Hornet
JF-Expert Member
- Apr 29, 2013
- 26,892
- 52,492
Habari ya wakati huu wanaJF?
...katika maisha ya kila siku kuna mambo mengi yamekua yakitokea kwa watu waliopo kwenye mahusiano ya kimapenzi,mambo haya yanaweza kuwa ya kufurahisha na pia ya kuhuzunisha..
..kero na makwazo pia ni sehemu ya maisha kwa kuwa ukiwazacho wewe sicho akiwazacho yeye..
..sasa basi,nimegundua kwamba mawasiliano ni muhimu sana baina ya watu wawili katika nyakati zote mbili(furaha na huzuni)..
..ili kuweza kutatua tatizo linaloleta huzuni ni vyema kukawa na masikilizano..
..kwa mfano,mwanaume anapokosea na kutenda kitu cha kuhuzunisha na kukera katika mahusiano,mwanamke anapaswa kutulia na kuuliza sababu ya hicho kitendo..
..lakini pia mwanaume anapaswa kutulia na kutoa maelezo stahiki na sio kuhamaki na kupaza sauti..
..katika maisha ya sasa watu wengi wamekua wanashindana kwa kauli na ubishi umekua mwingi..jambo hili limefanya mahusiano/ndoa nyingi kuwa chungu..
...penda sana kusikiliza inasaidia kuujua undani wa tatizo..pengine wewe ndio chanzo cha tatizo!..
...kwa mwenye maoni tofauti anaweza akanikosoa..
...kila la kheri katika ujenzi wa mahusiano bora na imara!