Jengo la ghorofa 16 Manispaa ya Ilala kuanza kubomolewa leo

Jengo la ghorofa 16 Manispaa ya Ilala kuanza kubomolewa leo

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
ghrofa.jpg

Mafundi wa Kampuni ya Patty Interplan, wakifunga vyuma maalumu kuzunguka jengo lenye urefu wa ghorofa 16 lililopo katika Mtaa wa Indira Gandhi Dar es Salaam jana. Picha na Venance Nestory
​

Kwa ufupi
Ubomoaji utakamilika kwa kipindi cha miezi mitatu

Dar es Salaam,
Jengo la ghorofa 16 lililopo Mtaa wa Indira Gandhi, wilayani Ilala limezungushiwa nguzo ili kurahisisha kazi ya ubomoaji inayoanza leo.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Patty Interplan iliyopewa kazi hiyo kwa gharama ya Sh1 bilioni, jana walionekana wakizungusha nguzo hizo.

Mwezi uliopita, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alitoa siku 18 kwa uongozi wa Manispaa ya Ilala kubomoa jengo hilo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngulumi alisema kazi hiyo imeshaanza na inatarajia kukamilika katika kipindi cha miezi mitatu.

“Kufunga nguzo ni maandalizi lakini kazi ya kubomoa itaanza kesho (leo) ili kutekeleza agizo la Waziri Lukuvi na tumejipanga kuikamilisha bila kuleta madhara kwa binadamu.

“Tunataka kazi hii ifanyike haraka hata kabla ya miezi mitatu ikiwezekana iwe imekamilika kwa sababu kuna baadhi ya majirani wa eneo hili wamelazimika kuhama makazi yao,” alisema.

Mngulumi alisema gharama za ubomoaji zitalipwa na mmiliki wa jengo hilo ambaye ni Ali Raza Investment.

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omar Kumbilamoto alisema jengo hilo lilikuwa hatarishi kwani lipo kwenye eneo lenye shughuli nyingi za kibiashara.

“Mtaa wa Indira Gandhi na Morogoro una watu wengi hivyo ghorofa likiwa limejengwa chini ya kiwango linaleta wasiwasi kwa wapitanjia,” alisema Kumbilamoto.

“Unajua wakati wa kubomoa hatari yoyote inaweza kutokea hivyo familia nyingi zimehama kwa ajili kujiepusha na maafa ambayo yanaweza kutokea,” alisema mmoja wa wafanyabiashara katika eneo hilo.

CHANZO: Mwananchi
 
Uandishi wa kibongo ni wa kuchochea mihemko ya watu tu!! Sasa hio bilioni hawa wabomoaji ni freelancers na hio 1b wanagawana wenyewe au hio 1b inalipwa kampuni ambayo ndio imepewa tenda ya kubomoa? 😕
 
loh one b kuboa tu 😛
Dada unachanganyikiwa
107170.jpg
hata mm naweza kubomoa kwa milioni 20 tu na kifusi wanielekeze nikamwage wapi hata Baharini nitakiuza tu kwa Manji
 
ukisema shilingi bilion 1 itaonekana ni ndogo, sema milioni elfu 1 za kitanzania.
 
Hapo kuna watu wamechukua 10%, ngoja mzee wa pushups afuatilie
 
Mtoahela zake ngapi kwenye hiyo b1? Maana inashangaza kubomoa tu kiasi hicho takukuru mchunguzeni huyo mtoa hela wa ilala
 
Tunaomba kujua thamani ya hilo jengo hadi hapo lilipofikia ili kuona ni jinsi gani njia zisizo sahihi zinavyoweza kumgharimu mtu. Weka uzembe figisu mbali na kids
 
Back
Top Bottom