Jerry Muro: Simba si washindani wetu tena

GREGO

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
4,279
2,913
Tamko hilo limetolewa hii leo na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa wanajangwani hao Jerry Muro wakati akitoa salam za pongezi kwa wachezaji, benchi zima la ufundi na wanachama kwa kufanikisha kile walichokifanya Jumamosi iliyopita kwenye mtanange wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara walipoinyuka 2-0 Simba.

Aidha Muro ameongeza kuwa kwa sasa wanachotazama ni shughuli tatu zilizo mbele yao mechi ya kombe la shirikisho dhidi ya JKT Mlale, mchezo wa klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Cercke de Joachim ya Mauritius na mechi dhidi ya Azam ikiwa ni ya ligi kuu Tanzania Bara.

Aidha amesema kuwa kikosi cha Yanga kimeanza mazoezi katika uwanja wa chuo cha polisi Kurasini kwa ajili ya mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya JKT Mlale Jumatano na mara baada ya mchezo huo kitaendelea na maandalizi ya mechi ya marudiano dhidi ya Cercle de Joachim.
 
Wajenge kiwanja. hawaoni aibu hata jeshi la polisi ambao michezo siyo jukumu lao la kwanza lakini wana uwanja angalau wa mazoezi.
 
wako wapi wasemaji wa mwanzo wa hizo timu kongwe ,hazina shukran time will tell
 
mwaka huu tutatukanwa sana kila aina ya matusi kwa sababu ya kujitakia. niliangalia dakika ishirini za mwanzo nilijua yanga hachomoki. ila ujinga uliofanywa wa kucheza rafu za mbili za hovyo kabisa kwa mchezaji ambaye amecheza VPL kwa zaidi ya miaka 3 mechi iliishia palepale. Pamoja na mapungufu kidogo ya mwamuzi lakini simba tulijimaliza wenyewe mapema kwa kadi nyekundu ya mapema.
 
Pressure ya mchezo mkuu ilimfanya atende yale, ila pia kwa goli la kwanza kulikua na uzembe kama sio kutojiamini kwa beki wenu
 
nakubaliana na wewe engineeer huwa inatokea pressure ya mchezo lakini kwa mchezaji ambaye ameshakutana na yanga na simba mara kibao akiwa coastal union. pia ameshakutana na yanga akiwa simba na akacheza kwa utulivu mkubwa hiyo pressure ilitoka wapi tena.
 
Kuna msemo unaosema "Binadamu kumla samaki hutasikia watu wakiongea ila samaki akimla binadamu dunia nzima itapata habari"
 
Huyu atakuwa mwehu si bure,tumewafunga miaka kadhaa hadi mashabiki wao walisusa kwenda uwanjani maana walijua wakienda watarudi huku wakisononeka leo wameshinda mechi mbili anaanza kulopoka!
Toka club zianzishwe wamekutana mara ngapi? Timu ipi imeshinda mara nyingi zaidi? Timu ipi imechukua ubingwa wa nchi mara nyingi?
 
Toka club zianzishwe wamekutana mara ngapi? Timu ipi imeshinda mara nyingi zaidi? Timu ipi imechukua ubingwa wa nchi mara nyingi?
Shangaa na wewe kaka, katika mechi zote za Simba na Yanga, Yanga kashinda mara nyingi zaidi.
 
Hiyo si hoja,kilicho wazi kwamba mara zote timu hizi zikikutana hakuna mwenye uhakika wa ushindi,ngojeni siku yenu ikifika ndio mtamtimua yule ponjoro na huyo kibaraka wake
Lini hiyo mkuu?
 
Ukiamua kufanya kazi na Simba au Yanga lazima akili zako uziache nyumbani ili maisha yaendelee jifanye chizi tu hata kama watoto wako watakushangaa wakikuangalia kwenye Tv jambo la msingi ni kuingiza siku.
Lakini huyu kama amezidi aisee
 
Hiyo si hoja,kilicho wazi kwamba mara zote timu hizi zikikutana hakuna mwenye uhakika wa ushindi,ngojeni siku yenu ikifika ndio mtamtimua yule ponjoro na huyo kibaraka wake
Hoja ni kwamba rekodi zinaonesha timu gani imepoteza mara nyingi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom