ibesa mau
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 2,109
- 1,697
Pengine labda kwa ajili ya ukosefu wa semina elekezi, huyu waziri hajui majukumu yake ni yepi yaliyopo katika wizara yake. Mara ya kwanza nilimsikia akimfukuza kazi mkandarasi mmoja aliyekuwa anajenga mfereji Dar-es- Salaam, lakini mkurugenzi akamtetea mkandarasi huyo kwa kumwambia hana fedha za kumlipa mkandarasi mwingine kwa sababu mkandarasi huyo ameshapewa fedha zaidi ya 70%, hivyo akamwambia mkandarasi huyo amalizie kazi yake.
Lakini jambo la pili ni hivi majuzi akiwa mkoani Singida, alikuwa anatoa maagizo kwa wasambazaji wa chakula kwa watu walioathirika na njaa mkoani humu, maagizo ambayo kimsingi yalikuja kutofautiana na yale yaliyotolewa na waziri mwenye dhamana ya kilimo.
Nadhani labda hajapewa job description ndio maana anakurupukia wizara za wenzake. Lakini si hivyo tu, Jenista amekuwa ni mtu wa kimbelembele tangu zamani lakini ni mtu mwenye uwezo mdogo wa kumudu majukumu ya kiuwaziri.