Huko kwingine wanakotaka kwenda kumhubiri Yesu nje ya kariakoo ambako hajahubiriwa ni wapi? Hebu tuondoleeni uvivu wa kufikiri hapa. Labda kama mnataka kurudi vijijini mwakwenu mlikozaliwa huko ningeweza kukubaliana na ninyi kwani injili haijaenea kwa kiwango cha kurizisha. Lakini kama ni hapa Bongo bado itakuwa mnadumisha kale ka mradi ka kuwezeshana kimapato na wala sii injili. Kwani hao waumini ni wa pasto wa hapo kariakoo au ni wa Bwana. Na kama ni wa bwana kwanini wasitawanywe ktk makanisa ya hapa Dar na mchungaji na watenda kazi wakaanza kazi ya kuwaleta kondoo wapya zizini hapo kariakoo? Au anahofia kupoteza jembe(mtaji) makanisa ya kipentekoste kwa jinsi nilivyoyastady hakuna mchungaji anaemwamini mwenzake. Unaweza ukafikiri kila mchungaji ana mungu wake anaetofautiana na wa mchungaji mwingine. Na mara nyingi utawasikia wakijinadi kwa kutumia neno Mungu wangu na akubariki. Na hiyo inatendaka kwa shabaha mahsusi ya kulenga kwamba mungu wake na wa mwingine ni tofauti na hawaaminiani. KANISA NI NINI? NA NI NANI ANADANGANYA KUWA KANISA NI MCHUNGAJI NA VIONGOZI NA HIVYO KUWAMILIKISHA UTASHI WA WAAMINI NA KUJIWEKA MAHALA PA UPATANISHI KATI YAO NA MUNGU MAHALA PA BWANA YESU? Acheni hizo hamnayo damu iwezayo kuwa dhabihu madhabahuni pa mbinguni ila ya Yesu. Hakuna cha papa, kadinali, askofu,mchungaji mzazi wala mnyenyekevu awae yeyote, wote tumekuja duniani kwa njia ile ile moja.