chama amini usiamini huenda gharama za mradi huo ni robo tu ya gharama ambazo tunaambiwa. Nchi hii imefika pabaya.Katika hizo gharama za ujenzi viongozi wa jiji walikula kiasi gani? Haya ni matokea ya wakubwa kushinikiza miradi ambayo haina faida ulaji ulianzia NSSF hadi jiji; ukweli kabla mkopo haujatolewa NSSF waliupitia mradi ili kuona namna gani wataweza kurudisha pesa zao ulaji uliwafanya wafumbe.
Chama
Gongo la Mboto DSM
Nikiliangalia lile jengo huwa nashangaa sana wale walioshauri kuweka vile vizimba ndani ya jengo.
sera mbovu za ccm utazijua tu. Bilioni 12 si zilitosha kuboresha miundombinu katika baadhi ya vijiji na kuwafanya vijana kubaki huko wajiajiri? Hata hivyo bado hawajachelewa wala kupata hasara. Lile jengo walibadili kwa kuliwekea parking za kukodisha pamoja na ofisi na kumbi za kukodisha. Hiyyo biashara ya machinga haitakaa ifanyike hapo kwa ufanisi.
Labda kama kuna mtu anaweza kutusaidia swali moja; NSSF inaongozwa na sera au taratibu gani kabla ya kuamua kuwekeza fedha za mfuko huo kwenye miradi mbalimbali? Kwa mfano, ni kitu gani kiliwafanya watoe fedha kwa mradi huu wakiamini kuwa utawarudishia faida?
here we go again .... mwanakijiji vs NSSF ... Dr. Dau kakufanya nini..?
Ahadi ni majengo matano mengine kama hayo ktk mikoa mingine mikubwa !Ritz Ukisikia uvivu wa Viongozi kufikiria ndiyo hule.....hivi ukiwauliza hao waliotengeneza hivyo vizimba waliwasiliana na hao wamachinga kama walikuwa wanavihitaji au lah!utasikia.
Labda kama kuna mtu anaweza kutusaidia swali moja; NSSF inaongozwa na sera au taratibu gani kabla ya kuamua kuwekeza fedha za mfuko huo kwenye miradi mbalimbali? Kwa mfano, ni kitu gani kiliwafanya watoe fedha kwa mradi huu wakiamini kuwa utawarudishia faida?
Hii 'movie' kama naiona inapoelekea vile! Jiji 'wanashindwa' kulipa mkopo, NSSF wanaamua kuuza hilo jengo pamoja na mali nyingine za jiji zilizowekwa kama collateral, waliofanya jiji lishindwe kulipa wanajitokeza kununua majengo na mali hizo kwa bei wanayotaka kwa kutumia pesa ya mkopo kutoka NSSF tena! . Dili limekamilika. Jiji limepoteza na NSSF pia inapoteza kwa kushindwa ku recover sehemu ya mkopo na riba! Maisha yanaendelea. Nani kasema bongo si tambarare!!!!!?
Kimahesabu kwa wapangaji 5000 @TShs 60,000= 300,000,000 kwa mwezi hii inafanya jumla ya TShs. 3.6 billion kwa mwaka. Assume gharama za kusimamia jengo ni 10% i.e. 30,000,000 Halmashauri ya Jiji ina uwezo wa kulipa si chini ya TShs. 250,000,000 kwa mwezi.
Deni linalipika ndani ya miaka kumi; unless pesa zinaingizwa kwenye kulipana posho.