GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Katika hali inayoonyesha kuwa kama hali hii haitadhibitiwa haraka na upesi na Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Serikali na Wadau kuna siku tutashuhudia dhahama kubwa nchini Tanzania katika Sekta ya Michezo itakayosababishwa hasa na Msemaji wa Klabu ya Yanga Jerry Muro ambae anaonekana hapa Tanzania yeye ni mtu wa nne kwa umuhimu baada ya Rais, Makamu na Waziri Mkuu.
Huyu msemaji wa Klabu ya Yanga kila mara amekuwa akija na kauli chafu, mbaya na za dharau dhidi ya mwenzake wa Klabu ya Simba Haji Manara.
Mimi siyo mdau wa mpira wala mfuatiliaji wa mpira na sina hata Klabu ninayoishabikia hapa Tanzania zaidi tu ya Timu Za Taifa ile ya Taifa Stars na Twiga Stars ila nimeguswa kama mtu ninayependa jamii yenye MAADILI.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida akizungumza muda mfupi tu na Kituo cha Redio ambacho kwa 90% kina MAHABA ya wazi na Klabu ya Yanga na kupenda kuwa na CHUKI ya wazi na Klabu ya Simba cha E FM leo Jerry Muro kasema nanukuu " Mtu mzima na akili zako tena Mtoto wa Kiume unaacha kufanya mambo yako kutwa UNAWASHWA WASHWA na kuzunguka huku na kule kuzizungumzia Yanga na Azam kama siyo anataka KUKUNWA huyu anataka nini? " mwisho wa kumnukuu Jerry Muro.
Kama wewe unajijua ni Mdau wa Michezo na Mwana Michezo tafadhali toa maoni yako hapa ya nini kifanyike ili hali hii IKOME au IISHE kabisa kwa maslahi mazima ya mchezo wetu pendwa wa Soka au Kandanda.
Karibuni sana tujadili.