Jenista Mhagama: Wizara zote zatakiwa Dodoma kabla ya Feb. 28

Reucherau

JF-Expert Member
Nov 26, 2014
756
1,740
19th Jan, 2017

Serikali imezipa msisitizo wizara mbalimbali kuhakikisha zinahamishia makazi yake Makao Makuu ya nchi mkoani Dodoma kabla ya Februari 28, mwaka huu, kama iliyotangazwa na Rais John Magufuli mwaka jana.

Mhagama1.JPG

Waziri Jenista Mhagama

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Ulemavu, Jenista Mhagama, alisema agizo la serikali lazima liwe limetekelezwa ifikapo Februari 28, mwaka huu.

“Kama agizo lilivyotolewa na Rais Magufuli kuhusu wizara na watumishi wake kuhamia Makao Makuu Dodoma, ndivyo wanavyotakiwa manaibu makatibu wakuu, makatibu, manaibu mawaziri na mawaziri kutakiwa kuwapo Dodoma mwishoni mwa Februari,” alisema Mhagama.

Waziri Mhagama alisema ofisi yake imeweza kukagua miundombinu na ujenzi wa majengo mbalimbali ya serikali yanayoendelea kujengwa na mengine yakiwa yamekamilika kwa ajili ya matumizi ya wizara hizo.

“Hakuna tatizo la ofisi za watumishi wa wizara zote, kwani majengo yamekamilika na yapo katika hali nzuri tayari kwa ajili ya kuanza kutumiwa, hivyo wakuu husika wakiwamo mawaziri wahakikishe wanatakiwa kuhamia Dodoma,” alisema.
 
Huyu mjane wa SS atulizane! Bwana wao ana stress za mapato less anatamani kuikodisha hii nchi kwa Dangote au Azam yeye anaongea upuuzii!!!!!! Kwa bajeti ipi na hela ipi ?? Wanahaha kukopa ndani na nje.....yeye analeta upuuzi! Hata kama hajui kusoma picha pia haoni na kuelewa???
 
Kwa hiyo wizara na mawaziri wote wakihamia Dodoma wakati mtakatifu yuko Dsm watakuwa wanafanyaje vikao vya baraza la mawaziri na mambo mengine yanayohitaji physical presence ya rais na waziri?
Au ndiyo zitakuwepo safari kama za Majaliwa kila siku sasa?
 
ofisi anasema zipo tayari na hao watumishi wanaenda kuishi juu ya miti au?
Kwa mujibu wa falsafa ya mkuu wao hajakosea kabisa: kwa faru miundombinu ya serikali ni muhimu na inatosheleza kuwa kielelezo cha maendeleo hata kama wananchi hawana makaazi ya kuishi.
 
Back
Top Bottom