa imara zaidi ya ulivyokuwa Mwanzo na ikawa msaada kwako kuweza kukuimarisha na kukusaidia kuishinda vita ambayo iko mbele yako,kumbe kila changamoto Kwa neema itakuimarisha na kukufanya kuwa shujaa,hatasinzia yeye akulindaye Kwa maana unatenda si Kwa kujikomboa wewe bali kulikomboa Taifa,Maana iliandikwa utakuja mteule wa kuweza kuyapitia haya ili kuweza kujenga msingi wa Taifa imara Kwa ajili ya kizazi hata vizazi vijavyo,Nikutie Moyo husiogope hata kila mtu anapocontradict the fact just believe in what you are doing,Kwa maana ndiyo njia pekee ya kulikomboa Taifa,ilitupasa kuipita njia hiyo miaka 20 iliyopita ila wengi tulichagua shortcut lakini kumbe hakuna shortcut na inatupasa kupitia kila changamoto ili tuweze kulijenga Taifa imara la Tanzania Kama Wachina walivyopitia Haya yote hata kuipata China ya Sasa ambayo ndilo Kilanja wa Dunia Kwa Sasa baada ya decade ya Marekani kuisha.

Baba wa Taifa, Mwl Nyerere aliwahi kusema "Urais si lelemama" akimaanisha "Urais ni mateso" Kwa mtu makini utakubaliana Na Hayati Mwl Nyerere na pia utakubaliana na Mh Rais Magufuli hasa inapokuja kuwa na timu imara unayoijua na kuiamini ili kuweza kukusaidia kutimiza majukumu ambayo ni ya juu na ya mwisho ya kuweza kulisaidia Taifa kusonga mbele,yakupasa kutenda Kwa kadri ya uwezo wako wote hata uwezo wa mwisho kabisa kulisaidia Taifa Kwa maono na mipango hata kuweka historia.

Kwa mtu makini hasa anayechagua kupita ile njia halisi ya kuelekea mafanikio lazima atawaza usiku na mchana na pengine kulala masaa manne hadi sita kuwaza na kuchanganua namna ya kulisaidia Taifa,kutengeneza maisha ya vizazi vitatu mbele baada ya kizazi chetu kupita,wengi wanawaza urais ni kula bata tu lakini Kwa mtu makini Urais ni kazi ambayo inakuhitaji kutenda hata uwezo wako wa mwisho,changamoto zitakuja hasa unapovunja miundo mbinu ya walaghai,walafi,wanadhirifu,wasio na uadilifu,mamwinyi na miungu watu,wauaji,wahuni,wezi,mafisadi,wanasiasa matapeli na wasio wazalendo Kwa Nchi yao,Vita itakuja zaidi wewe Kama Rais unapokuwa mwadilifu na hivyo kufanya system yote kuwa ya kiuadilifu,wengi watapenda husiendelee kuwepo

Kwa kuwa umeingilia anga zao na wizi wao,lakini Kwa kuwa imeandikwa atakuja masiha (mkombozi) ambaye sistahili hata kufunga gidamu za Viatu vyake,yeye ndiye atayepita njia ile ambayo watangulizi wake wameikwepa,Mteule huyo atapita miba ikimsonga,na pengine Mbwa mwitu kumzonga lakini atapita ili kuiongoza Tanzania kuelekea Tanzania ya maziwa na asali kuweza kuipata "The Great Tanzania" ambayo Mungu aliibariki kuwa Taifa tajiri lenye utajiri wa Mali ya asili lakini wahuni waliifanya ni Shamba la Bibi.

Kama ilivyokuwa miaka ya 1960 upepo wa Uhuru ulipovuma Afrika basi Sasa upepo wa mabadiliko ya kiuchumi unavuma tena Afrika na hasa kimbunga kikionekana Tanzania,vumbi litatimka lakini mwisho wa siku tutaipata Tanzania ya Viwanda,Tanzania ya Uchumi wa Kati ,Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika.

Mwandishi wa Makala hii ni Mwanahabari mwandamizi za Uchunguzi kwa Kipaji (talented) pia mtaalamu wa Uongozi wa Biashara na Masoko (kitaaluma) Mwenye Shahada ya Uzamili (Master Degree) MBA (2015)
Simu ya Mkononi : 0785333999
Barua pepe : jerrymuro98@gmail.com

Pia Makala hii Imetoholewa kutoka kwa Msemakweli Chakubanga.
Najiuliza kama wewe in muandishi ama kuwadi
 
When men of substance speak jerry muro is no where near. another PR stunt from wannabe mercenary.
 
Jerry Muro, kwa kujipendekeza kwako, ukipewa kuwa DC, tumekwisha, au umesahau mchezo wako wa kutembea na mapingu kama kwamba wewe ni polisi?.
 
Yuko bize na kuandika maujinga mkewe watu wanafumua marinda kama hawana akili nzuri..ni malayaaaa mbwaaa mpaka madogo wa bajaj kule ubungo riverside wanampakua lenyewe lipo tu kazi kujipaka cream.,

Nyinyi ndio mnaharibu hili jukwaa kwa lugha zenu za vyooni.Tatizo lenu hampendi watu waandike kile msichotaka nyinyi kukisikia, kila mtu yupo huru kuwasilisha mawazo yake, kwanini usijibu bango lake badala yake unamshambulia mtu maisha yake binafsi?huu sio ujanja ni ujinga!.
 
Wewe pia mjinga sana..unanishambuliamimi badala ya jerry muro..

Sent from my VIE-L09 using JamiiForums mobile app
 
Ndio maana mnaendelea kutawaliwa na Mbowe coz mmejawa na uvivu wakusoma mambo mengine,mawazo mgando ptuu
Mbowe ndo anatulipia ada na kuwaleta waalimu mashuleni shwetani kabisa ww,we umetawaliwa na mwenye viwanda vya maboksi mpk leo utanambia nn?
 
Mwandishi Mwizi, mnafiki ni janga la kitaifa. Mwandishi atamiliki vipi Pingu!

J Muro Nisaidie hapa inakuwaje? Tuache unafiki.
 
Nakumbuka Wakati Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akishirikiana na Waziri Mkuu ambae nae ni Marehemu Mzee wetu Edward Moringe Sokoine, baadhi ya wananchi walilalamika sana kutokana na Viongozi hawa kupambana na Rushwa na Ubadhirifu wa Mali ya Umma,

Naambiwa ilifikia mahali wahujumu UCHUMI walikana Mali walizonazo na wengine KUZITUPA majalalani zile zilizoweza kutupika, walijitahidi Kujenga taifa la Kizalendo, taifa lenye Umoja wa dhati Misingi ambayo tumeendelea kuitumia mpaka Leo wakati ambao Misingi hiyo imeanza kuweka NYUFA, inataka KUBOMOLEWA na Mataifa Makubwa kwa KIVULI cha kukwapua RASILIMALI zetu.

Mungu sikuzote ni mwaminifu na wa HAKI, baada ya Kilio cha Muda Mrefu Kutoka kwa Viongozi wa Dini, wanasiasa na wananchi kuhusu kukithiri kwa Vitendo vya KIFISADI, Mungu AMEJIBU maombi tena amejibu kwa MOTO, ametuletea Rais Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli anepita Katika NYAYO za Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, ametuletea Mhe Kasim Majaliwa Kasim waziri Mkuu Mzalendo anaefuata NYAYO za Marehemu Edward Moringe Sokoine, hii ni HESHIMA kubwa sana kwetu kuwa na Viongozi wa Haina hii.

Nilijaribu kufanya Udukuzi kidogo wa Taarifa zao za Benki Nilishanga kuona Kiasi KIDUCHUU cha fedha zinazotokana na Mishahara yao, nikadadisi tena kwa watu wao wa KARIBU nikaambiwa Mishahara yao ikiingia tu Benki Hutolewa kiasi kidogo kidogo kwa Ajili ya Kuchangia HARAMBEE za Ujenzi wa SHULE, ZAHANATI na wakati Mwingine kusaidia kununulia Magari ya Wagonjwa na Kiasi kinachobaki hutumia Na familia Zao.

Niliamua Kudadisi Tena Maisha ya Ndugu zao wa Karibu Ndugu Wa Kuzaliwa Tumbo moja, watoto wao, Mashemeji zao na majamaa na Marafiki zao nikakuta idadi kubwa Wanaishi Maisha ya kawaida kama sisi uku Ubungo Maziwa, watoto wao wanasoma Shule za Msingi na sekondari kama wa kwetu na Juzi juzi Niliona Mtoto Mmoja wa Mhe Rais amepata Udahili wa Masomo ya Shahada ya Uzamili katika chuo cha Tanzania, tena kiko Mkoani na Sio Mjini

NIKAENDELEA kumtukuza Mungu mana VIONGOZI hawa MATENDO yao yanaakisi Maisha yetu, hapa nimeona utofauti ambao umewafanya hata baadhi ya Wasaidizi Wao kuwarejesha watoto waliokuwa wanasoma UGHAIBUNI, tumeona uwiano wa Maisha ukianza Kurejea, waliochini taratibu wanaelekea katika Uchumi wa Kati kwa Kufanya kazi kwa BIDII kupitia Mapinduzi ya Viwanda iwe Ujenzi wa Viwanda Vikubwa mfano Kiwanda cha Kutengeneza SUKARI kule Mbigili vitakavyozalisha Ajira, na kuchangia mapato ya serikali kupitia KODI, viwanda vitakavyozalisha BIDHAA kwa ajili ya soko la Ndani hali itakayofanyika bei za bidhaa hizo kushuka mana zitakuwa Nyingi Sokoni, bidhaa zingine zitauzwa Nje ya Nchi (export) tutapata fedha za kigeni na Kuimarisha Shilingi dhidi ya Dollar.

Nimejifunza mambo mengi sana ambayo ya nazidi kuniimarisha katika SIASA, nimejifunza jambo moja kubwa, HAIJAWAI KUTOKEA TANGU ENZI YA UTAWALA WA MWALIMU NYERERE MPAKA LEO MHE MAGUFULI NIKAONA AU KUSIKIA RAIS ANAPONGEZWA.

1. Enzi ya Nyerere walimsema sana kuwa ni dikteta, kasababisha maisha Magumu lakini Alipofariki ametangazwa "Mtakatifu "na hotuba zake zinanukuliwa kila siku.
2. Mzee Mwinyi walimsema sana mara Anauza na kugawa mpaka tausi wa Ikulu wakampachika mzee wa Ruksa, japo walikudhihaki Leo WANAKUKUMBUKA wanatamani hata Ruksa Kidogo tu ya KUKWEPA KODI.
3. Mzee Mkapa wakalalamika maisha magumu sana wakamtundika jina la "UKAPA" wakasema amechukua migodi, kapewa pande la DHAHABU maneno Lukuki, Leo wanamuota na Kusema Heri ya UKAPA kuliko HAYA
4. Mzee Kikwete, huyu sihitaji hata kusema, walimdhihaki sana nadhani kuliko Rais Mwingine yoyote Tanzania, Mara ufisadi umeongezeka, mara mwanae Anauza UNGA, mara nchi haina Rais iko AUTO pilot, Mara Rais LEGELEGE, wakasema sana, ila nikashangaa Siku Mzee Kikwete amemsindikiza "MAMSAPU" kuapishwa Bungeni wale wale bila AIBU walilipuka SHANGWE na NDEREMO na kumwambia TUNAKUKUMBUKA MZEE, nilishangaa sana nikasema hivi hizi ndio SIASA za Tanzania KWELI?

Mzee Kikwete akabaki kuwacheka sana, najua alikuwa ANAWAZOMEA MOYONI mana alijua pamoja na mitusi yote ile "WALIKUMBUKA SAMBUSA NA JUICE TU " Ni sawa na wana wa Israel kukumbuka MANA za kule Misri.

Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, mama Samia Suluhu Hassan na Kaka Yangu Mhe Majaliwa Kasim Majaliwa siku mkiondoka MADARAKANI nawahakikishieni lazima hawa wanaowatukana WATAWATANGAZA nyinyi WATAKATIFU na mashujaa wa Tanzania, subirini mtaona kwa MACHO yenu, miaka nane sio MINGI, Subirini mtaona.

Urais Tanzania ni MATESO, Ngoja ninukuu alichosema Mwandishi mwenzangu Chakubanga hapa kidogo

"..... Kauli ya JPM kwamba "Urais ni mateso" inanikumbusha kauli ya Masiha wa Bwana aliposema"Ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke" Na hata pale Msalabani Calvary aliposema "Ee Baba Mbona umeniacha".

Kibinadamu Ni Kauli zinazoonesha kufikia mwisho wa uwezo wa kibinadamu,lakini kiimani ndipo Safari inapoanzia kuelekea kupita uwezo wa kawaida wa mwanadamu na kuweza kuandika historia,Kwa kiingereza "beyond human knowledge and ability,that's an exceptional case".

Masiha ni Mteule Kwa jina lingine ni Mkombozi,Neno hili linatokana na ushindi ama kuwashindia wenzako vita,ama hatari iliyokuwa inawanyemelea ama kuwakumba, Mara chache dunia inapata kuwashuhudia wakombozi katika jamii zao na katika vitabu vya dini tunapata kuona neno masiha, na kuliendana na kusulubiwa na kwa Masiha kusulubiwa msalabani kulimaanisha kuukomboa Ulimwengu, hivyo tunaipata picha ya kwamba changamoto zinapozidi na bado kila sensi inakutaka kuendelea na changamoto hizo basi wewe ni masiha Kwa maana nyingine ni Mkombozi.

Kuna story moja ya Paulo akisema "Baba mwiba katika mwili wangu" na Baba alimjibu "Neema yangu yakutosha" Ooh kumbe unapopewa mwiba katika mwili wako au Changamoto zinapokuzidia kuna neema ambayo inaweza kukutosha kukupitisha kwenye changamoto hizo na ukatoka ukiwa imara zaidi ya ulivyokuwa Mwanzo na ikawa msaada kwako kuweza kukuimarisha na kukusaidia kuishinda vita ambayo iko mbele yako,kumbe kila changamoto Kwa neema itakuimarisha na kukufanya kuwa shujaa,hatasinzia yeye akulindaye Kwa maana unatenda si Kwa kujikomboa wewe bali kulikomboa Taifa,Maana iliandikwa utakuja mteule wa kuweza kuyapitia haya ili kuweza kujenga msingi wa Taifa imara Kwa ajili ya kizazi hata vizazi vijavyo,Nikutie Moyo husiogope hata kila mtu anapocontradict the fact just believe in what you are doing,Kwa maana ndiyo njia pekee ya kulikomboa Taifa,ilitupasa kuipita njia hiyo miaka 20 iliyopita ila wengi tulichagua shortcut lakini kumbe hakuna shortcut na inatupasa kupitia kila changamoto ili tuweze kulijenga Taifa imara la Tanzania Kama Wachina walivyopitia Haya yote hata kuipata China ya Sasa ambayo ndilo Kilanja wa Dunia Kwa Sasa baada ya decade ya Marekani kuisha.

Baba wa Taifa, Mwl Nyerere aliwahi kusema "Urais si lelemama" akimaanisha "Urais ni mateso" Kwa mtu makini utakubaliana Na Hayati Mwl Nyerere na pia utakubaliana na Mh Rais Magufuli hasa inapokuja kuwa na timu imara unayoijua na kuiamini ili kuweza kukusaidia kutimiza majukumu ambayo ni ya juu na ya mwisho ya kuweza kulisaidia Taifa kusonga mbele,yakupasa kutenda Kwa kadri ya uwezo wako wote hata uwezo wa mwisho kabisa kulisaidia Taifa Kwa maono na mipango hata kuweka historia.

Kwa mtu makini hasa anayechagua kupita ile njia halisi ya kuelekea mafanikio lazima atawaza usiku na mchana na pengine kulala masaa manne hadi sita kuwaza na kuchanganua namna ya kulisaidia Taifa,kutengeneza maisha ya vizazi vitatu mbele baada ya kizazi chetu kupita,wengi wanawaza urais ni kula bata tu lakini Kwa mtu makini Urais ni kazi ambayo inakuhitaji kutenda hata uwezo wako wa mwisho,changamoto zitakuja hasa unapovunja miundo mbinu ya walaghai,walafi,wanadhirifu,wasio na uadilifu,mamwinyi na miungu watu,wauaji,wahuni,wezi,mafisadi,wanasiasa matapeli na wasio wazalendo Kwa Nchi yao,Vita itakuja zaidi wewe Kama Rais unapokuwa mwadilifu na hivyo kufanya system yote kuwa ya kiuadilifu,wengi watapenda husiendelee kuwepo

Kwa kuwa umeingilia anga zao na wizi wao,lakini Kwa kuwa imeandikwa atakuja masiha (mkombozi) ambaye sistahili hata kufunga gidamu za Viatu vyake,yeye ndiye atayepita njia ile ambayo watangulizi wake wameikwepa,Mteule huyo atapita miba ikimsonga,na pengine Mbwa mwitu kumzonga lakini atapita ili kuiongoza Tanzania kuelekea Tanzania ya maziwa na asali kuweza kuipata "The Great Tanzania" ambayo Mungu aliibariki kuwa Taifa tajiri lenye utajiri wa Mali ya asili lakini wahuni waliifanya ni Shamba la Bibi.

Kama ilivyokuwa miaka ya 1960 upepo wa Uhuru ulipovuma Afrika basi Sasa upepo wa mabadiliko ya kiuchumi unavuma tena Afrika na hasa kimbunga kikionekana Tanzania,vumbi litatimka lakini mwisho wa siku tutaipata Tanzania ya Viwanda,Tanzania ya Uchumi wa Kati ,Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika.

Mwandishi wa Makala hii ni Mwanahabari mwandamizi za Uchunguzi kwa Kipaji (talented) pia mtaalamu wa Uongozi wa Biashara na Masoko (kitaaluma) Mwenye Shahada ya Uzamili (Master Degree) MBA (2015)
Simu ya Mkononi : 0785333999
Barua pepe : jerrymuro98@gmail.com

Pia Makala hii Imetoholewa kutoka kwa Msemakweli Chakubanga.

Mkuu Pamoja na Uchambuzi wako mreefu lakini bado hujamfikia HAJI MANARA, mabadiliko ya MA-DC Bado kaka subiri labda 2020
 
Sikujua kama jerry muro una upeo wa juu wa uelewa kiasi hiki .Utatukanwa kukejeliwa lakini ukweli utabaki palepale kwa mahala nchi yetu ilipokuwa imefika Magufuli ndiye suluhisho , zingine zote kelele na ukosefu wa kumbukumbu ya jinsi mambo yalivyokuwa yakiendeshwa vibaya serikalini miaka michache iliyopita.
 
Back
Top Bottom