Jengo la Tanganyika- jijini Mwanza

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
23,372
54,909
Nawasilisha.

Kuna maeneo ukiyataja tu basi watu hushituka sana kwa umaarufu wake na maeneo mengine yamekuwa na umaarufu wenye maana nzuri ila mengine ni maeneo yenye umaarufu wa maovu.

Katika jiji la Mwanza kuna jengo lipo maeneo ya Sahara na limeanza kujizolea umaarufu kwa kuuza smartphone ambazo kwa kiasi kikubwa ni za wizi. Jengo hili lipo mkabala na sahara au (stand ya mjini) ambayo ina daladala za kwenda Airport.

Nilipata kufanya uchunguzi wangu wa Muda mfupi na nilibidi kufukua makaburi ili nijue hii biashara ambayo ina sintofahamu, Nilitafuta mawasiliano ya mmoja kati ya watu maarufu ambao wamekuwa ni wauzaji wa simu na kiukweli wanajulikana sana hapo mjini.

Nilikubaliana nae kunitafutia aina fulani ya simu na aliniahidi kuwa atanijulisha baada ya muda mfupi na siku chache alisema haijapatikana na kunitajia baadhi ya simu ambazo alikuwa nazo, Jengo lile lina maduka ya nguo na bidhaa kadhaa ila sehemu kubwa ni maduka ya nguo na ukiingia mle biashara inafanyika kama wauzavyo madawa ya kulevya ni hadharani unachukua simu yako unalala mbele kimya kimya bila wasiwasi.

Nini nilijifunza:

Kuna mafundi simu ambao ni wadau wa hawa wauzaji simu wapo nje ya jengo na hawa hutumika vizuri sana kuflash simu zinazokuwa na security code, Pattern,PIN, password n.k na ukipita pale utakuta vijana wako pale wengine hawana kazi na wanapiga hizo biashara za uuzaji wa simu zenye viulizo vingi, ukionekana unashangaa shangaa pale kuna ishara wanatumia na pia wanamsoma mtu kufahamu nini shida yake na muda mwingine wanakuuliza unataka mzigoo???

Kwa wakazi wa Mwanza kama utapata tatizo la kuporwa simu hebu tembelea hayo maeneo kwa umakini unaweza kununua simu yako kwa awamu ya pili ila pia jeshi la polisi lifanye upekuzi hapo watajua mengi zaidi.

Hii ni sehemu niliyoiweka sana kichwani wakati nilipokuwa kwenye mji wa Mwanza.....

Asanteni.......
 
nimekuja haraka nikijua bashite kalinunua, daaah

Back
Top Bottom